Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Kabla ya kujibu swali lako kwanza nijibu langu, chanzo cha Mungu ni kipi?
 
Kujua ni bora zaidi kuliko kuamini.

Kwa nini huyo Mungu ajifiche na aachie watu wakisie uwepo wake ilhali angeweza tu kujitokeza na wote tukamjua?

Kujificha kuna maana nani ? Au nani amekwambia Mungu amejificha ? Kwahiyo kila ambacho hakionekani kimejificha ?

Kingine watu hawakisii juu ya uwepo wa Mungu, bali ni hakika. Tena yeye Allah ndio aliwachagua miongoni mwa waja wake akawafanya kuwa mitume na manabii.

Unatofautisha vipi kujua na kuamini ? Shida naiona ni kwamba mna ufahamu mdogo sana juu ya tamko Imani na kuamini.
 
Imani ya Mola haitaki kubahatisha, hata ukiamini kwa lengo la kwamba ukimkuta iwe kheri kwako, hapa Imani yako sio sahihi na utaenda motoni tu. Bali Imani ya Mola inataka elimu, mazingatio na uhakika usilo kuwa na shaka kabisa, kwa ufupi ni mchakato wa muda mrefu wenye kuambatana na utiifu na kumpwekesha yeye katika ibada.

Ndio maana Allah anataka watu wenye kutafakari kwa kina na wenye mazingatio.
 
Imani ni nini?
 
Kabla ya kujibu swali lako kwanza nijibu langu, chanzo cha Mungu ni kipi?
Mkuu hoja kuwa huamini uwepo wa Mungu mimi nimekuacha nayo, nimeomba kuanzisha hoja nyingine kwenu nyie msio amini uwepo wa Mungu, mtuambie kwa kuthibitisha chanzo cha huu ulimwengu na viumbe vyake ni nini?
Ukishindwa kujibu hili basi ujijue bado we ni mweupe sana
 
Duh! We jamaa naona hatuelewani kabisa una tatizo la kushindwa kuelewa unachosoma.

Nachokupinga ni hizo kauliza za kusema sayansi inakubali kukosolewa mara sayansi inasema, unafanya sayansi ni kama mtu hivi kitu ambacho naona unakosea kuelezea hivyo. Mimi sipingi sayansi wala kuidharau sayansi.
 
Sasa ushajua hatima inayokusubiri ikiwa hautaamini hizi habari. Je tayari ushaanza kuwa muumini wa Anubis?

Kitu ambacho hamkijui ni kuwa, Imani nayo uhakikiwa.

Kwanza lazima tuzohakiki habari hizi zinazowa husu Wamisri na Imani yao hii. Wapi chimbuko la Imani hii ?
 
Mkuu hoja kuwa huamini uwepo wa Mungu mimi nimekuacha nayo, nimeomba kuanzisha hoja nyingine kwenu nyie msio amini uwepo wa Mungu, mtuambie chanzo cha huu ulimwengu na viumbe vyake ni nini?
Ukishindwa kujibu hili basi ujijue bado we ni mweupe sana
Sijui kama umenielewa lakini🤔 kwani nilazima kila kitu kiwe na chanzo?
 
Kujua kipo ndani ya Imani. Lazima kwanza ujue hakika ya jambo fulani kisha unaliweka moyoni na kulisadiki na kulifanyia kazi jambo husika.
Unachokifanya wewe ni kulazimisha jibu ambalo sio sahihi liwe sahihi . Ni kwamba hujui tofauti ya kujua na kuamini kweli?
 
Sijui kama umenielewa lakini🤔 kwani nilazima kila kitu kiwe na chanzo?
Wewe unataka kunirudisha kwenye maswali yenu ya kila siku, Mimi nakutoa huko nimekuuliza swali dogo unaruka ruka
 
Na kwa hilo unapaswa kufuata mafundisho yote yaliyoandikwa katika Quran tukufu, kwa kufanya hivyo utakuwa umeepuka moto na kuzawadiwa bikra 72 peponi.

Tunasema kuhakiki hiki unachokiandika, hizi habari za kuwa Kuna kuzawadiwa mabikra 72, umezipata wapi ? Umezisikia tu pasi na kulifanyia uchunguzi au unazijua kwa kulifatilia na kuzihakiki ?
 
Unachokifanya wewe ni kulazimisha jibu ambalo sio sahihi liwe sahihi . Ni kwamba hujui tofauti ya kujua na kuamini kweli?

Unatakiwa ukosoe nilicho kiandika kwa wewe kuandika kilicho sahihi.

Najua tofauti ya kujua na kuamini ndio maana nimeandika hayo.

Kwetu sisi Waislamu huanza kwanza elimu kisha kauli na vitendo.

Sasa jadili jambo kielimu.
 
Wewe unataka kunirudisha kwenye maswali yenu ya kila siku, Mimi nakutoa huko nimekuuliza swali dogo unaruka ruka
Ukisha thibitisha uwepo wa Mungu hakuna swali litakalo jirudia , yani hata huu mjadala hautakuwepo ni sawa natuanze kuuliza je mama samia yupo?
 
Mungu hayupo kila mahali, hii ni Imani potofu.

Mungu ana umbile na Wala Mungu sio Roho, yeye ndio ameumbwa hizi roho.
 
Unatakiwa ukosoe nilicho kuandika kwa wewe kuandika kilicho sahihi.

Najua tofauti ya kujua na kuamini ndio maana nimeandika hayo.

Kwetu sisi Waislamu huanza kwanza elimu kisha kauli na vitendo.

Sasa jadili jambo kielimu.
Wewe unahubiri tu kila siku wala haujawahi thibitisha uwepo wa Mungu , unachokifanya unataka niamini mahubiri yako ,wakati mimi sitaki kuamini nataka nijue sijui kama unaelewa🤔
 
Ukisha thibitisha uwepo wa Mungu hakuna swali litakalo jirudia , yani hata huu mjadala hautakuwepo ni sawa natuanze kuuliza je mama samia yupo?
Umeshindwa kujibu, kwa maana hiyo hujui chochote kuhusu huu ulimwengu, Atheist ni watu ambao wamekosa majibu ya maswali fikirishi kuhusu chanzo cha huu ulimwengu wakakimbilia kwenye conclusion bila kutaka kujifunza maarifa mapya
 
Hivi umesoma vizuri nilichokiandika ? Kwanini kwanza unahisi lazima kuwe na chanzo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…