Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Kumbe ni tafsiri iliyo base kwenye dini.

Nilitaka utoe tafsiri ambayo ni universal sio religion perception.

Nimecheka sana kijana, shida yako husomi ninacho kiandika. Katika nilicho kiandika nimeweka maana ya imani ya ujumla na maana ya imani ya kifani. Labda huenda mamiati nilio utumia ni mgeni kwako na hukujua ya kwamba nimetoa maana ya ujumla. Ukiambiwa maana ya kilugha ya tamko fulani ujue hiyo ndio maana ya ujumla, na ukiambiwa maana ya kiistilahi ndio maana ya kifani.

Sasa, kwa sababu hukuliona hilo, rejea katika ile maana niliyo itoa huko juu kisha ujenge hoja, baada ya hapo tujadili maana nilizo zitoa ili tuone je ni za kweli au si za kweli kwa kuzingatia uhalisia. Hivi ndivyo watu wenye ufahamu hupaswa kujadili, yaani tunajadili kilichoandikwa sio mnakimbia hoja.

Lakini, imani ya kidini kwa maana ya kiistilahi ina nguvu zaidi juu ya hiki tunacho kijadili labda uwe umesahau msingi wa mada yako na hili litakuwa la ajabu sana. Lakini sio geni kwa Wakanamungu, sababu mnauwezo mdogo sana wa kufikiri na kung'amua mambo.
 
Hii ndio umeitoa kule kwenye kiarabu na wale wanazuoni wako??

Sijaelewa una maanisha nini ? Kwamba sio maana ya imani au ? Hoja yako hapo ipo wapi ? Au wewe ulitaka niitoe wapi ? Maana nimejibu swali kama ulivyo uliza.

Kwani ya kwenye Kiarabu imeandikwaje ?
 
Sasa unasema huipingi sayansi, ila at the same time mimi napo nukuu policy za Sayansi kuhusu kukosolewa unazipinga kwa madai ya kuwa naifanya Sayansi kama mtu.

Hivi huoni kama wewe ndio unajichanganya?
Nimeeleza kuwa sayansi hapingwi bali kinaachopingwa au kukosolewa ni tafiti za kisayansi ambazo hufanywa na watu.
Hata hiyo kauli ya sijui sayansi imesema....si sahihi.

Ajabu unasema napinga sayansi, yani mimi kukukosoa wewe na mtazamo wako kuhusu sayansi ndio unanuona napinga sayansi.
 
Bado tu mnachanganya maji na mafuta? kuthibitisha mambo ya imani kwa kutumia fact/Logic. Kama huamini usitake logic kutoka kwa waamini sababu hakuna logic katika imani. Logic unaipata kwenye sayansi.
 
Haya maneno ya kujua na kuamini yanawachanganya sana, kujua hakutenganishi ukweli na uongo.
Kujua kuna uhakika, ushahidi na uthibitisho na ukweli.

Kama huna uhakika, ushahidi wala uthibitisho basi hicho unacho kijua bado hakina ukweli.

Sawa utakuwa unajua na kudhani unajua, Kumbe hujui na hicho unacho dhani ni ukweli ni uongo.
 
Kujua kuna uhakika, ushahidi na uthibitisho na ukweli.

Kama huna uhakika, ushahidi wala uthibitisho basi hicho unacho kijua bado hakina ukweli.

Sawa utakuwa unajua na kudhani unajua, Kumbe hujui na hicho unacho dhani ni ukweli ni uongo.
Kujua hakuna uhusiano na ukweli wala uthibitisho, huwezi kusema anachokijua mtu ni uongo kisa tu hana uthibitisho.
 
Kujua hakuna uhusiano na ukweli wala uthibitisho, huwezi kusema anachokijua mtu ni uongo kisa tu hana uthibitisho.
Mtu akaja kukwambia anajua kwamba kuna Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao.

Utakubali tu akisemacho ni ukweli, Au utataka uthibitisho na ushahidi wa uwepo wa hao Dragons?
 
