Je, kuna wanandoa wanajutia kuoa au kuolewa na wanatamani ndoa ivunjike?

Dr. Mwaka na Haji Manara ndoa zao zinapumulia mashine. Muda wowote zinavunjika
Unatoka kwenye ubachela baada ya kuoa, baada ya miaka 6 unarudi tena kwenye ubachela.
Hakuna tofauti na mtu uliyemuacha single
 
Ndoa nyingi zipo kwenye majuto 89%
Hii 89% ni kwa mujibu wa tafiti ipi?

Mimi sijaoa, ila kwa uzoefu mdogo nilionao; kuna kaukweli flani kwamba asilimia kubwa ya wanandoa hawafurahii ndoa zao (let's call it 'hypothesis formulation').

Nina rafiki yangu ameoa, yule binti aliyemuoa alikuwa mstaarabu sana kipindi cha uchumba na kipindi cha awali cha ndoa yao, ila kwa sasa binti amekuwa kitu kingine kabisa! Nafikiri mnanielewa nikisema binti amekuwa kitu kingine.

Jamaa yuko kwenye total confusion, ame-opt kujinywea pombe tu! Anatia huruma. Huyu ni mmoja kati ya wengi ambao hadithi zao za mahusiano na ndoa zinahuzunisha.

Mimi nadhani ni busara kumshirikisha Mungu kabla na baada ya kuingia kwenye sakramenti hii ya ndoa, kwasababu ipo hatari kubwa sana mbeleni kama ukiutumia ubinadamu wako kumchagua mwenza.

Unajua, wanaume wengi tunakufa mapema na kupata magonjwa yasiyoambukiza (kama presha na kisukari) kwasababu hiihii ya maswala ya ndoa. Tuwe makini sana ndugu zanguni.
 
Ukiwa kwenye ndoa kunamda unatamani ivunjike ila ikivunjika majuto yake utatamani urudishe wakati nyuma uzibe ufa
 
Mm Kwa hii miaka 10 naenjoy tu sijutii chochote na muda ukirudi nyuma ntamchumbia huyuhuyu mama watoto.
 
Hakika
 
Hizi mada nimezisoma kwamuda mrefu sama humu JF. Ila sasa hapa tulipofikia niujinga fulani wa kutaka kujazana na kulishana negativity na sumu juu ya maisha ya ndoa hasa kwasisi wanaume. Hizi mada zimeongelewa mno humu jamvini nazimepita hata na kuzikwa. Kama elimu iliyotarajiwa kutolewa ilishatolewa, sasa kinachozidi kuonekana ni childish mindset yakucheza mind games zakumuonyesha nani haitaji ndoa. Misery loves company, tuache uzinzi na kukwepa majukumu. Kitu chochote baada ya muda kinazoeleka hata kuchokwa ila there is always a way to continue as a family. Sisi ni wanaume, kutaka kujua upumbavu huo haikusaidii chochote na wala haijustify uzinzi wako, ukitaka oa usipotaka acha. Mnataka tushindane na wanawake kwenye manung'uniko si hasara ya masculinity traits kwa mwanaume sasa. Uoe au usioe, you will still die.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…