Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Jesus is here on earth physically
kwa kweli nimefurahi kujua hili baada ya macho Yangu kufunguka .yupo duniani tayari ila wengi kumjua ni vigumu maana amekuja kama a blackman
 
Kwangu Mimi Mungu yupo na anatenda matendo makuu.. Matendo hata ndio yanayonithibitishia uwepo wake.. Nilimuomba anipe mke na akanipa mke ambaye hata kama ningepewa nafasi kumi za kuchagua mke Tena Bado ningemchagua yeye..

Nimemuomba kuwajengea nyumba ya kuishi wanangu kabla hawajaanxa darasa la kwanza, nikaweza kuwajengea wanangu nyumba ya vyumba vinne sitting room kitchen etc ndani ya mwezi mmoja

.Matendo haya makuu aliyonitendea kwangu ni ushuhuda wa uwepo wa Mungu..

Wasioamini uwepo wa Mungu hayo ni matatizo yao ..
 
We ulikuwa ni mmoja wao wa watu walioamini Kikombe cha babu kinatibu ukimwi?

Kujibu hoja yako....

Unaposema hakuna uthibitisho wa kisayansi kwenye dawa za asili, unakuwa unalenga uthibitisho unaohusu nini?

Kwamba sayansi inasema hakuna uthibitisho kuwa hizo dawa zinatibu??

Kama jibu lako ni ndio basi utakuwa unakosea.

Japo ni kweli usiopingika kuwa katika sayansi dawa za asili zipo limited sana. Lakini bado haiondoi maana kuwa Sayansi inatambua zipo dawa za asili zenye uwezo wa kutibu magonjwa.

Mwaka 2015 WHO waliipitisha rasmi dawa ya kiasili ya kichina inayoitwa Artemisinin kama dawa rasmi ya kutibu Malaria.

Kwa hiyo sio kweli kuwa Sayansi inasema dawa za asili hazina uthibitisho kisayansi. Japo kuwa zipo pia dawa ambazo zinadaiwa kutibu baadhi ya magonjwa ambayo Sayansi im

Sayansi inasema hakuna uthibitisho wa kisayansi kuhusiana na efficacy zake hivyo utumiaji wa dawa za asili unaweza kuleta athari zaidi kwa mtumiaji.

Pia kunaweza kuwepo na hatari ya muingiliano wa dawa zingine na kusababisha tatizo lingine kiafya.

Sababu nyingine ambayo sayansi imeweka angalizo ni kuhusiana na kipimo rasmi cha dozi kwenye dawa hizo za asili mara nyingi dozi ni vague.

Kipimo cha dawa alichokunywa baba ndio kipimo hicho hicho anachopewa mtoto.
Mimi naposema hakuna uthibitisho wa kisayansi nina maana hakujafanyika utafiti wa kisayansi au hakuna maelezo ya kisayansi na si kwamba nachukulia sayansi kama imani fulani au dude fulani hivi ambalo ndio linaamua hivi na vile kama ambavyo wewe unachukulia.

"Kwahiyo sio kweli kuwa Sayansi inasemadawa za asili hazina uthibitisho kisayansi" kauli kama hii inanishangaza inanifanya njiulize kwani unaichukuliaje sayansi?

Nachosema ni kwamba zipo dawa za asili ambazo hujulikana faida zake katika aina ya magonjwa fulani na fulani na watu hutumia, lakini baadhi ya madai yake katika hizo faida zake unakuta hazina ushahidi wa kisayansi wenye kusapoti hayo madai japo watu hutumia na kupona.
 
Kila mtu alizaliwa Atheist bila kuwa na imani yeyote ile. Mpaka pale ulipo aminishwa na kukaririshwa kwenye imani za kidini na wazazi wako au walezi wako.

Kwa hivyo wewe ndio bendera fuata upepo wa dini za kuletewa.
Atheist hana imani yeyote au anapinga imani? Sio nyie mnaosema hamtaki kuamini mnataka kujua? Sio nyie mnaosema hakuna Mungu kwa sababu hakuna uthibitisho wa kuwepo kwake?