Kuna kujua kwa kudhani.

Na kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.
Sijui kwa nini mnapenda kulazimisha uthibitisho na neno kujua? Kwahiyo mtu ambaye hajafanya kipimo cha DNA kuthibitisha kama hao anaowajua kama wazazi wake ni wazazi kweli ama si kweli ndio unasema anajua kwa kudhani?
 
Mtu akaja kukwambia anajua kwamba kuna Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao.

Utakubali tu akisemacho ni ukweli, Au utataka uthibitisho na ushahidi wa uwepo wa hao Dragons?
Unachanganya vitu, mtu kusema yeye anajua ni jambo moja na mimi kukubali anachosema ni jambo lengine.
 
Sijui kwa nini mnapenda kulazimisha uthibitisho na neno kujua? Kwahiyo mtu ambaye hajafanya kipimo cha DNA kuthibitisha kama hao anaowajua kama wazazi wake ni wazazi kweli ama si kweli ndio unasema anajua kwa kudhani?
Ndio kwa kudhani.

Na ndio maana kuna wababa wengi wanalea watoto sio wao, wakidhani na kujua watoto ni wao. Kumbe sio wa kwao.

Hata wewe unaweza kulelewa na wazazi wa kambo ukadanganywa ni wazazi wako na wewe ukadhani na kujua kweli ni wazazi wako. Kumbe sio wa wazazi wako.

Kwa vile huna uthibitisho wa kwamba hao ni wazazi wako.
 
Safi kabisa, ukisoma historia ya Wanafalsafa wakale wa magharibi walau kidogo walikuwa wana maswali sahihi ila walikosa ala za kuwafikisha katika majibu sahihi. Kutofautiana juu ya kitu kimoja kwa majibu mengi na wewe ukaifanya kuwa ni hoja, kunadhihirisha wewe ni mchachefu sana wa elimu juu ya dini hizo, huenda hujazisoma ukajua machimbo yake na kwanini imekuwa hivi.

Ni kweli kuna miungu wengi, ila hata hao wenye kuabudu miungu yao wanajua ya kuwa kuna Mungu Mkuu aliyeumba, rejea historia ya Makafiri wa Makka na wasio kuwa hao.

Jaribuni kusoma vitu ili kidogo muwe mnajenga hoja zenhye maana na zenye nguvu.

Unapo ongelea tamko Mungu. katika Kamusi zote za lugha zinamtambua ya kuwa ni yule Mungu mkuu, muumba wa mbingu na ardhi na apasae kuabudiwa peke yake. Sasa unaposikia kuna dini wanamuabudu Ng'ombe na kumfanya Mungu, kwa akili makini tu inaonyesha wazi Ng'ombe hawzi kuwa mungu zaidi ya ujinga wa watu.

Ndio maana nikasema imani hiyo siyo sahihi, sababu ina chimbuko lake. Kijana kwa kukusaidia tu, unapotaka ujue uhakika wa jambo fulani hasa dini, kwanza tunaangalia historia husika za dini hiyo, kwako wewe na kwa jinsi ulivyo nina uhakika hujawahi kusoma historia za hizo dini na ukajua machimbuko na huu ni udhaifu mkubwa sana katika utafiti.
Mungu mkuu ni utambulisho wa kila dini katika kuelezea sifa za Mungu wanaye muabudu.

Hata zile dini za kale ambazo ni kongwe kuliko yako kama Sumerian zilikuwa zina amini Mungu zaidi ya mmoja, kwenye hiyo miungu zilikuwa na Mungu mkuu aliyekuwa anaitwa Enki ambaye ni mhusika na maswala hayo ya uumbaji.

Kwa hiyo sio kweli kuwa dini zenye kuabudu Mungu zaidi ya mmoja zinaamini nje ya imani yao kuna Mungu muumba wa ulimwengu kwasababu tumeona hata wao pia katika orodha ya Miungu wao wanaye huyo Mungu ambaye ni muumba.

