Ndio maana nikakuuliza nijue ni kipi ulichotumia kujua Miungu feki ambacho waumini wa hiyo Miungu wameshindwa kukitumia kukijua u fake wa Mungu wao ili nao waachane na Mungu wao feki waungane kuabudu Mungu wako ambaye ni original?
Tatizo lako sio issue ya mungu feki, bali ni dini feki. Lakini naelewa pia filosofia ya Mungu feki inatoka wapi. Tuanze na hilo. La msingi ujue mungu feki na dini feki vipo karibu sana, lakini unaweza kuwa na dini feki ambayo iinadai inakubalika na Mungu wa kweli. Hilo ni jambo jingine.
Mtu anaweza kusema anamwabudu Mungu wa kweli alieumba dunia na mbingu, ikawa ni sawa, lakini tatizo ikawa anafanya ibada feki. Unapaswa kutambua hilo
Kumbuka kwamba miungu feki kimsingi ni nafasi inayochukuliwa aidha na shetani moja kwa moja au na malaika walioasi kwa kumuunga mkono shetani. Wapo hapa duniani. Yaani kwa mfano, wewe hapo kwako ukiamua uwe na mungu wako katika kibuyu fulani ulicho nacho, hao malaika walioasi watakinafsisha (kukipa unafsi) hicho kibuyu kiasi kwamba kuna mambo unaweza kukiomba na kikakufanyia. Hivyo hivyo kwa mti, sehemu ya tambiko nk. Kitu chochote unachoamua kikiabudu hawa malaika walioasi wanaki-animate na kinakuwa na unafsi fulani wa kuweza kuwa na communication na wewe. Lakini sasa kumbuka wanaofanya hivyo na kuwa miungu feki ni malaika walioasi, na hata siku moja hawawezi kumzidi nguvu Mungu wa kweli, ambae ndie aliwaumba wakiwa malaika wazuri tu lakini wakaamua kuasi na wakafukuzwa toka mbinguni. Pia wanajihuisha kwa namna ambayo watu wanaita majini, ghosts, kupitia kwenye hirizi nk. Hawa ndio waliochukua nafasi katika miungu feki ya Egypt. Na mara nyingi miungu feki inawakilishwa kwa namna ya kinyago au sanamu ya namna fulani.
Kwa upande wa pili, maandishi ya kwanza kabisa toka Mungu wa kweli katika flow ya dini isiyo feki yaliandikwa kwenye jiwe na Musa yakiwa kama Amri Kumi miaka karibu 4000 iliyopita, pale Mlima Sinai Egypt wakati Musa akiongoza Israel kutoka Misri.
Hadi hapo tayari kulishakuwa na dini duniani, na miungu feki. Kwa mfano, Wa-Egypt walikuwa na miungu yao na ibada yao. Lakini ili kuonyesha u-fake wa Miungu ya Egypt Mungu wa kweli aliwapiga Wa-Egypt ili wawaachie Waisrael na Miungu ya Israel haikuwa na uwezo wa kuzuia yale mapigo. Mungu wa kweli alipogeuza fimbo ya Musa kuwa nyoka, miungu feki ya Egypt ilijaribu kugeuza fimbo ya mganga wa Egypt kuwa nyoka na nyoka wa Musa akammzeza nyoka wa mganga wa Egypt kuonyesha ukuu wa Mungu wa kweli wa Musa
Kumbuka kwamba miungu feki kimsingi ni nafasi inayochukuliwa aidha na shetani moja kwa moja au na malaika walioasi kwa kumuunga mkono shetani. Wapo hapa duniani. Yaani kwa mfano, wewe hapo kwako ukiamua uwe na mungu wako katika kibuyu fulani ulicho nacho, hao malakika walioasi watakinafsisha (kukipa unafsi) hicho kibuyu kiasi kwamba kuna mambo unaweza kukiomba na kikakufanyia. Hivyo hivyo kwa mti, sehemu ya tambiko nk. Kitu chochote unachoamua kukiabudu hawa malaika walioasi wanaki-animate na kinakuwa na unafsi fulani wa kuweza kuwa na communication na wewe. Lakini sasa kumbuka wanaofanya hivyo na kuwa miungu feki ni malaika walioasi, na hata siku moja hawawezi kumzidi nguvu Mungu wa kweli, ambae ndie aliwaumba wakiwa malaika wazuri tu lakini wakaamua kuasi na wakafukuzwa toka mbinguni. Pia wanajihuisha kwa namna ambayo watu wanaita majini, ghosts, kupitia kwenye hirizi nk. Hawa ndio waliochukua nafasi katika miungu feki ya Egypt. Na mara nyingi miungu feki inawakilishwa kwa namna ya kinyago au sanamu ya namna fulani.
