Mungo Park
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 2,115
- 1,834
Kiulinzi na kiusalama siyo 'afya' sana kwa Walinzi wa Rais kutembea na silaha zinazoashiria utayari wa mapambano ('non-concealed') kwa wakati wote. Hii inamaanisha kuwa urari wa usalama('Threat Level') uko juu kupelekea kuongeza ulinzi. Hii pia inaweza kuwa mbinu ya kisaikolojia ya kuwanyongonyeza adui.
Kwa huko Puerto Rico askari uliowaona wanatoka Kikosi cha Ulinzi wa Rais (Presidential Protection Unit -Emergency Response). Hawa PPU-ERT ni wajuzi wa mashambulio ya haraka katika halaiki. Mwanzoni hili lilikuwa jukumu la FFU-ERT lakini kwa sasa wanaanza kupokwa polepole.
Dhumuni la Walinzi wa Rais ni Ulinzi ingawa wanaweza kushambulia ikibidi na Rais huko Puerto Rico ana walinzi wengi hadi kufikia Platuni nzima watu 15+ kwenye 'detail' yake kutokana na urari wa usalama.