Je, hii kauli ya Lissu ni kukosa hekima, kutokujali au ndio changa la macho kwa wananchi baada ya tuhuma za kulamba asali?

Je, hii kauli ya Lissu ni kukosa hekima, kutokujali au ndio changa la macho kwa wananchi baada ya tuhuma za kulamba asali?

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Posts
4,437
Reaction score
13,836
Akiwa 'nyumbani kwake' huko Ubelgiji, makamu wenyekiti wa mitandaoni wa CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu ameandika hivi mtandaoni.

Je huku sio kumkosea adabu partner wa CDM kwenye maridhiano ambaye technically ameshika upande wa mpini?

Si amesema hadharani kuwa mchakato unakuja na utakuwa shirikishi? tena ameyasema hayo baada ya maridhiano na chama cha Lissu!

Kwamba Lissu hana uvumilivu au hakubaliani na msimamo wa chama chake ama ni kukosa tu hekima na busara?

Alafu hili la kudai hela zake kila mara hili ni nini hasa? Kwamba ndio sera yake endelevu? Si alisema amelipwa huyu? 🤣🤣🤣

Na hiyo viza ya Ubelgiji inachukuwa miezi mingapi kuihuisha?? Au ndio yaleyale ya akina Liberatus Mwang'ombe ya kurudi wakati wa uchaguzi alafu wakiangukia pua haooo wanakimbilia zao 'makwao' kwa mabeberu?

======

Kupamba mji kwa mabango hakuleti umoja wala kuondoa uhasama. Katiba Mpya, Mfumo Huru wa Uchaguzi, Tume ya Ukweli, Haki & Upatanishi ndio jibu. Ondoa ukimya juu ya waliotaka kuniua & walioua, kupoteza & kutesa Watanzania wengine. Lipa haki zangu & za wengine ndio utuwekee mabango!

Screenshot 2023-03-26 at 12-46-16 Tundu Antiphas Lissu on Twitter.png
 
Huyu Lissu kwanza hayupo bongo hajui hata kunaendelea nini.

Hela za ruzuku mmechukua?
Mmepewa na hela zenu mifukoni?
Madeni mmelipiwa?
Ila kwenye mabango hamtaki kuwekwa mna matatizo gani?
Kwenu pesa mbele kama tai...mkipenda kulamba asali mjiandae na kuumwa na nyuki siku moja 🤣🤣
 
1. Katiba Mpya.

2. Tume Huru.

3. Tume ya Ukweli, Haki, na Upatanishi.

Kama mambo hayo hayajatekelezwa MABANGO ya kujisifu ya kazi gani?

Na mabango yanatengenezwa kwa kutumia KODI za wananchi wengi wao wakiwa masikini.
 
Akiwa 'nyumbani kwake' huko Ubelgiji, makamu wenyekiti wa mitandaoni wa CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu ameandika hivi mtandaoni.
View attachment 2564267

Je huku sio kumkosea adabu partner wa CDM kwenye maridhiano ambaye technically ameshika upande wa mpini?

Si amesema hadharani kuwa mchakato unakuja na utakuwa shirikishi? tena ameyasema hayo baada ya maridhiano na chama cha Lissu!

Kwamba Lissu hana uvumilivu au hakubaliani na msimamo wa chama chake ama ni kukosa tu hekima na busara?

Alafu hili la kudai hela zake kila mara hili ni nini hasa? Kwamba ndio sera yake endelevu? Si alisema amelupwa huyu? 🤣🤣🤣

Na hiyo viza ya Ubelgiji inachukuwa miezi mingapi kuihuisha?? Au ndio yaleyale ya akina Liberatus Mwang'ombe ya kurudi wakati wa uchaguzi alafu wakiangukia pua haooo wanakimbilia zao 'makwao' kwa mabeberu?
Huyu ni kirusi hatari zaidi kuliko kile cha covid 19 ndani ya hicho chama. Si mwana siasa hata kidogo bali ni mwanaharakati kama Fatuma Karume, Maria Sarungi na Kunambi. Akipewa nchi, Tanzania itakuwa jamii ya LGBTQQIP2+.
 
Back
Top Bottom