Sasa wakati wa uwepo wa dini feki za Egypt kulikuwapo na dini nyingine katika mataifa mengine pia. Kwa mfano Hinduism, ambayo ilikuwapo tangu enzi za kina Nuhu ambao Biblia inawataja kama wafuasi wa Mungu wa kweli. Pia kulikuwa na Ubudha, ambao ulianza karibu miaka 1500 baada ya kuwapo kwa Uhindu.
Lakini jambo la msingi utambue kuwa Mungu wa kweli wa Musa hata siku moja hakutambua uwepo wa dini ya Budha au Hindu japo alitoa maagizo kwa Musa, Yesu nk hizi dini zikiwapo. Ni kama vile tu Yesu hakutambua uhalisi wa dini nyingine zilizokuwapo wakati wake.
Sasa ili kufuata mlolongo wa Mungu wa kweli na dini ya kweli, anza na pale mwanzo kabisa Mungu wa kweli akimwambia Musa aandike maandishi aliyompa Musa karibu miaka 6000 iliyopita, Musa alipoandika "Hapo Mwanzo Mungu aliziumba mbingu na dunia", kulingana na kitabu cha Biblia Mwanzo 1:1.
Sasa kuanzia hapo anza kumfuatilia huyu Mungu alietoa maagizo kwa Musa. Baadae alikuja kuwafanya Waisrael kama taifa lake maalum, lakini akawakataza katakata kuwa na ushirikiano na watu au dini nyingine yeyote ile. Akiwapa amri hii, kulikuwa na Ubudha na Uhindu. Hilo ni jambo la maana sana ku-note.
Sasa Israel kama taifa teule la Mungu, ikawa na mfumo wa ibada ambao tunauita Judaism, ambayo, kimsingi ndiyo ilisimamiwa na Mungu wa kweli na ilikuwa na mambo ya sabato, usile kitimoto, utahiri watoto, nk. Lakini Mungu wa kweli aliweka wazi kabisa kwamba kuna wakati Judaism ingebadilika na kuwa Ukristo baada ya Yesu kuja. Ilipofikia wakati wa kubadilika, wengi wa wafuasi wa Judaism wakakataa kubadilika kulingana na mafundisho ya Yesu, japo walisoma katika vitabu kwamba ile Judaism Mungu wa kweli aliitumia kama njia ya kuwaleta kwenye Ukristo. Wafuasi wa Judaism wakawa wakali sana kwa wale waliobadilika kuwa Wakristo na hata kuwaua. Paulo, akiwa Sauli wakati huo, naye alikuwa ana msimamo mkali wa kubaki na Judaism, akawa kinara wa kupinga ukristo hadi alipotokewa na Yesu na kupofushwa ndio akawa Mkristo. Hadi leo nchi ya Israel kama taifa inafuata dini ya Judaism na hivyo hawamtambui Yesu. Judaism bado wanamsubiri Masihi alieahidiwa na hawakubali kwamba Yesu ndie alikuja kama Masihi.
