Habarini wakuu!
Upinzani Tanzania kwaheri ndugu zangu. CHADEMA hawana chao tena. Kwanza ukiangalia huoni ambacho wanakifanya majimboni kwao. Wana strategies mfu kabisa. Waoga na ni watu wa kususa susa sana bila kuwa na msimamo dhabiti!
Majimbo tajwa hapo juu yameshaenda na maji. Siyo swala la kuuliza tena.
CHADEMA watawambia nini wananchi mwaka 2020 ? Ni nano ambaye atadanganyika ?
Mamiradi makubwa makubwa yanayofanywa na jembe letu, Rais JPM imeshawamaliza hawa jamaa!
Sera zao zote zimeshatekelezwa. Hawana la kusema.
Bungeni atabaki Zitto pekee labda na Hashimu Rungwe ( maana atagombea Ubunge ). Wengine wote kwakeri yao.
Hatutaki watu wa kupingapinga kila kitu halafu mwisho wa siku wanakuja kulialia wanaomba miradi.
Muda utaongea!
Tukae mkao wa kula.
Wanapata taabu sana, watapata taabu sana mpaka mwisho wa maisha yao!