Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Sawa sitahofu tena🤣
 
Uchawi = ignorance .
Kabisa mtafiti, ndio maana nawashangaa sana napoona wazungu ambao unakuta wana elimu kabisa na wanaishi katika jamii iliyoendelea yenye kuamini zaidi kwenye sayansi ila unakuta wazungu hao nao et wanaamini uchawi sijui hata wana shida gani?
 
Sawa sitahofu tena🤣
Yeah kuwa na amani mkuu, kwa sababu pamoja na jamii yetu kuwa na ujinga na imani za kichawi ila kwa kiasi kikubwa ila hospitali hazijawahi kukosa wagonjwa au shule kukosa wanafunzi.
 
Kitu ambacho huwa sikielewi ni hicho.

Wanasema uchawi humpata kirahisi "anaeuamini na ambaye ana hofu nao"

Kiufupi uchawi hufanya kazi kirahisi kwa anaeuogopa..

Hata hivyo, msimamo wangu ni ule ule. Atakaeniona primitive ni yeye. Ila mimi naamini UCHAWI UPO 100%
 
Sasa inawezekana vp mkuu kuwepo kwa uchawi ilhali kuna watu ndani ya miaka 40+ Tanzania hii hii hajaona huo uchawi?
 
Naomba ufike Tanga wilaya ya Handeni alafu ujue ulete mrejesho.

Fika hapa
Kwa msisi
Kwadikwazu
Sindeni

Haya ni maeneo baadhi tu.

Hakurogi ufe Ila wanakuroga ujifunze.
Watu wanaenda kwa waganga wa mjini. Hawa janja janja wanaochuma dawa wakiwa na akili zao timamu, au ndo wale mikoba iliwachagua ila wakashindwa kuitumikia mwisho wa siku wanabaki hawana kitu zaidi ya kudanganya watu.
 
Na watu wa aina hii ni jamii isiyosoma, elimu ni muhimu sana
Ni sahihi, hata ukikuta wenzetu wazungu wenye kuamini mambo kama haya jinsi wanavyoelezea haya mambo ni tofauti wenye kuamini haya mambo katika jamii ambao hawajasoma.

Ndio maana huku imani potofu nyingi sana ila wenzetu wanafundishana kabisa uchawi wazi wazi ila hakuna imani potofu sababu watu wana elimu.
 
reference ya uchawi navyohusisha na ukoloni nilikupa huo mfano,
mkuu yanayohusishwa na uchawi ni yapi
 
Kitu usichokijua jinsi walivyo watanzania kwenye fikra pia wazungu nao wapo hivyo hivyo , sema tu tofauti ni uwingi.
 
Reactions: Lax
Sasa inawezekana vp mkuu kuwepo kwa uchawi ilhali kuna watu ndani ya miaka 40+ Tanzania hii hii hajaona huo uchawi?
Mbona kuna watu wengi tu wamefariki nchi hii bila kuona maji ya bomba au kitu simple kama umeme. Je, inaondoa ukweli kuwa vitu hivyo vipo

Yani kwa sababu kuna mtu hajui kama internet ya Starlink ipo duniani na hajawahi kuitumia. Ina manisha hicho kitu hakipo?...

Kwa hiyo existence ya kitu ni sahihi ikiwa tu itathibitishwa na kila mtu kuwa kipo.

Je, kabla ya Isaac Newton kugundua gravity, je inamaanisha gravity haikuwepo

Vipi kwa waliogundua electrons, au hata micro organisms ambazo leo hii huwezi kuziona pasipo kutumia microscope. Je kwa sababu wewe hujawahi kumuona protozoa lakini ukiwa diagnosed kutokana na impact ya hicho kitu. Ukapewa dawa na ukapona.. Japo hujui hata process ya hiyo dawa inafanyaje kazi mwilini hadi unapona "Ignorance" Yet kutokana na kupona "unaamini"

Sasa wewe Una tofauti gani na mtu ambaye hajawahi uona uchawi kwa macho ila akienda kwa mganga, anaafushwa anaaguliwa na kupona japo hajui hata huo uchawi unafanye kazi "ignorance" Ila bado "anaamini".

