Je, inawezekana Jakaya Kikwete ndiye Nyerere wa leo?

Hapana, haiwezwkani. Jakaya yupo juu sana ya Nyerere kiuongozi.

Magu ndiye unaweza kumfananisha na Nyerere, wote hao walikuwa hawaambiliki, wakurupukaji na walitumia nguvu nyingi kuliko akili katika uongozi.
πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘†πŸ€£πŸ€£
 
Nyerere alikuwa juu sana huwezi kumlinganisha na hawa wote waliomfuatia. Diplomatic figure of highest quality, na nina uhakika hata Kikwete mwenyewe alijifunza mengi ya kimaisha kutoka kwake kwa muda wote aliokuwa ikulu.
Tusitumie Nguvu sana kulazimisha mambo.Kwa nini watu wote waliokuwa na Nyerere walienda kinyume na yeye kama kweli walijifunza kwake?
 
Sifa pekee ya Mwalimu ni kujenga utaifa,hakuna zaidi ya hicho.
 
Nyerere alikuwa juu sana huwezi kumlinganisha na hawa wote waliomfuatia. Diplomatic figure of highest quality, na nina uhakika hata Kikwete mwenyewe alijifunza mengi ya kimaisha kutoka kwake kwa muda wote aliokuwa ikulu.
Hakuwa kama unavyofikiria, angekuwa kama unavyifikiria asingeng'atuka na nchi ni masikini wa mwisho duniani.
 
Never, jamaa kauza nchi kukomboa jangili asiye na maslahi na nchi yetu (Ridhiwani) ili asinyongwe na Wachina kwa kuuza madawa ya kulevya. Nyerere angemwachia mwanaye anyongwe tu ili iwe fundisho kwa wananchi wake wajinga
 
Hakuwa kama unavyofikiria, angekuwa kama unavyifikiria asingeng'atuka na nchi ni masikini wa mwisho duniani.
Kung'atuka ni maono ya hali ya juu kulinganisha na marais wa kizazi chake wa nchi za Afrika wakati ule.

Kaunda aling'ang'ania madarakani, nini kilikuja kumkuta?. Banda rais wa maisha ya Malawi, nini kilimkuta baada ya kushindwa kuongoza nchi?.

Umaskini upo nchi nyingi duniani, na usione mabadiliko ya wakati wa JK kwa kulinganisha na ule wa Nyerere ukaja kumsifu Mkwere, ni muda unafika na mabadiliko ya uchumi yanatokea.

Hata JPM hatakiwi kujisifu sana kwa kujenga miundo mbinu aliyokuja kujenga, wasomi walioandaliwa miaka ya Nyerere walikwisha kufika wakati wa wao kufanya kazi wakati wa JPM hivyo wakamrahisishia kazi ya urais.
 
Tusitumie Nguvu sana kulazimisha mambo.Kwa nini watu wote waliokuwa na Nyerere walienda kinyume na yeye kama kweli walijifunza kwake?
Kwenda kinyume ni presha za wahisani zinazokuwa ni sababu tusizozifahamu za nyuma ya pazia.

Kwenda kinyume pengine ni ile roho ya wasaidizi wa marais wanaotaka kutajirika wakijua kuwa kipindi cha kupata neema ni ile miaka kumi ya kuwa pamoja na rais.

Kuongoza nchi sio kazi ya rais peke yake, anakuwa na timu nzima ya wasaidizi nyuma yake.
 
Hapana, haiwezwkani. Jakaya yupo juu sana ya Nyerere kiuongozi.

Magu ndiye unaweza kumfananisha na Nyerere, wote hao walikuwa hawaambiliki, wakurupukaji na walitumia nguvu nyingi kuliko akili katika uongozi.
Hili bibi lina udini na linaonekana lichawi
 
Ni bora kwa sababu ni muislamu mwenzio
 
Nilisikia kuna meli ya serikali iliuzwa kwenye utawala wake.Hii unaisemaje?.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Ukiwapanga marais wanne bora kidemokrasia nchini
Namba 1 ni JKN
2. Mzee Ruksah
3. Ni JMK
4. Samia (huyu mpaka amalize kipindi chake akiendelea hiv, akawapuuza wahafidhina) kuna uwezekano akawa namba 2)
5. Mkapa
6. Hakuna
Udini unakusumbua
 
Nyerere hakuwa fisadi. Acha kabisa kumlinganisha baba wa taifa na hivi vitu vingine vya .........!
Meli ya serikali iliyouzwa kipindi chake siyo ufisadi?.
Halafu kumpa sifa mtu aliyeshindwa kukuza uchumi wa watu kati ya milioni 9 na 15,ni upuuzi ukimlinganisha na aliyekuza uchumi wa watu kati ya milioni 40 na 50.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…