Sasa hili la Israel kama taifa teule la Mungu kumkataa Yesu lilimuudhi Mungu, kwa sababu walengwa wa kwanza wa dhabihu ya Yesu walikuwa Waisrael. Sasa Israel walipomkataa Yesu na kuchagua kumuua, Mungu wa kweli aliamua kuacha kuwatambua rasmi kama taifa lake teule. Akasema kuanzia sasa, mtu yeyote duniani ana nafasi sawa kuwa mtu wake, bila kujali ni Muisrael, Mwarabu, Mwafrika au Mhindi, ili mradi huyu mtu atambue sehemu ya Yesu kama dhabihu, jambo ambalo watu wangu niliowaona kama taifa langu teule wamekataa kulikubali. Akaenda mbali ya hapo. Akaamua kuwaadhibu Waisrael kwa kumkataa na hata kumuua Yesu. Aliwatumia Waroma kuwaadhibu Waisrael, baada ya kuhakikisha Waisrael wote waliomkubali na kumtambua Yesu wametoka nje ya Yerusalemu, kama walivyoagizwa na Yesu kabla hajauwawa, pale aliposema mkiona Waroma wameizunguka Jerusalem tokeni ndani yake mkimbilie milimani msirudi hata ndani kuchukua kitu. Wakristo wafuasi wa Yesu walitii hili. Wale Wajudaism na Mafarisayo walikaidi wakakumbwa na dhoruba ya Waroma. Cha moto walikiona!
IIlikuwa mwaka 70 Mungu alipowatumia askari Waroma kupiga Israel na kuisambaratisha yote, na kuharibu hekalu walilolitumia na kujivunia na Judaism yao. Waroma wakawaondoa Waisrael waliobaki na kuwapeleka Roma na kwingineko, na ukawa ndio mwisho wa Israel kama taifa, huo mwaka 70. Waisrael waliishia kutawanyika Ulaya na Marekani na sehemu yao ikaja kukaliwa na Wapalestina baada ya kubaki tupu baada ya Waisrael kusambaratishwa na Waroma. Wengine waliishia German, UK, USA nk, hadi mwaka 1948 ambapo baada ya kuuwawa sana na Hitler, mpango ulifanyika ili kuwapatia nchi yao. Kwanza iliamuliwa waje Uganda, koloni la Uingereza. Wakagoma, wakasema historia (Biblia) inasema nchi yetu ni pale wanapokaa Wapalestina kwa sasa. Wakaambiwa mliondoka pale toka mwaka 70 leo 1948 mnataka tukawaondoe Wapalestina kuwa ile ni nchi yenu? Hatimae iliamuliwa kwamba basi wakae pamoja, na yakawa ndio matokeo ya kuwa na Palestina na Israel ya sasa. Waisrael walikubali, Wapalestina walikataa. Ikaleta vita, na ndio mgogoro uliopo hadi leo.
Turudi kwenye Mungu wa kweli. Wakati aisrael wamemktaa Yesu, Mungu alihitimisha ujumbe wake kwa wanadamu kama namna ya kuwapa maagizo katika kitabu kinaitwa Biblia, kitabu cha mwisho kikiwa Ufunuo kikieleza nini kitafuata baada ya yesu kupaa mbinguni, na kikikamilishwa kuandikwa na Yohana mwaka 93, miaka karibu 60 tangu Yesu auwawe na kupaa mbinguni.
Tatizo ni kwamba baada ya kitabu cha Ufunuo, wakaja wanadamu wengine ambao wakadai nao ni wawakilishi au mitume wa Mungu wa kweli. Na wakaja na vitabu vyao au filosofia zao. Sasa ili kujua kama je, kweli hawa waliokuja baada ya kukamilika Ufunuo mwaka 93, ni wawakilishi wa Mungu wa kweli? Sasa hawa wawakilishi waliokuja baada ya Yesu imani kubwa walizonzisha zilikuwa zifuatazo
1. Uislamu, ukaanzishwa na Mohammed mwaka 610,miaka kama 577 baada ya Yesu kuuwawa
2. Usingasinga wa India ulianzishwa karibu miaka 900 baada ya Uislamu
Sasa hizi ndizo dini kubwa, na utaona kwamba wafuasi wake wote wanadai wote wanakubalika kwa Mungu wa kweli. Kwa mfano, Uislamu ulipoanza mika ya 610, mauaji na mpambano mkubwa ulifuatia kati ya Uislamu na Ukristo. Sasa haiwezekani kwamba kama wote walikuwa wanafuata Mungu wa kweli wangekuwa na mpambano huu.Pia utaona baada ya Uislamu kuanzishwa, kuna mambo ndani ya Uislamu yalipingana kabisa na Ukristo, na yakarudisha tena mambo yaliyokuwa seheu ya dini ya Judaism ambayo nayo ilipingana na Ukristo.
Nadhani nimekupa msingi wa kutosha kukufanya uanze kuchukua uamuzi