Sasa hapo utasemaje tunazaliwa tukiwa atheists ikiwa atheists wenyewe wana misimamo yao?
 
Kama sarakasi ni kwa ajili ya maonesho basi ngoja nibadilishe mfano.

Vipi kuhusiana na ufanyaji ngono? Hii pia si tunakubaliana kuwa ni sehemu ya maisha ya watu??
Ndio ngono ni sehemu ya maisha ya watu, kupitia huko hupata kuzaliana.
 
Atheist hana imani yeyote au anapinga imani?
Atheist hana imani ya Mungu au miungu.
Sio nyie mnaosema hamtaki kuamini mnataka kujua? Sio nyie mnaosema hakuna Mungu kwa sababu hakuna uthibitisho wa kuwepo kwake?
Tunapinga madai yenu ya kusema kuna Mungu.

Sisi hatuhitaji kuamini Mungu yupo, tunahitaji nyie waamini Mungu mnayedai kuna Mungu mumthibitishe huyo Mungu na mthibitishe mlijuaje yupo?

Ili tujiridhishe na tuhakikishe hayo madai yenu kama yana ukweli au ni imani zenu tu zisizo na uthibitisho wowote ule.
Sasa hapo utasemaje tunazaliwa tukiwa atheists ikiwa atheists wenyewe wana misimamo yao?
Atheist ni binadamu asiye na imani ya Mungu wala miungu.

Kila mtu alizaliwa Atheist, Bila kuwa na imani ya Mungu au miungu. Mpaka pale ulipo aminishwa, kukaririshwa na kuridhishwa imani za kidini na wazazi au walezi wako.

Ndipo ukawa Theist.
 
Swali: Je Atheists hawatuogopi siku ya mwisho kukutana na hukumu ya Mungu na kutupwa kwenye moto wa milele?
🤔
Wakati mwingine huwa najiuliza na kukosa majibu. Kwa mfano ukiwa na mwanao akawa na tabia za ajabu na kukera mfano Wizi, Umalaya, Ujinga ujinga nk.
Je utamchoma moto kwa sababu ya hizo tabia na matendo yake ?
Na maandiko matakatifu yanasema Mungu ni pendo yaani ana upendo na huruma sasa kwanini siku ya mwisho aje akubanike kwenye moto ?
Kuna nadharia nyingi sana ambazo huwa zinafikirisha na ukijifikirisha sana unakosa hata majibu.
 
Mimi naposema hakuna uthibitisho wa kisayansi nina maana hakujafanyika utafiti wa kisayansi au hakuna maelezo ya kisayansi na si kwamba nachukulia sayansi kama imani fulani au dude fulani hivi ambalo ndio linaamua hivi na vile kama ambavyo wewe unachukulia.

"Kwahiyo sio kweli kuwa Sayansi inasemadawa za asili hazina uthibitisho kisayansi" kauli kama hii inanishangaza inanifanya njiulize kwani unaichukuliaje sayansi?

Nachosema ni kwamba zipo dawa za asili ambazo hujulikana faida zake katika aina ya magonjwa fulani na fulani na watu hutumia, lakini baadhi ya madai yake katika hizo faida zake unakuta hazina ushahidi wa kisayansi wenye kusapoti hayo madai japo watu hutumia na kupona.
Wapi nimesema kuwa sayansi ndio inayoamua hivi na vile?

Mbona unanipakazia maneno ambayo mimi sijayasema?

Sayansi ni elimu ya iliyozingatia kufanya tafiti kuhusu natural phenomena zilizotuzunguka.

Wapi katika maneno hayo kunafafanua kuwa Sayansi ndio inayoamua hiki na kile??

Unajua kuwa Sayansi inakubali kuwa haipo perfect kwenye tafiti zake na hivyo inatoa mwanya kuruhusu ukosoaji kwa wale wenye majibu mazuri zaidi?

