Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Sababu tunakosea ba hatujakamilika mlango wa toba uko wazi muda wote.
kutokana na kauli hiyo uliyotoa. nikisema Mungu kakusudia kumuumba mtu ili akafanye makosa nitakuwa nakosea?
Si kweli hapa inabidi uthibitishe kauli yako, si uishie kusema tu.
Ndiyo maana tunaambiwa kila mwanadamu ni mkosani, na mbora ya wakosaji ni mwenye kutubia.
Mola amemuumba mja ili amuabudu. Hili lina ushahidi.
ukipitia vizuri hizo post tokea awali nilikwambia ya kwamba kitendo cha wewe kukiri kuwa binadamu anakosea kwavile hajakamilika kinathibitisha kuwa Mungu ameumba watu makusudi ili wakosee. Nasema hivyo kwasababu Mungu ni muweza wa vyote hivyo alikuwa anaweza kuumba watu wakiwa wakamilifu wasiofanya hata chembe ya kosa. Au unakataa kuwa Mungu angeshindwa kuumba watu waliokamilika ambao wasingeweza fanya makosa?Soma kwa umakini unachokiandika na ujue wapi ulipoegemea.
Sasa ulitaka nisemaje ? Sasa wapi nimepinga kwamba mwanadamu hakosei ?