Usijali mijadala kama hii kuelewana ni ngumu sana ndio maana na mimi naendelea kujadiliana na wewe kwa sababu naamini point yangu hujaifahamu pia.
Sawa na mimi baadae nitaenda unavyotaka wewe ili tunogeshe mazungumzo yetu.
Sasa hivi nitajibu kwa kifupi ili iwe rahisi kwako kusoma na kuelewa point ya moja kwa moja.
Ndio Mungu kamuumba binadamu katika asili ya kutokuwa mkamilifu.
Na hapa maana ya ukamilifu ninayoikusudia ni ; kutokukosea kabisa ama kutokutenda dhambi yeyote iwe hafifu ama kubwa.
Hii ndio maana ya ukamilifu.
Sasa Mungu hajawahi kusema kuwa kamuumba binadamu aliyekamilika kwamba hakosei wala hatendi dhambi,yeye mwenyewe anasema kuwa binadamu wote tunakosea na tunatenda dhambi.
Ndio maana
Kuna toba : ili aliyetenda dhambi ajirudi kwa amungu.
Kuna pepo : aliyeacha madhambi aingie huko
Kuna motoni : mfanyaji wa madhambi aende huko.
Laiti kama Mungu angekuwa kwa hakika ameumba mtu mkamilifu asiyekosea basi bila shaka asingesamehe kwa sababu wewe kwa nini ukosee na ni mkamilifu ?
Na kama ingekuwa kamuumba mtu mkamilifu hakosei basi kusingekuwa na haja ya kuwepo kwa moto na pepo kwa sababu watu wote wamekamilika hawakosei,jee motoni angeingia nani wakati watu wote ni wasafi....
Kwa maana hiyo Mungu tokea asili na asili alimuumba binadamu ambaye sio mkamilifu,sio msafi kabisa.
Mungu alikusudia kumuumba mtu ambaye hajakamilika yaani hakosei kwa sababu huko kukusudia kumuumba mtu ambae hajakamilika ndio maana akampa nafsi ambayo inaweza kufanya baya na kuacha,inaweza kufanya mema na kuacha.
Kwa hiyo tafsiri ya Mungu kumuumba mtu ambaye hajakamilika ni kule Mungu kumpa mtu nafsi ambayo inaweza kufanya mema kwa kuamua,na kufanya mabaya kwa kuamua kwa maana nafsi imeumbwa na uhuru wa kufanya ilitakalo.
Na tunaposrma uhuru,kufanya jambo bila kulazimishwa tunapima ama tunajua kwa kuangalia tu matendo yetu ya kila siku.
Ukitaka kufanya jambo huoni kama kuna nguvu yeyote inayokukataza.
Yaani mfano ukitaka kula huoni kama kuna nguvu inazuia mkono wako usile,kutokuwepo kwa nguvu hiyo maana yake ndio uhuru wa kufanya unalotaka.
Kukamika kwa maana ya kutokumpa nafsi yenye maamuzi ya kuchagua mema na mabaya uwezo huu alikuwa nao,
Lakini kumbuka kuwa ili iwe mtihani lazima kuwe na jaribio na ili iwe jaribio kwetu basi tuwe na uhuru wa nafsi,tuwe na nafsi ambayo haijakamilika.
Mungu anaweza kupenda jambo na asilifanye.
Na anaweza kufanya jambo ambalo halipendi.
Kupenda kwa Mungu hajakufungamanisha na kufanya,kwamba akipenda jambo lazima afanye.
Na kufanya kwa Mungu hajafungamanisha na kupenda kwamba akifanya jambo basi lazima iwe amelipenda.
Kwa hiyo unaposema kapenda kufanya hivyo sio sahihi sema kataka kufanya hivyo.
Kama ambavyo mtu huamka mapema na kwenda kupigwa na jua shambani sio kwamba anapenda jua limpige bali kataka kufanya hivyo ili atimize malengo yake.
Kwa hiyo sio sahihi kufungamanisha baina ya kufanya na kupenda.
Sio kila lifanywalo na wahusika basi linapendwa hapanaa.
Kama tulivyoelezana kuwa usiseme mapenzi,sema ametaka.
Kwa hiyo Mungu ametaka kumuumba binadamu ambaye hajakamilika kwa maana ya kuwa nafsi yake ina uhuru wakuacha zuri na kufanya baya,kufanya hiki na kuacha kile.
Huku kuwa na uwezo wa kufanya hili na kuacha lile basi ndio uhuru wenyewe huu.
Na huu uhuru wa nafsi maana yake ndio watu wanautumia kufanya mabaya,na mazuri pia.
Na ndio maanaukamilifu wa kufanya mema tu,kutokukosea akawapa malaika kwa sababu wao sasa hawapo katika miitihani ya dunia,hawapo katika kujaribiwa kabisa.