Unaelewa kwamba Sayansi ikisema Cyanide ni kemikali yenye sumu, hakuna maana ni maamuzi yaliyofanywa na watu baada ya kupatikana kwa kura nyingi zilizokubali kuwa ni sumu bali yemyewe inakuwa imetimiza wajibu wake kwa kutoa majibu kulingana na tafiti zilizofanywa?
 
"Kwahiyo sio kweli kuwa Sayansi inasemadawa za asili hazina uthibitisho kisayansi" kauli kama hii inanishangaza inanifanya njiulize kwani unaichukuliaje sayansi?
Sijui unasomaje.

Nimekuambia hivi, dawa nyingi za kiasili zipo limited sana kuwa approved kulingana na efficacy zake.

Sayansi inapishana mtizamo na hizo dawa kwenye swala zima la ufanisi linaloweza kusababisha side effects zenye hatari kwenye afya ya mtumiaji.

Na mimekuelezea kwa kirefu kwanini sayansi inaseme dawa hizo zinaweza kuleta athari kwa binadamu.

Lakini kama haitoshi nimekupa mfano hapo wa dawa ya kiasili ya kichina ambayo WHO waliidhinisha rasmi mwaka 2015 kama tiba ya malaria.

Kipi hujaelewa?
 
Ndio ngono ni sehemu ya maisha ya watu, kupitia huko hupata kuzaliana.
Wanaoifanya hiyo ngono wakiwa makwao na privacy zao, na wale wanaofanya ngono kwenye maonesho hadharani je ni nani kati ya hao anakuwa hajafanya ngono?
 
🤔
Wakati mwingine huwa najiuliza na kukosa majibu. Kwa mfano ukiwa na mwanao akawa na tabia za ajabu na kukera mfano Wizi, Umalaya, Ujinga ujinga nk.
Je utamchoma moto kwa sababu ya hizo tabia na matendo yake ?
Na maandiko matakatifu yanasema Mungu ni pendo yaani ana upendo na huruma sasa kwanini siku ya mwisho aje akubanike kwenye moto ?
Kuna nadharia nyingi sana ambazo huwa zinafikirisha na ukijifikirisha sana unakosa hata majibu.
Na anafaidika nini yeye kukuchoma kwenye moto?

Je anafanya hivyo kutuliza hasira zake?

Kama ana hasira basi sio mkamilifu kwasababu hasira ni product ya emotion ambayo huja baada ya kushindwa kuihimili.
 
Mkuu ndio hapo huwa nawaza na kuwazua na majibu huwa siyapati.

Wakati mwingine huwa nawaza sana kuhusu haya maandiko matakatifu, Sijui kama ni kweli yalitoka kwa Mungu au Wazungu na Waarabu waliamua kututisha sisi Binadamu.
 
Mkuu haya maandiko yana hitilafu nyingi ambazo ukisoma utaelewa tu hayaandikwa na Mungu wala watu walioongozwa na Mungu.

Kitabu ambacho kimeandika kuwa mtumwa anapaswa awe mnyenyekevu kwa boss wake ni rahisi kufikiria kuwa aliyeandika ni Slave master mwenyewe.

Kitabu ambacho Mungu anatoa maagizo ya kuangamiza watoto wa uzao wa kwanza wasio na hatia kwasababu tu ya kumkomoa farao, hakiwezi kuwa kimeandikwa na Mungu mwenye upendo wote.
 
Atheist hana imani ya Mungu au miungu.

Tunapinga madai yenu ya kusema kuna Mungu.

Sisi hatuhitaji kuamini Mungu yupo, tunahitaji nyie waamini Mungu mnayedai kuna Mungu mumthibitishe huyo Mungu na mthibitishe mlijuaje yupo?

Ili tujiridhishe na tuhakikishe hayo madai yenu kama yana ukweli au ni imani zenu tu zisizo na uthibitisho wowote ule.

