Je, hii kauli ya Lissu ni kukosa hekima, kutokujali au ndio changa la macho kwa wananchi baada ya tuhuma za kulamba asali?

Hoja ya Lissu ina nguvu , naiunga mkono , wanafiki wanaomdanganya Hangaya ndio wanatumia picha hizi kupotosha jamii , hatutakubali
Yaliyoandikwa ni ya kweli. Waliokuwa wamekimbia nchi si wamerudi? na akina Lissu wameamua kuondoka wenyewe kwa hiyari zao.

BAWACHA hadi mmefikia hatua ya kumwalika mama (mwenyekiti wa CCM) kwenye shughuli yenu, sasa kama sio kuunganisha nchi huko ni nini?

Katiba mpya inakuja, ameahidi na anatekeleza ahadi zake, na ndio maana hata nyie hamtoweka mgombea urais 2025.
 
Kumbe alikuja kuchukua tu pesa yake. Alichukua yote bali ilikatwa withholding tax ya 24% kama ilivyo kawaida na kisheria. Sasa anadai alipwe hata hiyo 24%.
Labda analipa kodi kwao huko Ubelgiji, hapa kwetu anataka kuvuna tu.
 
Arudi singida..mbaya wake JPM si hayupo, eti?
Ataanzaje kumweliza wife na watoto, tuhame ulaya twende zetu Singida 🤣🤣🤣🤣

Huyu jamaa tusipokuwa makini atatupiga sana pesa alafu anakwenda zake huko Ubelgiji, kwasasa wamkazie tu. Akitaka hela basi arudi achape kazi😂😂
 
..walaghai ni Samia na Ccm.

..wao ndio wanapoteza muda bila sababu za msingi.
Hiyo yajulikana uzuri tu.

Lakini ni sawa kwa CCM kufanya hivyo maana ni kwamba mpango wa CCM ni kuelekea mchakato wa 2025 bila bughudha.

Ila suali ni kwamba kwanini Tundu Lissu amerejea Ubelgiji na huenda pengine asirudi hivi karibuni?
 
Hiyo yajulikana uzuri tu.

Lakini ni sawa kwa CCM kufanya hivyo maana ni kwamba mpango wa CCM ni kuelekea mchakato wa 2025 bila bughudha.

Ila suali ni kwamba kwanini Tundu Lissu amerejea Ubelgiji na huenda pengine asirudi hivi karibuni?

Katiba Mpya.

Tume Huru ya Uchaguzi.

Tume ya Ukweli, Haki, na Upatanishi.

Utekelezaji wa mambo hayo matatu ni muhimu zaidi kuliko habari za Lissu kuwepo au kutokuwepo nchini.

Tunatakiwa tuwe makini / focused kwenye hoja hizo 3.
 
..walaghai ni Samia na Ccm.

..wao ndio wanapoteza muda bila sababu za msingi.
Mkuu ukisoma kwa kina post nyingi katika thread hii utagundua watu wengi uwezo wao kuelewa katikati ya mistari ni wa level ya chini sana.
Lissu yuko sahihi kabisa, kuna haki gani kuweka mabango yakionyesha maridhiano wakati matidhiano hayo hayakamilika hata one third ya kutimia?
Kuna watu wamedhulumiwa haki zao na hawajafidiwa, walio shambulia watu na hata kuua wapo katika ofisi za umma na hawajashughulikiwa, mchakato wa katiba mpya hadi leo bado ni hadithi tamu na kadhalika.
Bila hayo kutekelezwa hizo picha za kupeana mikono inabaki ni ulaghai wa mapema pengine kwa malengo maalum
 
Shikamoo Tundu Antipas Lissu.

Huyo ndiye mwanasiasa anayesimama kwenye ukweli bila kupepesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…