Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Imani ni kwa kitu chochote.

Kwa muktadha wa imani za kidini. Ninyi mna amini tayari kuna Mungu ila hamna uthibitisho wala uhakika.

Na hapa ndio utata unaanza.

Mnaamini kwamba Mungu yupo, ila kumthibitisha hamuwezi. Sasa huoni kwamba hayupo?

Mungu angekuwepo kweli Kusingekuwa hata na haja ya kuhoji uwepo wake.

Kila mtu angejua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho kabisa kwamba kuna Mungu.

Kulingana na maandiko yenu ya kidini. Mnatafsiri imani kama kuwa na uhakika wa jambo, kumbe kiuhalisia sio tafsiri sahihi.

Imani ni kutokuwa na uhakika, ushahidi wala uthibitisho.

Ndio

Lakini huwezi kujua mpaka ufanye uhakiki upate uhakika wa either hao ni wazazi wako kweli, Au sio wazazi wako.
Unajichanganya sana mkuu.
 
Kwa kipi nilichosema hadi ionekane hivyo?
Unasema naichukulia Sayansi kama dubwasha kitu ambacho si kweli.

Umeenda mbali kuituhumu Sayansi kuwa ni imani fulani ya dini.

Hii inaonesha mashaka juu ya elimu yako na namna ambavyo unaweza kuielezea Sayansi.
 
Aiseee!!

Kwanza natamani nikutane na huyo Mungu tufanye mjadala mkali.

Maana nina maswali mengi sana ya kumhoji na kujua uwezo wake wa kufikiri kama uko sawasawa kweli?

Na kama kweli yupo nitahitaji anipe majibu ya kueleweka.

Maana haiwezekani aumbe viumbe vije viteseke duniani, Halafu yeye anakula bata huko mbinguni halafu akiombwa aje atoe msaada japo kidogo hapa duniani haonekani kwenye jambo lolote kusaidia.

Watu wanazidi kuteseka na kuumia tu.

Sasa kama kweli Mungu yupo, Alituumba kwa nini?

Aje atutese duniani, Halafu baadae ndio tuje kui enjoy mbinguni!!!

Hivi hii ni akili ya namna gani kama sio makusudi haya?

Yani unaumba kiumbe ukitese kwanza, Halafu baadae ndio uje ukipe raha!!

Hivi hii ni akili au matope
Yani kama huyo Mungu yupo,

Anastahili kufurushwa kabisa maana hajielewi kabisa.
Sema una hoja Ndugu usipuuzwe
 
Aliyeweka kumjua si muhimu. Tunajadili hoja hatujadili mtu.

Wikipedia ina njia zake za ku verify taarifa na ndio maana kuna link za external sources ambazo unaweza kuzitumia kuhakiki taarifa kama legit.

Link hii hapa

Kuhusu Makavel kuwa na miungu mingi halafu wao wakiamini kwenye hiyo miungu yao hakuna Mungu muumba kwasababu waliamini Mungu mkuu ni yule ambaye ameumba mbingu na nchi ambaye sio miongoni mwa miungu yao.

Haina maana kwamba na dini zingine zenye kuamini Mungu zaidi ya mmoja nazo ziwe na mtizamo huo.

The fact kwamba kuna dini inaabudu miungu zaidi ya mmoja ambao hakuna Mungu muumba, haiwezi kuwa sheria ya kufanya dini zingine zinazoamini Mungu zaidi ya mmoja nazo zisiwe na Mungu anayehusika na uumbaji.

Sasa hili ndio tatizo, ndio maana unashindwa kujenga hoja na kutetea hoja, lazima tujue nani aliyeanzisha.

Usinipe link, wapi ametoa hizo habari. Hata wewe unaweza unaweza kuweka unachotaka. Watu wa elimu Wikipedia sio marejeo.
 
Uwe unajibu maswali ninayo kuuliza.
Najibu, na pale ambapo hoja yako imekuwa vague lazima uulizwe pia swali ili kuondoa ambiguity ili na mimi niweze kutoa jibu sahihi.

Kwa hiyo usiweke ionekane kwamba wewe tu unayeuliza maswali haupaswi kuulizwa maswali haya pale inapotokea maswali yako yanahitaji kujibiwa kwa maswali zaidi ili kuyafanya yaeleweke.
 
Sasa hili ndio tatizo, ndio maana unashindwa kujenga hoja na kutetea hoja, lazima tujue nani aliyeanzisha.

Usinipe link, wapi ametoa hizo habari. Hata wewe unaweza unaweza kuweka unachotaka. Watu wa elimu Wikipedia sio marejeo.
Kwanini iwe ni lazima?
 
Wala sijichanganyi, Wewe ndiye ambaye huelewi vizuri.
Kama unachokiandika mkuu hakieleweki unafikiri nitaelewaje? Imani umefanya kitu chenye kuhusu wakati ujao tu wakati unajua kuna vitu ambavyo ni vya kiimani ila ni vya wakati uliyopita na vyengine wakati uliyopo, sasa unadhani hapo mkuu mtu ataweza kukuelewa?
 
Uliona neno "muktadha wa kidini" kwenye kile nilicho kuwa nimeandika kwenye ile post?

Imani inaweza kuwa kwenye jambo lolote in future.

Lakini Mimi naongelea specifically kwenye "imani za kidini kuhusu uwepo wa Mungu"

Hapa ninyi waamini Mungu ndio mna amini Mungu tayari alikuwepo na yupo siku zote. Kitu ambacho sio kweli.

Hivyo imani yenu kusema Mungu yupo haina ukweli.
 
Unasema naichukulia Sayansi kama dubwasha kitu ambacho si kweli.

Umeenda mbali kuituhumu Sayansi kuwa ni imani fulani ya dini.

Hii inaonesha mashaka juu ya elimu yako na namna ambavyo unaweza kuielezea Sayansi.
Hakuna niliposema sayansi ni imani ya dini bali nimesema unafanya sayansi kama imani fulani ya dini, labda iwe ndio mara ya kwanza wewe kusikia ila wapo watu hufanya sayansi kama dini. Yani watu ambao mnafanya sayansi ndio muamuzi wa kuamuwa kipi cha kweli na kama sayansi haijaeleza kitu hicho basi mnachukulia ni uongo au hamkizingatii.
 
Ndio kukosea kwenyewe huko.
 
Uliona neno "muktadha wa kidini" kwenye kile nilicho kuwa nimeandika kwenye ile post?

Imani inaweza kuwa kwenye jambo lolote in future.

Lakini Mimi naongelea specifically kwenye "imani za kidini kuhusu uwepo wa Mungu"

Hapa ninyi waamini Mungu ndio mna amini Mungu tayari alikuwepo na yupo siku zote. Kitu ambacho sio kweli.

Hivyo imani yenu kusema Mungu yupo haina ukweli.
Sijazungumzia kuwa hiyo imani ni kweli au sio kweli.
Hoja yangu ni huko kusema kwamba imani inahusu jambo la future tu.
 
Sijazungumzia kuwa hiyo imani ni kweli au sio kweli.
Hoja yangu ni huko kusema kwamba imani inahusu jambo la future tu.
Kwa ufupi ni kwamba imani ni kwa jambo ambalo huna uhakika nalo.

Ukishakuwa na uhakika huitaji tena imani.
 
Back
Top Bottom