Atheist ni binadamu asiye na imani ya Mungu wala miungu.

Kila mtu alizaliwa Atheist, Bila kuwa na imani ya Mungu au miungu. Mpaka pale ulipo aminishwa, kukaririshwa na kuridhishwa imani za kidini na wazazi au walezi wako.

Ndipo ukawa Theist.
Hakuna mtoto anayezaliwa akiwa anaamini au haamini, suala la kuamini au kutokuamini linahitaji ufahamu na mtoto hana huo ufahamu wa hayo mambo hivyo ni mambo tunayojifunza kutoka kwa wazazi na jamii. Huwezi kusema mtoto mdogo haamini Mungu wala miungu wakati hata hajui kama kuna madai ya kuwepo Mungu wala miungu.
 
Mkuu haya maandiko yana hitilafu nyingi ambazo ukisoma utaelewa tu hayaandikwa na Mungu wala watu walioongozwa na Mungu.

Kitabu ambacho kimeandika kuwa mtumwa anapaswa awe mnyenyekevu kwa boss wake ni rahisi kufikiria kuwa aliyeandika ni Slave master mwenyewe.

Kitabu ambacho Mungu anatoa maagizo ya kuangamiza watoto wa uzao wa kwanza wasio na hatia kwasababu tu ya kumkomoa farao, hakiwezi kuwa kimeandikwa na Mungu mwenye upendo wote.
Kwahiyo wewe unamjua vizuri sana Mungu?
 
Wanaoifanya hiyo ngono wakiwa makwao na privacy zao, na wale wanaofanya ngono kwenye maonesho hadharani je ni nani kati ya hao anakuwa hajafanya ngono?
Yani wewe hubadilikagi ni mzito kuelewa.

Hivi wewe unaweza kufananisha ngono inayofanywa na wacheza filamu za ngono na ngono inayofanywa na watu wa kawaida katika faragha? Lengo la ngono ni kufanya kama maonesho hadharani?
 
Hizo ni kauli mbiu (motto ) tu za dini zisikuchanganye ukajihisi kana kwamba wewe ndio special sana na kwamba wenzako ni inferior kwasababu wamekosa kauli mbiu kama hizo.

Hiyo ni kauli mbiu tu ya kiuhamasishaji ni sawa na "Daima mbele nyuma mwiko"

Ukristo wanayo kauli mbiu yao inasema "Yesu ndio njia ya ukweli na uzima"

Sidhani kama mkristo akitamka maneno hayo yatakufanya ukubaliane na Mungu Yesu.
Simba nguvu moja😁
 
Sijui unasomaje.

Nimekuambia hivi, dawa nyingi za kiasili zipo limited sana kuwa approved kulingana na efficacy zake.

Sayansi inapishana mtizamo na hizo dawa kwenye swala zima la ufanisi linaloweza kusababisha side effects zenye hatari kwenye afya ya mtumiaji.

Na mimekuelezea kwa kirefu kwanini sayansi inaseme dawa hizo zinaweza kuleta athari kwa binadamu.

Lakini kama haitoshi nimekupa mfano hapo wa dawa ya kiasili ya kichina ambayo WHO waliidhinisha rasmi mwaka 2015 kama tiba ya malaria.

Kipi hujaelewa?
Wewe ndio hujanielewa mimi, hata sijui hayo maelezo unanielezea mimi kwa maana gani?

Hakuna naposema kuwa dawa za asili zinapigwa na sayansi maana naona maelezo yako ndio yanaeleza hivyo, nachosema ni kutokuwepo na tafiti za kisayansi au kutokuwa na maelezo ya kisayansi kwa baadhi ya dawa au tiba ila ijapokuwa watu hutumia na kupona.

Na si dawa za asili tu hata sasa kuna vitu vyenye kudaiwa kuwa na faida mbalimbali za kiafya ila hakuna ushahidi wa kisayansi kusapoti hayo madai, hicho ndio nachozungumzia mimi hapa.
 
Back
Top Bottom