Habari Wakuu.
Hivi inakuje kuna baadhi ya familia unakuta watoto wote wana akili, wamesoma mpaka level za juu kabisa. Au unakuta familia nyingine karibu wote wana uchumi mzuri, wana biashara kubwa na mafanikio kede kede.
Kwa upande mwingine unakuta familia nyingine watu karibuni wote hawaja fanikiwa kielimu wala kiuchumi. Wana umasikini uliotopea.
Je, hizo familia zinazo kuwa na watu wengi wamefanikiwa ni kuwa wamebarikiwa au ni genetics au nini ndugu wajumbe.
Karibuni kwa michango yenu.
Habari Wakuu.
Hivi inakuje kuna baadhi ya familia unakuta watoto wote wana akili, wamesoma mpaka level za juu kabisa. Au unakuta familia nyingine karibu wote wana uchumi mzuri, wana biashara kubwa na mafanikio kede kede.
Kwa upande mwingine unakuta familia nyingine watu karibuni wote hawaja fanikiwa kielimu wala kiuchumi. Wana umasikini uliotopea.
Je, hizo familia zinazo kuwa na watu wengi wamefanikiwa ni kuwa wamebarikiwa au ni genetics au nini ndugu wajumbe.
Karibuni kwa michango yenu.
Nimefurahishwa sana na kukutana na huu Mtazamo. Na ni kwasababu katika miaka fulani niliishi nikiamini hivyo.
Leo naandika hili nikiwa nje ya kile nilichoamini, binafsi nimetokea katika familia yenye wingi wa watu walioishia njiani katika masomo na ni hakika leo hii kupitia mimi wamefuta dhana waliyokuwa nayo.
Ndipo hapo nikijitathimini najikutaa naanza kujicheka kwanini nilidhani kuwa sitafika mbali kama ndugu zangu.
NAJIBU HOJA YAKO KWA KUSEMA.
Kwanza ni kiri kuwa ni kweli zipo familia zina mnyororo wa kutofanikiwa kielimu na zenye mnyororo wa mafanikio kielimu. Hata inafikia wakati watu wanaamini watu wa makabila fulani wapo vizuri kielimu na makabila fulani huishia kuvaa misulupwete.
Basi leo nakupa majibu ambayo walau yatakuridhisha hata ikiwa sio kwa asilimia mia.
Naweka wazi kuwa SIO KWELI YA KWAMBA BAADHI YA FAMILIA ZIMEBARIKIWA ZAIDI WALA SIO KWAMBA BAADHI YA FAMILIA ZIMELAANIWA (Niwie radhi kwa kutumia neno hilo)
SABABU YA KUWEPO KWA HALI HII HUSABABISHWA NA NADHARIA TOFAUTITOFAUTI (Miongoni mwao umekwisha kuzitaja)
Nazo ni kama zifuatazo:
1. Kurithi / Genetics (Huaminika zaidi kisayansi).
2. Malezi na Mazingira ya makuzi.
3. Haio ya kiuchumi ya familia.
4. Utamaduni na mitazamo.
5. Rasilimali na misaada
6. Motisha binafsi (kujitambua).
Ningeweza kueleza kila nadharia kwa upana lakini walau hiyo inatosha kuwafanya mtafakari.
Kwa kuhitimisha ni kwamba mafanikio ya familia ni matokeo ya mwingiliano wa sababu nyingi zaidi ya zilizotajwa hapo na sio moja pekee. Inawezekana umerithi genetics za kizombie walakini malezi yakiwa bora, ukapata support, ukawa na motisha binafsi, ukaweza KUTOBOA.
Na ifahamike kuwa kutokana na sababu hizo baadhi ya familia hujikuta katika mnyororo au mzunguko wa umaskini. Hivyo sio genetics peke yake humfanya mtu kutoendelea.
Kila familia ni ya kipekee, na hivyo ni muhimu kuzingatia mambo haya yote katika kuelewa tofauti za mafanikio kati ya familia mbalimbali.
Watu hawapasqi kuamini na kujifunga kwa historia za familia zao bali kuamini kila mtu anaweza kufanya kitu cha tofauti.