Je, harusi ya Adam na Hawa ilifanyikia wapi, nani aliwafungisha ndoa?

Je, harusi ya Adam na Hawa ilifanyikia wapi, nani aliwafungisha ndoa?

Waliambiwa waue wote, wao wakabakiza mmoja, huko si kukaidi? Na kukaidi amri ya Mungu si dhambi? Na kama ni dhambi, huoni ile kauli ya malaika hawatendi dhambi si kweli? Na hivyo kitabu kimejipinga?
Onyesha waliambiwa hayo kwenye kitabu gani kwamba wauwe wote ? Swali langu la msingi ni hili ambalo mwenzako ameshindwa kulijibu.

Ili iwe imejipinga onyesha wapi katika andiko kumeonyeshwa agizo hilo ? Na wao malaika wakafanya kinyume.
 
Wangekuwa na uwezo wangeshaacha. Kitendo cha mtu kuendelea kufanya jambo fulani maanake ameshindwa kuacha. Ukiona kaacha hiko kitendo ujue ameweza kuacha.
Kwa nini tusiseme hajaamua kuacha ndio maana anaendelea ?

Kwa sababu wapo ambao wanakuwa walevi na baadae wanaacha,wakati huo kabla ya kuacha walisema hawawezi kuacha lakini baadae wakaacha.

Sasa mtu kusrma hawezi kuacha sio kweli kwa sababu pia alianza,sasa kama alianza ina maana kabla ya kuanza aliweza kukaa bila hiko kitu.

Kwa maana ya kuwa anaweza kurudi katika hali yake ya zamani ya kutokuanza hilo jambo,nature iko hivyo.

Ukisema umemuoa mwanamke alafu unampenda na kusema huwezi kumuacha au huwezi kuishi bila yeye sio kweli kwa sababu kabla ya kumjua mbona uliishi bila yeye..

Huyu hawezi kutumia hoja ya kuwa anampenda sana ndio maana hawezi kuishi bila yeye,anaweza kuishi bila huyo anaempenda

Hivyo kusema hawawezi kuacha wakati kabla ya kuanza hawakufanya hiko kitu ni dhaahir kuwa wao wameamua kuwa katika hali hiyo.

Sasa ni ngumu kuthibitisha kuwa mtu hawezi kuacha jambo wakati nafsi yake ina uhuru wa kuchagua mambo mbalimbali iweje hili asiweze kuliwacha wakati kabla ya kuanza hakuwa akilifanya.

Kama ingekuwa Mungu anawalazimisha waja wake watende dhambi basi huo moto wa kazi gani si atakuwa anawaonea tu ? H

الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ

[ ANNAJM - 32 ]
Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu.

Ukiangalia aya imeeleza kuwa kuna wale ambao wanajiepusha na makosa ama madhambi makubwa makubwa.

Isipokuwa makosa khafifu yale madpgo madogo ambayo kila mwanaadamu huyatenda kwa namna yake

Hapo ni katika ishara kuwa Mola amewapa watu fursa na uhuru wa kujizuia na madhambi hasa makubwa makubwa kama kuuua kwa makusudi,kumbaka mama mzazi na mengineyo makubwa.

Hapo ni ishara kuwa mja anaweza kutoka na akachagua kujiepusha na mambo kadha wa kadha bila kutenzwa nguvu na Allah
 
“Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”
— Mwanzo 1:28 (Biblia Takatifu)
Kauli hiyo iliwahusu adam na hawa pekeee au ni binadamu wote hadi leo hii?
 
Walifungia ndoa kanisani au msikitini?
Kabla ya swali lako, je una uhakika kulikuwa na kanisa au msikiti wakati huo?

Kama huna uhakika kama vilikuwepo kwanini unauliza hilo swali?

Jibu kinagaubaga.
 
Uta
Utamwaminije mtu usiye muona? Na asiyeweza kukusaidia lolote? Ni akili ndogo tu zinazo amini kuwa Kuna kitu kinaitwa Mungu ,,story za kusadikika tuu
Mkuu, samahani naomba unijibu swali nje ya mada hii. I declare this, ninaamini katika uwepo wa Mungu. Naomba unijibu maswali yangu yafuatayo :-

* Nini asili ya Jua?

