Wanabodi,
Hivyo hakuna ubishi kuhusu uwezo wa wanawake kwenye baadhi ya maeneo, wanawake wana uwezo mkubwa kuliko wanaume kwenye mambo mengi tuu, hata katika uongozi.
Japo kazi ni kazi, na wanaume ndio wanajihesabu wao ndio watenda kazi na wachapa kazi hodari kuliko wanawake, yaani wanaume ni watu wa kuchuma na wanawake ni watu wa kupokea, siku hizi kuna wanawake ndio wachumaji na vi benten vinalelewa!.
Huu mfumo dume umepelelea baadhi ya nafasi kupewa majina ya kiume mfano Boss ni jina la kiume, boss akiwa ni Mwanamke anaitwa The Boss Lady, lakini mabosi wa kike wanapenda kuitwa Boss, na wafanyakazi wengi wana prefers Boss awe mwanaume na sio Mwanamke., maana boss akiwa ni Mwanamke, kuna watu wanakoma!.
Pia nafasi kama ya Chairman/Mwenyekiti, ni jina la kiume, akiwa mwanamke alipaswa kuitwa Chairwoman ila ikaonekana hainogi, hivyo Mwenyekiti akiwa mwanamke anaitwa Chairperson.
Hata cheo cha President na Amiri Jeshi Mkuu kilidhamiriwa kuwa ni cheo cha mwanaume, l mwanamke anaitwa Amirati, ila hata Amiri Jeshi Mkuu anapokuwa Mwanamke, hapendi kuitwa Amirati ana prefers kuendelea kuitwa hivyo hivyo Amiri ambalo ni jina la kiume au chairman badala ya Chairwoman or chairperson.
Tukubali tukatae bado tuna baadhi ya watu miongoni mwetu, waliofilisika kiakili na kisiasa, ambao bado wana tatizo la kutawaliwa na mfumo dume vichwani mwao na kuamini urais wa nchi ni kazi ya kiume!, hivyo ni kweli lile tukio la March 17, lilitokea kabla ya Machi 17!, hivyo lilipotokea wakafanya siri ili kumtafuta mwanaume wa kushikilia kwa kuamimi Mwanamke hawezi!
Bandiko hili ni kuhusu fupa fulani, ukimuondoa Baba wa Taifa aliyetuachia katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, marais wanaume wanne, waliofuatia, hilo fupa liliwashinda, maraisi Mwinyi, Mkapa, JK na JPM, walilishindwa fupa hili. Sasa kama urais ni kazi ya kiume, na tumekuwa na marais wanaume wanne na wote wameshindwa, jee rais Mwanamke mmoja ataweza?. Ili kulijua fupa hili tembelea hapa
Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Jee Mama Samia Ataliweza Fupa Hili?.
Paskali!.