Unakuza mambo bila sababu yoyote ya msingi, umeshasema case ya CUF itatumika kama precedent, na kule mwanzo ulisema unataka kesi iliyotumika kama precedent, nimekupa, lakini bado unakuja na maneno mengi ya kujichanganya bila sababu.
Basi niambie ni sheria gani inayompa Spika mamlaka ya kupinga maamuzi ya KK ya Chadema?
Tena uniambie, huoni Spika kugoma kwake kuwaondoa hao wabunge kutasababisha tatizo jingine, kwani hairuhusiwi mbunge asiwe huru (bila kuwa kumuwakilishi wa chama)?
Unataka mahakama ijiingize kwenye huo mgogoro wa kitoto?
Article 83 inasema mahakama ndio chombo cha kuamua, na imeshawahi kuamua kwenye issue ya wabunge wa CUF, but mpaka uende mahakamani lazima kuwe na mgogoro kati ya wanachama na chama chao, hapo Spika hausiki, Spika kazi yake ni formality tu akishapelekewa taarifa na chama husika mtu flani sio tena mwanachama wao kwa maandishi hatakiwi kuhoji kwa nini, anatakiwa kuwaondoa tu, kama anayo hayo mamlaka ya kuhoji ameyapata wapi, nipe sheria?
Sheria ukiisoma siku zote lazima ujue na kuitafsiri, sio unaisoma tu halafu unaishia hapo.
Nina maswali mengi tu ya msingi ya kukuuliza ila naona napoteza muda bure, vyema ujiamini iache akili yake ifikirie, kusema unawasubiri magwiji wa Constitutional Law mahakamani waka argue kuhusu issue iliyo wazi kama hii ni kujidumaza akili.