Je, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina mamlaka juu ya Spika?

Tatizo siyo dungai Wala CCM Wala CDM tatizo ni alieleta Sera ya wabunge wa viti maalamu, sioni Kazi Yao zaidi ya kuleta migogoro ya kisiasa ndani na nje ya vyama vyao, kupoteza pesa za bure za walipa Kodi na kuendekeza rushwa za ngono nchini.

Nalog off.
 
Mkuu,
Katika awamu hii inaonekana haijalishi sheria au katiba inataka nini. Awamu hii ni mkulu anataka nini, whether katiba imesema au haikusema kwao hili si muhimu!
Watanzania tunaponzwa na uoga na upole wetu, si unaona yote haya yanafanywa watu tupoo tunaangalia tu kwa macho. Tunaoweza kuandika ndio huandika na kuishia kulalamika tu basi!

Si angalau sisi wengine ambao hatuna sauti za kusikika huandika...angalau tutaseme 'we did something about it'! Ila kuna watu wenye sauti zao kwa mfano Viongozi wa dini, na baadhi ya wastaafu woote kimyaaaaaaa!!! kama kwamba hakuna kilichotokea! Mzee Msekwa kidogo kwa kujua kitakachoetokea kaona aseme kabla ili asije akalazimika kusema baadae haya tuseme sihaba. Kule kwetu kuna msemo usemao "Nalitote tugawane mbawa". Tukiendelea hivi tutegemee siku moja tutaamka kila mtu na ubawawe!.
 
Wacha kujichanganya.

Katiba yetu iko very clear, ili mtu awe mbunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha siasa, ukishavuliwa uanachama na chama chako automatically unapoteza sifa hii, na hata Spika hana mamlaka yoyote ya kuendelea kumtambua mtu huyo kama mbunge, kwani kwa kufanya hivyo anakuwa ameingilia maamuzi ya chama ambacho kipo halali kisheria (hili nalo ni kosa).

Kuendelea kumtambua mtu huyo kama mbunge unakuwa umevunja sheria nyingine, nchi yetu hairuhusu watu binafsi kuwa wabunge, ukishavuliwa uanachama na chama cha siasa unakuwa huru hivyo hustahili tena kuwa muwakilishi bungeni, au uniambie akishavuliwa uanachama anakuwa mbunge kwa ruhusa ya Spika? hayo mamlaka Spika ameyapata kwa sheria ipi?

Kwa hili hakuna mahakama iliyo huru itakayopata shida kutafsiri hiyo sheria, labda mahakama hizi za "CCM" ndio zishindwe, hakuna mgogoro wowote hapo wa kikatiba.

Chadema wangetakiwa waende mahakamani kama kuna mgogoro, lakini hakuna, wamemaliza kazi yao kama chama kwa kufuata taratibu.

Wanachotakiwa kufanya Chadema kwasasa ni kuandika barua kuijulisha ofisi ya Spika kwamba hao wasaliti sio wanachama wao tena, Spika ndio aangalie sheria inasemaje aamue, kama alivyowahi kufanya kwa wale wabunge wa CUF, this is very short, simple and clear... no messing around.
 
Ndio maana Ndugai anasema wateule 19 walioapa, bado wanawatambua kuwa ni Wabunge wa Bunge la JMT, unless waamue kujiudhuru wenyewe. "Yanayoendelea huko Chadema ni yao"
Chadema haina shida na ubunge wa hao covid 19...ila hawatambuliki kama wabunge wa CDM...$900m za dezo hakuna kwa miaka mitano
 
Lazima kwanza Tume ipewe na chama taarifa rasmi ya kufuta wanachama. Kisha Tume inampa taarifa Spika. Ubunge haufutwi kupitia vyombo vya habari!
 
Uko sahihi kabisa!
 
Lazima kwanza Tume ipewe na chama taarifa rasmi ya kufuta wanachama. Kisha Tume inampa taarifa Spika. Ubunge haufutwi kupitia vyombo vya habari!
Sijui taarifa tume, sijui taarifa kwa spika ili iweje?
Mahaba ya job na halima kwanini kuyaingilia?
Watu wamehongana ubunge halafu eti uwaingilie,, ili iweje?
Waachwe wale bata.
 
Mambo mengine best tuwaachie constitutional lawyers

Hiyo aspect ya chama mnayoitumia imetajwa sehemu moja tu tena subsection yenyewe it’s literal meaning is weak argument to present at court.

Katiba inatambua kiongozi wa serikali anaweza teuliwa kuwa mmbunge anytime na ikitokea anatakiwa aache nafasi yake serikalini. On the other hand Civil Servants wanatakiwa wasiwe na party affiliations (kwa maana hiyo kuna wabunge wanaweza wasiwe na vyama vya siasa kwa mujibu wa katiba).

Kesi ya CUF mahakama iliwatambua wabunge waliofukuzwa uanachama na hii ya Hakina Mdee ikienda mahakamani hakuna much sufficient difference to distinguish the two cases; in maana precedent itakayo tumika ni case ya CUF.

83 ya katiba inasema uamuzi wa suala la ubunge (meaning kama ubunge wa mtu unakuwa contested, chombo cha kuamua ni mahakama kuu).

Whereas 71 (e) inasema iwapo mmbunge atakapo acha kuwa mwanachama i.e kwa ridhaa yake; aisemi atakapofukuzwa.

Kwa ivyo katiba pekee is vague unless kama kuna sheria inayotoa clarification zaidi.

Kesi kama hiyo mahakamani tayari kuna literal conflicts kwenye katiba kwenye swala zima la uanachama na mmbunge. Na mgogoro wowote wa sheria, you and I know ikishatoka bungeni chombo chenye kuamua ni mahakama.

Ila ukishakuwa mfuasi wa CDM kikawaida wao ndio; jurists, prosecutioners and judges. Especially viongozi wao wakiamua na Lissu akisema apparently ndio Gwiji wa sheria dunia nzima kwa mujimu wa wafuasi wa CDM.

Binafsi nataka kusikia mjadala wa lawyers kuhusu ili swala mahakamani kuliko majadiliano yetu ya JF bush lawyers.
 
We ni mpuuzi mmoja ambae unajifanya unajua wakati ni fala tu. Katiba ina sections. Subsection gani unayo isema ipo kwenye katiba?

Katiba ni tofauti na hizi sheria zingine. Ndio maana ina Articles, Ariticle 71(1)(e) ipo wazi kabisa in plain meaning ukomo wa mwanachama either kwa kujiuzulu au kufukuzwa ndio mwisho wa uanachama.
Unaleta utetezi gani wa kipuuzi. Kesi ya Cuf na hii zinafanana? Wale walikuwa wabunge wa viti maalumu ambao hawakupata baraka za Cc ya Cuf?
 
Ndugai ana ufupi wa kimo na akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…