Sio kweli kuwa tamko Mungu ni tamko linalomaanisha ni Mungu pekee anayepaswa kuabudiwa.

Hii itabaki kuwa ni maoni yenu binafsi kulingana na lenye mipaka isiyovuka imani yenu hivyo haiwezi kuwa ni tamko lenye kujumuisha imani zingine na ndio maana tumeweza kuona imani zingine zikiwa na Mungu zaidi ya mmoja na wote wakiabudiwa.

Kusema imani ya wengine sio sahihi, hauwezi kuwa sahihi. Kwasababu hauwezi kutumia sheria za dini yako kukosoa dini za wengine.

Hata hizo dini zinaweza kukuambia kuwa dini yako ni ya uongo kwasababu wanazoziona zinahitilafiana na kanuni za dini yao.
 
Ndio maana nikakuuliza nijue ni kipi ulichotumia kujua Miungu feki ambacho waumini wa hiyo Miungu wameshindwa kukitumia kukijua u fake wa Mungu wao ili nao waachane na Mungu wao feki waungane kuabudu Mungu wako ambaye ni original?
Tatizo lako sio issue ya mungu feki, bali ni dini feki. Lakini naelewa pia filosofia ya Mungu feki inatoka wapi. Tuanze na hilo. La msingi ujue mungu feki na dini feki vipo karibu sana, lakini unaweza kuwa na dini feki ambayo iinadai inakubalika na Mungu wa kweli. Hilo ni jambo jingine.

Mtu anaweza kusema anamwabudu Mungu wa kweli alieumba dunia na mbingu, ikawa ni sawa, lakini tatizo ikawa anafanya ibada feki. Unapaswa kutambua hilo

Kumbuka kwamba miungu feki kimsingi ni nafasi inayochukuliwa aidha na shetani moja kwa moja au na malaika walioasi kwa kumuunga mkono shetani. Wapo hapa duniani. Yaani kwa mfano, wewe hapo kwako ukiamua uwe na mungu wako katika kibuyu fulani ulicho nacho, hao malaika walioasi watakinafsisha (kukipa unafsi) hicho kibuyu kiasi kwamba kuna mambo unaweza kukiomba na kikakufanyia. Hivyo hivyo kwa mti, sehemu ya tambiko nk. Kitu chochote unachoamua kikiabudu hawa malaika walioasi wanaki-animate na kinakuwa na unafsi fulani wa kuweza kuwa na communication na wewe. Lakini sasa kumbuka wanaofanya hivyo na kuwa miungu feki ni malaika walioasi, na hata siku moja hawawezi kumzidi nguvu Mungu wa kweli, ambae ndie aliwaumba wakiwa malaika wazuri tu lakini wakaamua kuasi na wakafukuzwa toka mbinguni. Pia wanajihuisha kwa namna ambayo watu wanaita majini, ghosts, kupitia kwenye hirizi nk. Hawa ndio waliochukua nafasi katika miungu feki ya Egypt. Na mara nyingi miungu feki inawakilishwa kwa namna ya kinyago au sanamu ya namna fulani.

Kwa upande wa pili, maandishi ya kwanza kabisa toka Mungu wa kweli katika flow ya dini isiyo feki yaliandikwa kwenye jiwe na Musa yakiwa kama Amri Kumi miaka karibu 4000 iliyopita, pale Mlima Sinai Egypt wakati Musa akiongoza Israel kutoka Misri.

Hadi hapo tayari kulishakuwa na dini duniani, na miungu feki. Kwa mfano, Wa-Egypt walikuwa na miungu yao na ibada yao. Lakini ili kuonyesha u-fake wa Miungu ya Egypt Mungu wa kweli aliwapiga Wa-Egypt ili wawaachie Waisrael na Miungu ya Israel haikuwa na uwezo wa kuzuia yale mapigo. Mungu wa kweli alipogeuza fimbo ya Musa kuwa nyoka, miungu feki ya Egypt ilijaribu kugeuza fimbo ya mganga wa Egypt kuwa nyoka na nyoka wa Musa akammzeza nyoka wa mganga wa Egypt kuonyesha ukuu wa Mungu wa kweli wa Musa

