Kama wote wameumbwa kwa roho ambazo zina uhuru wa kuchagua sawasawa
Nisome vizuri mkuu.
Nimesema sote tuna roho zenye uhuru wa kuchagua,sikusema sawasawa.ukisema sawasawa maana yake Mungu kaweka limitations kwa watu wote.
Neno usawa sawa usiliweke kwa sababu sikulisema.
je nini kinapelekea mtu A nafsi itende lililojema na mtu B achague lililoovu?
Ni kwa sababu ya uhuru waliopewa wa nafsi zao kuchagua mambo ndio inapelekea mtu fulani kutenda mema na mwingine kutenda uovu.
Kama ambavyo sote tuna mikono lakini kuna watu wanatumia mikono kufanya uovu wa kuiba,wengine wanatumia mikono kufanya uovu wa kuua,wengine hutumia mikono kufanya wema wa kufagia,wengine hutumia mikono kufanya wema wa kusaidia maskini n.k
Huyu anaesaidia maskini anao uwezo wa kuiba ila hajataka kwa sababu nafsi yake hajaiamrisha ifanye hivyo,na huyu anaeiba anaweza kufanya wema ila hajataka nafsi yake iwe hivyo.
Kwa hiyo kama ambavyo tumepewa mikono inayofanana tunafanya mambo tofauti kwa utashii wanafsi zetu.
Basii na roho tumepewa zinazofanana lakini tunafanya mambo tofauti kwa utashi wetu na uhuru tuliopewa na Mungu.
Na kufanana hapo ni kule kuwa yote ni mikono,ama kuwa zote ni roho ama kuwa vyote ni vichwa lakini bila shaka tuna vichwa tofauti,mikono tofauti japokuwa sote tunavyo.
Kutokana na binadamu kuumbwa na mapungufu, huoni kwamba hawa watu wanatofautiana kiasilimia za mapungufu hivyo kupelekea kuzidiana kwa utashi?
Ndio mapungufu kama vile kuna watu Mungu huwaumba machizi,utashi wa chizi na mzima ni tofauti.
Inategemea wewe utatafsiri vipi neno upungufu.
Unasema mtu kapewa uhuru wa kuchagua,
Uhuru ni ile hali ya nafsi kuweza kutenda baya ama zuri,yaani kuweza kutenda yote huu uwezo wa kutenda yote ndio uhuru wenyewe kwanza.
ingelikuwa mtu kapewa uhuru asingesurutishwa kuwa asipotenda mambo fulani anaadhibiwa
Sasa ndio maana nikakuambia hapa tupo kwenye game duniani,umepewa uhuru (uwezo)wa kufanya mema na mazuri
Alafu ili Nafsi yako ijaribiwe unaambiwa usifanye hili ambalo uwezo wa kulifanya unao,usizini na uwezo unao.
Kwa hiyo tumekatazwa kuyafanya hayo kwa sababu uwezo tunao wa kuyafanya.
Ndio maana hatukukatazwa kuumba ulimwengu kwa sababu uwezo hatuna,tunayokatazwa ni yale ambayo tunayaweza ili sasa ile mantiki ya kuwa tupo katika mtihani ipatikane.
Na kule kuadhibiwa kwa kutotenda mambo fulani maana yake ni ishara kuwa ulikuwa unaweza kuyatenda lakini ukayaacha kwa jeuri.
Hivyo maswali unayoiza yanaenda sambamba na thana hii ya kuwa hapa duniani tupo katika kujaribiwa nafsi zetu wenyewe.
angeachwa aamue aliyokipenda pasipo kupewa mipaka. Ukimpa mtu mipaka hapo hakuna uhuru.
Unachanganya hapo kuhusu uhuru.uhuru niliougusia mwanzo ni ule wa nafsi kuamua lipi afanye na lipi asifanye kwa kujiuliza na kwa uwezo wake mwenyewe.
Kitendo chakuwekwa adhabu kwa watakaofanya mabaya maana yake hayo mabaya walikuwa wanaweza kuyatenda ndio maana wataadhibiwa.
Sasa hapa ni kwamba uwezo wa nafsi kuamua kufanya mambo wayatakayo ndiyo uhuru ambao niliuzungumzia.
Uhuru huo wa kuchagua tuliopewa katika nafsi zetu sasa,tukaletewa Muongozo kuwa sasa kutokana na uhuru wa nafsi mliopewa mnatakiwa mfuate taratibu hizi na zile na zile atakayekeuka ataadhibiwa adhabu fulani.
Sasa hapa maana yake ni kuwa unatumia uhuru wako kufuata maamrisho,na unatumia uhuru wako wa nafsi kuacha yale makatazo ya dini.
Na pia ukizingatia vizuri utaona kuwa kuwepo kwa sheria maana yake ni kuwa wapo ambao watazifuata maana yake hizo sheria zimeletwa kwa sababu tunauwezo wa kuzifuata ama kuzikeuka.
Huu uwezo wa kuzifuata ama kuzikeuka ndio uhuru wa nafsi,na Mungu kajua kuwa ametupa uhuru wa nafsi kwa kuchagua jema na baya ndio maana akaweka adhabu kwa watakaowacha kufuata.
Kwa hiyo haya mambo mawili usiyachanganye.