Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Nadhani hili Lina ukweli flani. Na umeeleza vizuri, sayansi haiwezi ku violate laws of physics and biology in a sense watu wamasimulia.

Watu wanaojiita wachawi nadhani pia wapo na Wana practice rituals ambazo watu wanaziita uchawi wenyewe. Ingawa nadhani haiwezekani nipo mbali hichi tunacho kiterm kama uchawi kinifikie Iran na US wangekuwa wameshautumia siku nyingi, Tanzania tarh 29 wangekuwa wameshautumia kusimamisha zoezi na kuleta vurugu.

Nadhani ni practice kama practice nyingn either kwa kutrain wanyama may be na kutumia dawa kama sumu ambayo inaweza kuleta effect kwa mwanadamu.
 
Nadhani ni uoga wa watu na hofu iliyopo kwenye jamii. Nimewahi kushuhudia matunguli lakini sidhani kama uchawi unafanya kazi in a sense kama watu wanavyoelewa. Ungekuwa unafanya kama watu wanavyo simulia nadhani effect yake tungeiona kwa watu wengi sana pengine baadhi ya viongozi wangeondolewa au kunipa madaraka.
 
Ni vitu ambavyo tulivyoshindwa tu kuvieleza tu.. ndio tunaita uchawi

Chukulia utungwaji wa mimba mpaka mtoto anazaliwa.. tusingepata mchanganuo wake tungeita tu uchawi

Unalala na mtu , anapata mimba, baada ya mda anajifungua mtoto

Yaani tusingepata ufafanuzi tungesema ni uchawi.. japokuwa tumepata ufafanuzi lakini bado ni moja kati ya miujiza…

Vimaji maji tu vije kuwa binaadamu au kiumbe mkubwa tu
 
Hakuna uchawi ni stories za kijinga tu , na hilo la kupotea kwa nyeti limebumburuka kwa sababu fahamu za watu wengi kwa sasa zimeamka sana, hebu fikiri kipindi cha nyuma hakuna elimu kubwa kwa watu ni jinsi gani walivyokuwa wanajidanganya🤔
Halafu hilo la kuona huko nyuma watu walikuwa wajinga tu sio mtazamo sahihi, ujinga upo hadi sasa na kwa kila sehemu hakuna ambako hakuna ujinga. Huko zamani watu walifanya mambo kibao tu na sayansi imekuja kuonyesha faida zake katika hayo mambo.

Shida ya huu ubishani kuhusu uchawi ni kwamba watu wanatetea tu misimamo yao, kwahiyo kivyovyote vile yeye atatea msimamo wake inakuwa kama ushabiki wa mpira tu.
 
Uzuri mmoja maujinga mnayo yaamini yanajitokeza yenywe , aya nasikia mnaibiwa nyeti
 
Mbona hata wazungu wanaamini tu uchawi na wana madarasa ya kufundisha kabisa uchawi, kuna mavitabu kibao ya wazungu wakifundisha uchawi.

Halafu afrika uchawi ni zaidi ya hicho ulichoeleza, wewe hapo umeeleza tu watu kuhusisha vitu wasivyovielewa na uchawi ila watu hujihusisha na uchawi kwa mambo mengi sana kuanzi kuhusiana na maradhi, harakati za utafutaji, kesi, kusolve mambo yao, issue za mapenzi, uzazi n.k
 
Reactions: Lax
Uchawi wa kwanza kabisa ni wa kushika akili ya mtu asione wala kujua nini kinafanyika na mwisho kushindwa kutafsiri ht anapojiuliza akili yk kuwa nachokiona ndio chenyewe au ni vipi ?
 
Reactions: Lax
Zamani watu walikua wana amini magonjwa yanatokana na hewa chafu wanayoivuta( Miasma theory) na waliamin kwa mamia ya miaka.


Germ theory ikaja batilisha na kutoa sababu za magonjwa mbalimbali.
Sio hivyo tu, kwenye miaka ya 1960s watu waliaminishwa nadharia potofu kuhusu cholestrol na hadi kutiwa hofu kula vyakula vyenye cholestrol, ila baadaye ikajulikana watu walijazwa hofu kwa kitu ambacho hakikuwa na ushahidi wa kutosha wa kisayansi.
 
Wasiojulikana wametamba Nchi nzima😆😀
Sikuoni kazi ya wachawi wamemsaidia vipi maana wanaodai wanaweza kumyeyusha mtu kwa radi
Si ungesema tu hakuna ushahidi na ukakataa kama unavyokataa mengine, muhimu wewe simamia msimamo wa kwamba hakuna ushahidi lakini hayo ya kusema mbona hawajafanya hiki na kile si hoja yenye msingi.
 
Sio hivyo tu, kwenye miaka ya 1960s watu waliaminishwa nadharia potofu kuhusu cholestrol na hadi kutiwa hofu kula vyakula vyenye cholestrol, ila baadaye ikajulikana watu walijazwa hofu kwa kitu ambacho hakikuwa na ushahidi wa kutosha wa kisayansi.
Kama uchawi unaweza kutiwa chumvi na hata hao wachwi na waganga wasing'amue kama ni ukweli ujue uchawi ni uongo ,rejea issues za ukimwi kipindi cha nyuma
 
Reactions: Lax
uchawi ulishindwa mdhuru mkoloni
Wewe unajishughulisha na mambo ya ukoloni ukiambiwa wakoloni waliwasidi wazee wetu kwa uchawi utakuja kusema nini? Ndio maana mimi sioni maana ya kushikilia habari za ukoloni wakati hata sasa kuna imani ya uchawi wa kumkinga mtu na silaha kama visu,mapanga n.k na ni katika imani zilizokuwepo kipindi hicho cha ukoloni.
 
Reactions: Lax
Kwani uchawi ni nini kwa unavyoelewa wewe hadi huo uchawi utambuwe issue ya ukimwi? Shida hapa tunakusanya kila kitu kwenye kapu moja la uchawi.
 
Kwani uchawi ni nini kwa unavyoelewa wewe hadi huo uchawi utambuwe issue ya ukimwi? Shida hapa tunakusanya kila kitu kwenye kapu moja la uchawi.
Uchawi ni hadithi za kutungwa na yale mambo yanayotokea bila kutambulika vizuri na ni kutokana na ignorance tu
 
Nani kakwambia hayo madai yamepotea mkuu? Hadi leo bado kuna imani za mtu kusumbuliwa na magonjwa ya kibaolojia yenye kusababishwa na uchawi au majini.

Shida yako unashindwa kutofautisha imani potofu na uchawi, imani potofu zimekuwepo hadi kwenye masuala yenye kuhusishwa na sayansi ndio maana nikatoa mfano wa zamani watu kupotoshwa kuhusu cholestrol na kutishwa kula vyakula vyenye cholestrol.
 
Sijazaliwa leo , uchawi na ujinga ni mapacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…