Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Tutajiuliza maswali mengi Kuhusu Mungu ila ukisoma vitabu vya dini vinaongelea busara na hekima za kushinda dunia hii soma vizuri utajifunza mengi nakuona hekima iliyomo hayo mengine yatakuumiza kichwa maana kila dini inazungumza life wisdom tu jinsi ya kuthamini maisha jinsi ya kua muaminifu jinsi ya kua mtu kwenye hekima mafunzo ni mengi natamani ningeshiba dini mwanzo kabla sijaanza kutafta maisha
 
Mungu ni waajabu sana yeye anaona wavaa kobazi wanavojilipua na kukata shingo za makafiri ila yeye ametulia huko aliko akiaangalia watu wanapigana mashine Janah
 
Aiseee!!

Kwanza natamani nikutane na huyo Mungu tufanye mjadala mkali.

Maana nina maswali mengi sana ya kumhoji na kujua uwezo wake wa kufikiri kama uko sawasawa kweli?

Na kama kweli yupo nitahitaji anipe majibu ya kueleweka.

Maana haiwezekani aumbe viumbe vije viteseke duniani, Halafu yeye anakula bata huko mbinguni halafu akiombwa aje atoe msaada japo kidogo hapa duniani haonekani kwenye jambo lolote kusaidia.

Watu wanazidi kuteseka na kuumia tu.

Sasa kama kweli Mungu yupo, Alituumba kwa nini?

Aje atutese duniani, Halafu baadae ndio tuje kui enjoy mbinguni!!!

Hivi hii ni akili ya namna gani kama sio makusudi haya?

Yani unaumba kiumbe ukitese kwanza, Halafu baadae ndio uje ukipe raha!!

Hivi hii ni akili au matope
Yani kama huyo Mungu yupo,

Anastahili kufurushwa kabisa maana hajielewi kabisa.
Umesahau point moja, why alituumba hili aje atuchome moto, na according na wafuasi wake alitupa utashi makusudi tunafanye tunachotaka but so some reason ana chukia tukifanya baadhi ya mambo
 
Tutajiuliza maswali mengi Kuhusu Mungu ila ukisoma vitabu vya dini vinaongelea busara na hekima za kushinda dunia hii soma vizuri utajifunza mengi nakuona hekima iliyomo hayo mengine yatakuumiza kichwa maana kila dini inazungumza life wisdom tu jinsi ya kuthamini maisha jinsi ya kua muaminifu jinsi ya kua mtu kwenye hekima mafunzo ni mengi natamani ningeshiba dini mwanzo kabla sijaanza kutafta maisha
Ukishasema vitabu vya dini unakuwa unajitoa kwenye logic.

Kwa nini Mungu awaache wafuasi wake watutukane na kukata watu kisa tu hawakubaliani na wao...
 
Nitakuuliza kwanini kuamini kuwe ni muhimu kuliko kujua
Sijazungumzia umuhimu na wala neno kujua kinyume chake si neno kuamini, mara nyingi nasema kuwa kujua hakuna maana ya kwamba hicho unachokijua ndio ukweli na si vinginevyo.
Huko kuhusisha neno kujua na uthibitisho sijui mmetolea wapi? Kama neno kujua lingekuwa na maana ya kuwa na uthibitisho basi tungekuwa tunalitumia kwa uchache mno katika mazungumzo yetu ya kila siku.

Labda nikuulize unaposema hauamini kitu fulani, huwa unakusudia nini kwa kusema kuwa haumini hicho kitu?
 
Huyu pepo anaewavagaa watu watake uthibitisho wa uwepo wa Mungu.
Ni pepo yule yule aliekuwa amewavagaa wale askari yesu alipokuwa msalabani
KAMA KWELI NI MWANA WA MUNGU SHUKA MSALABANI/OTEA NANI ALIEKUPIGA.
MUngu hayupo kwa kila mtu
Yeye hujionyesha kwa wanaomtafuta. Si wamaonyesho
Hata kifo msalabani hakikuwa kwa ajil ya watu wote
Ila aliopewa
Mmoja alikuwa anaubishi wako alipokufa alimwona upande wapili lazaro akiwa amejilaza kifuani kwa ibrahim akamwomba ampake ata mate kwa tabu anazopitia
Kisha akamwomba ibrahim amtume lazaro duniani akawambie ndugu zake kuwa yanenwayo yamoo
Akajibiwa hata uko duniani wapo wanaohubiri nakuwaambia na hawaawaamini.

