Je, kuna uhusiano kati ya IQ ya mtu na kabila lake, umasikini wake au kimo chake?

Naunga mkono hoja, hili jambo niliwahi kulizungumza pia katika mabandiko haya

Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu? - JamiiForums

Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo!. Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?!. - JamiiForums

Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye Maendeleo au kwenye Ignorance? - JamiiForums

Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision, au ni Ignorance? - JamiiForums
P
 
Pascal umesahau takwimu ya udumavu Tz 60% au !!?? Maana ungekuwa umekumbuka usingeleta mada hii. Haswa ukizingatia Udumavu unaathiri mwili na akili mbaya zaidi ukishahathirika utotoni hakuna kubadilika ataa kama utapata lishe bora baadae .Lete mada ya kupigia chapuo Lishe bora iwe kipaumbile cha kwanza cha Taifa .kama Ujerumani walivyo fanya baada ya vita kuu .hii IQ uwezi pata ndani ya wadumavu aijalishi wa kabila au dini au eneo gani .kwa lugha ingine njaa haichagui [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwa swala la IQ watu wafupi wengi ndio ma Genius mind compared to warefu ijapokuwa wana tatizo la inferiority complex, fanya utafiti vizuri utagundua hilo
 
hawa ni janga janga na ukoloni umewasupport sana kuwa juu Kielimu kinyume na hapo nothing
 
Kiukweli Pascal huwa ananisikitisha kwa posts zake za kikabila na ukanda. Sijui anajaribu kuleta ujumbe gani kwa Taifa?! Wacha tuangalie.
Karibuni na pande hii huu pia unaweza kuwa ni ukabila?.
P
 
Mikoa ambayo elimu ilipewa kipaumbele kabla ya uhuru ndio yenye maendeleo ya watu.

Kuna kipindi mabosi nane wa TRA walikuwa ni wachagga watu wakalalamika ukabila.

Lakini miaka ile ungeenda IFM na vyuo vingine vya masuala ya pesa ungekutana na wachagga wengi wakipiga kitabu.

Hivyo ulikuwepo uhusiano wa moja kwa moja kati ya vyeo vyao vikubwa na wao kuzaliwa katika mikoa yenye kuijua thamani ya elimu.

Mikoa mingine na yenyewe imetambua maana ya elimu ndio sasa tunawaona watu wa makabila mengine wakishikilia vyeo vikubwa.
 
Mkuu Naunga mkono Hoja Pwani wapo watu Smart tu Angalia akili kubwa kama Hon.Jakaya kikwete ila pia watoto wengi wa Mjini ni wa Pwani asilia. Watu kama wasukuma au wanyakyusa wanakuja tu mjini na akili za kukariri na kuvukia barabara kidogo wachaga
 
I.Q ya mtu huezi kupima kwa kutumia bunge la JMT na mithani ya bongo mzer. Halafu inamaana Ruvuma IQ yao Ni ndogo kuliko mikoa ya pwani, sio kweli broo km utakuwa umemuelewa Pascal mayalla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakula kweli kingi ila Sijui kama ni bora. Protein from 0 To 5years old mazingira yanayomsunguka
Na ishu ya genes historikali ni my humu as well nadhani cross breading nayo muhimu sana. siamini sana kwenye kundi lilolosoma sana mfano kuna
MTU katana wachaga wahaya na wanyakyusi Sijui. Nadhani Inteligence haipimwi kwa kiwango cha ufaulu peke
 
Duh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal nakubaliana na wewe kwa upande mmoja ila napingana na wewe kwa sehemu kubwa.
Hasa kwenye suala la umasikini. Kwa hapa Tanzania kuna maeneo yana umasikini wa kutisha ila ni maeneo yanayofahamika kuwa na watu wenye akili sana.
Mf. Nyasa, kwa wanyasa na Ukerewe kwa wakerewe. Haya ni maeneo ya watu wenye akili sana kwa sababu tuliosoma mashuleni na vyuoni tumekutana nao na tumewaona ila pia maeneo yao yana umasikini wa kutupwa.

Kwa mtazamo wangu, Umasikini Tanzania unatokana na Sababu Mbili kuu ambazo ni Ushirikina na Wivu wa Kijinga.

Kwa Historia maeneo mengi ya wachaga tangu miaka ya zamani hawakuwa na tabia za kishirikina hivyo kupelekea watu kupaendeleza sana kwao kwa sababu watu hawana hofu ya kupaendeleza kwao. Vilevile hawana wivu wa kijinga kwamba mtu akijenga nyumba nzuri kwao basi wanamfanyia fitna na mambo ya ajabu.
Tuseme ukweli paskali maeneo mengi ya Tanzania yapo nyuma kwa sababu ya ushirikina. Watu hawataki kupaendeleza kwao, kuendeleza maeneo yao kuogopa kurogwa au kufanyiwa mambo ya ajabu.

Kuanzia Mtwara, Lindi, Njombe Mf Ludewa hadi mkuu wa Wilaya alienda kuwatolea uvivu wananchi kwa tabia zao za kijinga za kuroga maendeleo, Dodoma,Singida, Rukwa, Katavi, Mbeya, Iringa, mikoa ya kanda ya Ziwa ni ushirikina na umefanya jamii hizi kuwa masikini na kutokuwa na maendeleo.

Kuna Taasisi moja ilifanya utafiti na ikagundua kuwa Tanzania ndo inaongoza wananchi wake kuamini kwenye ushirikina. Kwenye ushirikina watu hawana maendeleo, hawawezi kufikiri vizuri na umasikini lazima utamalaki.
 
Nakubaliana na wewe. Tuseme utamaduni wa watu unahusiana sana maendeleo yao. Kuna mtu namfahamu leo hii namshauri ajenge kibanda cha rumu japo mbili cha tofali anasema nataka afe! Maana jamaa zake wote hawana. Ukoo mzima hakuna mwenye elimu na mzazi kumwambia mtoto asiende shule ni kawaida tu. Watu wanalima hawaoni umuhimu wa mbegu bora au mbolea na dawa.
Suluhisho ni kuwabadili watu kupitia elimu.
Kwa nini maeneo mengine watu wana IQ kubwa kuliko mengine?
Kuna suala la lishe pia. Maeneo hayo utakuta yana hali ya hewa nzuri chakula ni kingi, samaki nk. Watoto wanazaliwa na kupata lishe bora kuloko maeneo mengine.
Pia urithi. Jamii yenye uwezo mkubwa wa akili huwarithisha vizazi na vuzazi.
So, utamaduni, lishe na urithi ni factors chache zinafanya jamii kutofautiana katika kiwango cha maendeleo na akili


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…