Wangekuwa na uwezo wangeshaacha. Kitendo cha mtu kuendelea kufanya jambo fulani maanake ameshindwa kuacha. Ukiona kaacha hiko kitendo ujue ameweza kuacha.
Kwa nini tusiseme hajaamua kuacha ndio maana anaendelea ?
Kwa sababu wapo ambao wanakuwa walevi na baadae wanaacha,wakati huo kabla ya kuacha walisema hawawezi kuacha lakini baadae wakaacha.
Sasa mtu kusrma hawezi kuacha sio kweli kwa sababu pia alianza,sasa kama alianza ina maana kabla ya kuanza aliweza kukaa bila hiko kitu.
Kwa maana ya kuwa anaweza kurudi katika hali yake ya zamani ya kutokuanza hilo jambo,nature iko hivyo.
Ukisema umemuoa mwanamke alafu unampenda na kusema huwezi kumuacha au huwezi kuishi bila yeye sio kweli kwa sababu kabla ya kumjua mbona uliishi bila yeye..
Huyu hawezi kutumia hoja ya kuwa anampenda sana ndio maana hawezi kuishi bila yeye,anaweza kuishi bila huyo anaempenda
Hivyo kusema hawawezi kuacha wakati kabla ya kuanza hawakufanya hiko kitu ni dhaahir kuwa wao wameamua kuwa katika hali hiyo.
Sasa ni ngumu kuthibitisha kuwa mtu hawezi kuacha jambo wakati nafsi yake ina uhuru wa kuchagua mambo mbalimbali iweje hili asiweze kuliwacha wakati kabla ya kuanza hakuwa akilifanya.
Kama ingekuwa Mungu anawalazimisha waja wake watende dhambi basi huo moto wa kazi gani si atakuwa anawaonea tu ? H
الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ
[ ANNAJM - 32 ]
Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu.
Ukiangalia aya imeeleza kuwa kuna wale ambao wanajiepusha na makosa ama madhambi makubwa makubwa.
Isipokuwa makosa khafifu yale madpgo madogo ambayo kila mwanaadamu huyatenda kwa namna yake
Hapo ni katika ishara kuwa Mola amewapa watu fursa na uhuru wa kujizuia na madhambi hasa makubwa makubwa kama kuuua kwa makusudi,kumbaka mama mzazi na mengineyo makubwa.
Hapo ni ishara kuwa mja anaweza kutoka na akachagua kujiepusha na mambo kadha wa kadha bila kutenzwa nguvu na Allah