Nani/wakina nani walilitengeneza na kuliamuru liangaze kutoka linapotokea na kuzama linapozama?

* Nini asili ya maji?

Naomba tu unijibu hayo PLEASE.
 
Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu.

Ukiangalia aya imeeleza kuwa kuna wale ambao wanajiepusha na makosa ama madhambi makubwa makubwa.

Isipokuwa makosa khafifu yale madpgo madogo ambayo kila mwanaadamu huyatenda kwa namna yake

Hapo ni katika ishara kuwa Mola amewapa watu fursa na uhuru wa kujizuia na madhambi hasa makubwa makubwa kama kuuua kwa makusudi,kumbaka mama mzazi na mengineyo makubwa.

Hapo ni ishara kuwa mja anaweza kutoka na akachagua kujiepusha na mambo kadha wa kadha bila kutenzwa nguvu na Allah
nadhani unashindwa kuelewa point yangu ni ipi. Haya ngoja twende unavyotaka wewe. Naomba hapo ulipoaandika makosa madogo madogo ambayo kila mwanadamu huyatenda. Unaweza kuniambia kwanini iwe lazima mtu ayatende makosa hayo Kama sio ndio asili aliyoumba mwenyewe Mungu?

Mfano mimi ni fundi ujenzi; nimejenga nyumba lakini baada ya kujenga ile nyumba naangalia juu kwenye bati naona kuna matundu ambayo pindi mvua ikinyesha, nyumba itakuwa inavuja na maji kuingia ndani. Hapo nimejua dosari

Lakini baada ya kulijua hilo sijarekebisha bali nimekabidhi nyumba vile vile kwa mteja.

Je hapo huoni kuwa hapa fundi kakusudia nyumba aliyojenga ivujishe maji ndani? Laiti kama angekuwa hajakusudia angerekebisha baada ya kugundua kuwa hii nyumba haipo sawa.

Twende upande wa Mungu:

Mungu anamuumba mtu ambaye kwa maelezo yenu mnasema na kukiri kuwa hajakamilika.
ili Mungu awe hajakusudia kumuumba mtu asiyekamilika kuwa hajafanya kusudi basi niambie kuwa Mungu hana uwezo wa kumuumba mtu aliyekamilika. Kwa maana kwamba kumuumba mtu aliyekamilika ilikuwa nje ya uwezo wake.
Kama uwezo wa kuumba mtu aliyekamilika anao lakini yeye Mungu kwa mapenzi yake kaamua kuumba mtu mwenye sifa ya kutokamilika, basi maanake Mungu mapenzi yake ni kumfanya binadamu awe kiumbe asiyekamilika.

Huku kutokamilika kwa binadamu ndio kunakopelekea kufanya makosa aidha ni madogo madogo au yawe makubwa.
 
Yaani unasema kabisa kuwa mtu hajakamilika halafu bado unakazana kusema umepewa utashi na akili. Je hiyo akili na utashi itasaidia nini wakati haujawa mkamilifu?
Hahaha ndio ujue kuwa hawa waumini wa hizi dini ni vichaa wa akili 😂
 
Waliambiwa waue wote, wao wakabakiza mmoja, huko si kukaidi? Na kukaidi amri ya Mungu si dhambi? Na kama ni dhambi, huoni ile kauli ya malaika hawatendi dhambi si kweli? Na hivyo kitabu kimejipinga?
Huyo jamaa akili hana ni type ya wale watu ambao huwa waabishana tu vijiweni ili muda uende hana fact hawezi hata kutetea hoja zake ilimradi tu anabishana
 
Onyesha waliambiwa hayo kwenye kitabu gani kwamba wauwe wote ? Swali langu la msingi ni hili ambalo mwenzako ameshindwa kulijibu.