Kama huamini endelea kutokuamini,ila kuna watu huwezi ukawambia hayupo kwa sababu washawaona,wengine wametokewa mpaka na malaika
Mimi binafsi nimetokewa na kiumbe cha kimbinguni cha ajabu nikiwa na jamaa yangu kwenye maombi tuu.
Radi ilitoka kwenye ardhi,ukubwa kimo cha mtu mrefu.
Nimeshuhudia mengi mnooo.
Alishapoteza ngoma na TB kwa vipindi tofauti kwangu nawakati huo madaktari walithibitisha na sayansi na vipimo na vikapotea.
Ni mambo mengi mnoo mnoo mnoo

Usimtafute mungu kwa hisi tano za kimwili
Mungu si wa kimwili.
Hisi tano ulipewa uweze kuishi duniani na ku interact.
Ila mkristo halisi amepewa hisi ya sita.
Kuona visivyoonekana,kusikia visivyosikika.
Kuishi yasiyowezekaana
Paulo alitokewa na yesu kama nuru na aliiona peke yake moaka akawa kipofu,lakini wengine hawakuiona
Yohana mbatizaji aliona njiwa akimshukia yesu peke yake kwenye umati wa wtu
Mungu hujionyesha kwa ampendae,na amtafutae

Na ukishamthibitisha hakuna mjinga atakaekuambia hayupo.
 
Wewe unashinda na mamovie ya Hollywood,unakesha bar
Unafatilia ushoga.
Mamiziki ya kilimwengu umoo.
Unavuta bangi ama sigara,
Umelelewa kishua shua,mayai+ ushoga na single mama.
Hujawahi kumtafuta Mungu,unaenda kanisani kwa sbabu umezaliwa kwnye ukristo.
Wewe unatarajia utamuona Mungu.
Muda uo wapo watu wanataabika kwa uchafu unaoendelea kwenye dunia hii.
Wanaomba Mungu kila siku awaepushe.
Aache kuwatokea hao aje kwako ambae umeanguka kwenye uongo duuuuuuni wamwisho kabisa wa ibilisi kuwa Mungu hayupo.?
 
Sijazungumzia umuhimu na wala neno kujua kinyume chake si neno kuamini, mara nyingi nasema kuwa kujua hakuna maana ya kwamba hicho unachokijua ndio ukweli na si vinginevyo.
Huko kuhusisha neno kujua na uthibitisho sijui mmetolea wapi? Kama neno kujua lingekuwa na maana ya kuwa na uthibitisho basi tungekuwa tunalitumia kwa uchache mno katika mazungumzo yetu ya kila siku.

Labda nikuulize unaposema hauamini kitu fulani, huwa unakusudia nini kwa kusema kuwa haumini hicho kitu?
Hujazungumzia umuhimu ila kwangu naona kujua ndio kitu muhimu zaidi.

Kuamini ni kama betting
 
Hujazungumzia umuhimu ila kwangu naona kujua ndio kitu muhimu zaidi.

Kuamini ni kama betting
Hakuna umuhimu kwenye kujua kwa sababu unaweza ukawa unajua kisicho cha kweli pia, kujua haijalishi unachojua kimejengwa kwenye msingi wa kweli,imani au uongo.

Nikikuuliza unamjua mungu Krishna Utanijibu nini?

Kuamini ni sehemu ya maisha ya mwanadamu, na kama kuamini ni kama kubet ina maana kuna muda hutokea kweli unachoamini sasa kwanini wewe ukatae kabisa kuamini?
 
Kwenye "kujua" zipo njia za ku-verify "jawabu" kwa hiyo bado kujua ni muhimu zaidi kwasababu hata baada ya kupata jibu. Jibu linaweza kuhakikiwa kama ni kweli limefuzu sifa ya kuwa jibu.
 
Maelfu ya watoto wadogo wasio na hatia yeyote ile wamekufa sana huko Gaza na huyo Mungu anayedaiwa yupo anatuangalia muda wote na anatupenda, Hajafanya chochote kile kusaidia!!👇
View attachment 3178160
Hii picha inasikitisha sana jamani.Kumzika mtoto wako tena umemuokota kwenye hali hii?Haya maumivu hayaelezeki.Ee Mungu dunia hapa sio nyumbani kwetu natumaini wamepata kheri ya milele .Amen.Vita inasaidia nini kwa nini watu wasikae wakaongea yakaisha madhara yake ni haya wanateseka wasiohusika
 
Kwenye "kujua" zipo njia za ku-verify "jawabu" kwa hiyo bado kujua ni muhimu zaidi kwasababu hata baada ya kupata jibu. Jibu linaweza kuhakikiwa kama ni kweli limefuzu sifa ya kuwa jibu.
Kujua ni muhimu zaidi dhidi ya nini? Mbona unalazimisha ushindani usiokuwepo?

Nimekuuliza unamjua mungu krishna?
 
Back
Top Bottom