Je, hii kauli ya Lissu ni kukosa hekima, kutokujali au ndio changa la macho kwa wananchi baada ya tuhuma za kulamba asali?


..I agree with you 100%.

..Watanzania inabidi tuwe na uchungu na nchi yetu.

..Ukisoma mijadala yetu unaona tunatilia mkazo mambo yasiyo na manufaa, na kuacha yale yenye manufaa.
 
Sasa wadhani CCM wamekurupuka kuweka hayo mabango?

Wanaweka mabango watajitetea kwamba kwa kuwa mchakato upo mezani, kuweka mabango ni njia ya kuukumbusha umma kwamba kuna maridhiano yafanyiwa kazi yaani wako kwenye "process".

Au kwa kiingereza yasemwa "Chadema and CCM Reconcilation Talks continue, still long way to go".
 
Mmelamba asali wenyewe mkamtosa Lissu. Lissu alijua mbowe ana masihara na njuruku?
 

..hilo bango ni mali ya nani?

..amepata ridhaa ya Lissu kumuweka kwenye bango?

..nadhani itafutwe namna kumshtaki.
 
Hawa jamaa ni nyumbu ila Kuna baadhi ya raia apa wanaweka Imani zao kwao kama chama Chao kimemukubali mwenyekiti wa CCM wengine mnangoja nn chama hamna pale wanesalim amri kwa kisingizio Cha Maridhiano Hangaya ni shujaa kawamaliza kwa macho tu nyumbu wote imooo
 
Tukimpa uraisi hazina yetu ataikausha kwa kuipeleka kwenye akaunti yake huko Uswizi.
 
Mkuu siku zote za uhai wao , ccm huwa wanachelewa kulielewa jambo... Usisoma comment zao unaona kbs wengi wao akili zao ni sawa na mtoto njiti ... kichwani hawako vzr kbs
 
Ni sababu zipi zimemfanya Tundu Lissu akatishe harakati zake za siasa Tanzania na arejee uhamishoni Ubelgiji?
Si alienda kukaguliwa maendeleo ya afya? Mbona aliongea kupitia mahojiano ya star tv?
 
Si alienda kukaguliwa maendeleo ya afya? Mbona aliongea kupitia mahojiano ya star tv?
Hivyo vi plates, screws na nails vilivyowekwa kwenye long bones za mguu wake wa kulia, mbona mabingwa wetu wabobezi waliopo pale MOI wana utalaamu huo huo sawa na hao wabeligiji na mama kawapatia vifaa tiba vyote na vya kisasa sawa na hivyo walivyo navyo wabeligiji. Huyu tukimpa uraisi akiumwa hata mafua tu yeye au mke au watoto wake watakuwa wanaenda kutibiwa Ubeligiji. Hawaamini watalaamu wetu na hataboresha vitendea kazi vyao ili viwe sawa na hivyo vya kwao ubeligiji.
 
Unaongea utopolo mtupu.
ALiliyapitia Lissu sio ya kubeza na kuchulia poa.
Bora msimpe huo urais wenu usiokuwa na tija katika taifa...zaidi ni ulaji tu.

Huwezi kwenda kufanya check up kwa daktari asiyejua historia kamili ya upasuaji mkubwa na hatari kama hui.

Kwanza akienda myhimbili ccm mtammalizia mlivyo na chuki
 
..hilo bango ni mali ya nani?

..amepata ridhaa ya Lissu kumuweka kwenye bango?

..nadhani itafutwe namna kumshtaki.
Kuhusu bango ni suali gumu kidogo kwa kweli maana yawezekana ni walo nje ya meza ya maridhiano au watazamaji au washika mabango.

Yawezekana pia ikawa ni vijana wa CCM au wa Chadema kwa utashi au maelekezo wameamua kuweka hilo bango.

Kwani kuweka bango hilo katika barabara muhimu kama hiyo kwahitaji kulipia fedha kiasi fulani au?
 
Safi sana mhafidhina mwenzangu Tundu Lissu [emoji122]

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Umetumia neno sahihi sana wahafidhina.

Hawa ni lazima wawepo katika mchakato wowote ule wa kisiasa na wala hakuna haja ya kuwasakama.

Nakumbuka hata kwenye masuala ya mpira klabu yangu ya Yanga iliwahi kuwa na mzee ambae alikuwa mhafidhina khasa Adam Bairu au mzee mwingine Ibrahim Akilimali walikuwa huwaambii masuala ambayo hayaeleweki kuhusu maridhiano au mambo yasoeleweka. .

Maridhiano yataka stratejia inoelekea kuleta matunda kwa kila pande na si upande mmoja kuonekan wazi wautuia upande mwingine kujinufaisha kisiasa.
 
Upasuaji wake huo wa kuweka plates and nails in in his lower limb bones ni upasuaji wa kawaida tu ambao MOI wanafanya kila siku. Hata kwenye hospitali zetu za kanda na mikoa unafanyika kwa ufanisi mkubwa. History ya ugonjwa na upasuaji wake uko well documented. Siyo lazima check up ifanywe na daktari huyo huyo mmoja. Ina maana akiwa hayupo kwa sababu ye yote hususani kwa ugonjwa, kustaafu, kufariki dunia etc daktari mwingine atashindwa kufanya proper check up? Hizo plates, nails na screws zitakaa milele kwenye hiyo mifupa yake na haihitaji any check up. They are permanent parts of his body. No complications is expected from them
 

..Magufuli alijitia ujuaji kwenda JK na Mzena mnajua kilichomtokea.
 
Na kwa kuongezea tu ni kwamba kama aenda hospitali ya Tanzania basi huwaambia madaktari wa Ubelgiji ambao nao hutuma tu hizo "documents" au "medical history" kwa njia ya email tu kwenda systems za hospitali yoyote atayochagua nchini Tanzania.

Ila kuna tatizo la "logistics" kwa vifaa za matibabu kwani kwa kule Ulaya masuala hayo hayana shida kulinganisha na huku TZ ambako "authentication" ya vifaa huwa ni muhimu sana kuepusha kununuliwa vifaa vilivyo chini ya viwango vya kimataifa.

Pia kuna expenses ambapo kwa Ulaya ni "straight forward" mchanganuo wajulikana tofauti na hapa TZ ambapo watu wataanza kupiga hesabu za cha juu hivyo kukwaza shughuli nzima ya kumshughulikia mgonjwa kiufanisi.

Lakini nadhani mheshimiwa Tundu Lissu yupo "stable" sana financially hivyo sidhani kama kutakuwa na shida sana kwenye kumudu gharama za "check-ups".
 
Si alisema amelipwa huyu? 🤣🤣🤣
Kasema kalipwa,viza kurenew akikubaliwa miezi 3-6.
Akikataliwa itabidi aombe tena.
Huko alipo kuna wakimbizi kibao toka nchi za Africa wa karima yake so ni ya kawaida sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…