Ili iwe imejipinga onyesha wapi katika andiko kumeonyeshwa agizo hilo ? Na wao malaika wakafanya kinyume.
Nimekutolea Mpaka sura jombaa but still unabishana 😂 ngoja nikitulia nakuletea Aya hiyo 😂 idiot
 
nadhani unashindwa kuelewa point yangu ni ipi. Haya ngoja twende unavyotaka wewe. Naomba hapo ulipoaandika makosa madogo madogo ambayo kila mwanadamu huyatenda. Unaweza kuniambia kwanini iwe lazima mtu ayatende makosa hayo Kama sio ndio asili aliyoumba mwenyewe Mungu?

Mfano mimi ni fundi ujenzi; nimejenga nyumba lakini baada ya kujenga ile nyumba naangalia juu kwenye bati naona kuna matundu ambayo pindi mvua ikinyesha, nyumba itakuwa inavuja na maji kuingia ndani. Hapo nimejua dosari

Lakini baada ya kulijua hilo sijarekebisha bali nimekabidhi nyumba vile vile kwa mteja.

Je hapo huoni kuwa hapa fundi kakusudia nyumba aliyojenga ivujishe maji ndani? Laiti kama angekuwa hajakusudia angerekebisha baada ya kugundua kuwa hii nyumba haipo sawa.

Twende upande wa Mungu:

Mungu anamuumba mtu ambaye kwa maelezo yenu mnasema na kukiri kuwa hajakamilika.
ili Mungu awe hajakusudia kumuumba mtu asiyekamilika kuwa hajafanya kusudi basi niambie kuwa Mungu hana uwezo wa kumuumba mtu aliyekamilika. Kwa maana kwamba kumuumba mtu aliyekamilika ilikuwa nje ya uwezo wake.
Kama uwezo wa kuumba mtu aliyekamilika anao lakini yeye Mungu kwa mapenzi yake kaamua kuumba mtu mwenye sifa ya kutokamilika, basi maanake Mungu mapenzi yake ni kumfanya binadamu awe kiumbe asiyekamilika.

Huku kutokamilika kwa binadamu ndio kunakopelekea kufanya makosa aidha ni madogo madogo au yawe makubwa.
UnaongeaUnaongea fact sana but wafia dini wa humu hawawezi kukuelewa
 
Nimekutolea Mpaka sura jombaa but still unabishana 😂 ngoja nikitulia nakuletea Aya hiyo 😂 idiot
Sura uliyo iweka kweli inaelezea kisa cha nabii Adamu, ila haionyeshi hilo agizo kwa Malaika kwenda kuwaua majini wote kisha wakakaidi wakambakiza mmoja. Nachotaka mimi ni hilo agizo na utuonyeshe wapi walipo kaidi.

Kisa kimesimuliwa kuanzia aya ya 30 mpaka 38 katika surat al Baqarah.

Soma hapa :

30. Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua.

31. Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli.

32. Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima.

33. Akasema: Ewe Adam! Waambie majina yake. Basi alipo waambia majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani, na ninayajua mnayo yadhihirisha na mliyo kuwa mnayaficha?

34. Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri.

35. Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio dhulumu.

36. Lakini Shet'ani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyo kuwamo, na tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu na starehe kwa muda.

37. Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu.

38. Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. (al Baqarah : 30 - 38)
 
Hahaha ndio ujue kuwa hawa waumini wa hizi dini ni vichaa wa akili 😂
Naona mmekutana pipa na mfuniko sijui nani atamfunua mwenzake. Yaani kwa mnavyojichanganya kwa kuvamia mambo msiyo yajua, mnajifariji kwamba hatuna akili, sasa jibuni hoja zetu.

Mwenzako anarudia rudia tu jambo ambalo ameshajibiwa akirudi tena kujadiliana na mimi, atizidi kuthibitisha ya kuwa ni kwa namna gani hafikirii na maneno yake mwenyewe hayaelewi.

Hakuna watu wenye akili tangu dunia iumbwe na mpaka mwisho wake, kuzidi watu wa Dini.

Nipo ....
 
Back
Top Bottom