Je ignorance yako kuhusu spiritual world ndio sababu kuu ya kuthibitisha kuwa spiritual world haipo??...

Na ukitaka uthibitisho wa kisayansi. Je, hiyo sayansi ni kitu perfect cha kuthibitisha kila kitu ikiwa yenyewe tu kila siku inakuwa improved. Imagine 2023 ndio tunaanza kuachana na kutumia internet ambayo haitegemi fibers kwenye infrastructures sababu ya kutumia satellite.

What if level ya sayansi ya leo haijawa kubwa kiasi cha kuingiliana na spiritual world. Sasa vipi kama kesho ikifikia hatya hiyo, utaamini kama wale walioamini dunia ipo flat kama meza hadi pale walipothibitishiwa na sayansi kuwa ipo spherical??...

Je ignorance yako binafsi na incapacity ya sayansi iliyopo ndio conclusion ya kuwa kitu flani kipo ama hakipo??...
 
reference ya uchawi navyohusisha na ukoloni nilikupa huo mfano,
mkuu yanayohusishwa na uchawi ni yapi
Nilikueleza vizuri tu kwamba hata kama wazee wetu wangewashinda wakoloni na ushindi huo ukahusishwa na uchawi bado kusingekuwa uthibitisho na hicho ndio kikwazo kikubwa, yani ingebaki tu story sawa na kuibiwa nyeti.

Imani ya uchawi imekuwepo toka karne na karne na hadi hakuna uthibitisho sasa unadhani kungekuwa na madai ya wazee wetu kutumia uchawi kuwashinda wakoloni ndio ingebadili nini kwa kitu ambacho kwa karne zote kimekosa uthibitisho?
 
Reactions: Lax
Uchawi upo kwenye jamii na kama upo huku pia hawakosekani tunataka wathibitishe ili tutofautishe na yale ya nyeti na popobawa
 
Uchawi upo kwenye jamii na kama upo hukubpia hawakosekani tunataka wathibitishe ili tutofautishe na yele ya nyeti na popobawa
Wakuthibitishie kivipi. Wakuandikie thesis na vitabu ama wafanye maonesho ya uchawi Africa?..

Wewe kwanza unaamini katika spiritual world
 
Kitu usichokijua jinsi walivyo watanzania kwenye fikra pia wazungu nao wapo hivyo hivyo , sema tu tofauti ni uwingi.
Mimi nazungumzia waliyoelimika na wasio na elimu, huku afrika watu wanaamini uchawi ni kwa sababu hawajaelimika na ndio maana hata jamii zao unakuta ni mafukara sana ila wenzetu ni tofauti wenyekuamini hayo mambo sio kwa sababu ya kigezo cha kukosa elimu au ufukara.
 
Wakuthibitishie kivipi. Wakuandikie thesis na vitabu ama wafanye maonesho ya uchawi Africa?..

Wewe kwanza unaamini katika spiritual world
Kuamini sio sababu , hata wachaga wanachinja mbuzi nyama kidogo inaachwa kaburini mbwa wanakula wanadai ni mizimu , uchawi upo upo wapi ?
 
Reactions: Lax
nami nikaja kusema mwishoni kwamba


mkuu maelezo yote toka mwanzo wa mjadala , naweka nukta mkuu

mimi niweke nukta tu kwenye hili mkuu, maana kama hatutapata udhibitisho tuendelee kuziita tu story maana kama uchawi wenyewe hauna usawa wa kupiga kazi
 
Kuamini jambo ni machaguo tu , ila ukweli wa jambo ni uhakika
 
Reactions: Lax
Kuamini sio sababu , hata wachaga wanachinja mbuzi nyama kidogo inaachwa kaburini mbwa wanakula wanadai ni mizimu , uchawi upo upo wapi ?
Nimekuuliza unaamini katika spiritual world? ....

Hilo ndilo swali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…