Kumbuka kwamba miungu feki kimsingi ni nafasi inayochukuliwa aidha na shetani moja kwa moja au na malaika walioasi kwa kumuunga mkono shetani. Wapo hapa duniani. Yaani kwa mfano, wewe hapo kwako ukiamua uwe na mungu wako katika kibuyu fulani ulicho nacho, hao malakika walioasi watakinafsisha (kukipa unafsi) hicho kibuyu kiasi kwamba kuna mambo unaweza kukiomba na kikakufanyia. Hivyo hivyo kwa mti, sehemu ya tambiko nk. Kitu chochote unachoamua kukiabudu hawa malaika walioasi wanaki-animate na kinakuwa na unafsi fulani wa kuweza kuwa na communication na wewe. Lakini sasa kumbuka wanaofanya hivyo na kuwa miungu feki ni malaika walioasi, na hata siku moja hawawezi kumzidi nguvu Mungu wa kweli, ambae ndie aliwaumba wakiwa malaika wazuri tu lakini wakaamua kuasi na wakafukuzwa toka mbinguni. Pia wanajihuisha kwa namna ambayo watu wanaita majini, ghosts, kupitia kwenye hirizi nk. Hawa ndio waliochukua nafasi katika miungu feki ya Egypt. Na mara nyingi miungu feki inawakilishwa kwa namna ya kinyago au sanamu ya namna fulani.

Sasa wakati wa uwepo wa dini feki za Egypt kulikuwapo na dini nyingine katika mataifa mengine pia. Kwa mfano Hinduism, ambayo ilikuwapo tangu enzi za kina Nuhu ambao Biblia inawataja kama wafuasi wa Mungu wa kweli. Pia kulikuwa na Ubudha, ambao ulianza karibu miaka 1500 baada ya kuwapo kwa Uhindu.

Lakini jambo la msingi utambue kuwa Mungu wa kweli wa Musa hata siku moja hakutambua uwepo wa dini ya Budha au Hindu japo alitoa maagizo kwa Musa, Yesu nk hizi dini zikiwapo. Ni kama vile tu Yesu hakutambua uhalisi wa dini nyingine zilizokuwapo wakati wake.

Sasa ili kufuata mlolongo wa Mungu wa kweli na dini ya kweli, anza na pale mwanzo kabisa Mungu wa kweli akimwambia Musa aandike maandishi aliyompa Musa karibu miaka 6000 iliyopita, Musa alipoandika "Hapo Mwanzo Mungu aliziumba mbingu na dunia", kulingana na kitabu cha Biblia Mwanzo 1:1.

Sasa kuanzia hapo anza kumfuatilia huyu Mungu alietoa maagizo kwa Musa. Baadae alikuja kuwafanya Waisrael kama taifa lake maalum, lakini akawakataza katakata kuwa na ushirikiano na watu au dini nyingine yeyote ile. Akiwapa amri hii, kulikuwa na Ubudha na Uhindu. Hilo ni jambo la maana sana ku-note.

Sasa Israel kama taifa teule la Mungu, ikawa na mfumo wa ibada ambao tunauita Judaism, ambayo, kimsingi ndiyo ilisimamiwa na Mungu wa kweli na ilikuwa na mambo ya sabato, usile kitimoto, utahiri watoto, nk. Lakini Mungu wa kweli aliweka wazi kabisa kwamba kuna wakati Judaism ingebadilika na kuwa Ukristo baada ya Yesu kuja. Ilipofikia wakati wa kubadilika, wengi wa wafuasi wa Judaism wakakataa kubadilika kulingana na mafundisho ya Yesu, japo walisoma katika vitabu kwamba ile Judaism Mungu wa kweli aliitumia kama njia ya kuwaleta kwenye Ukristo. Wafuasi wa Judaism wakawa wakali sana kwa wale waliobadilika kuwa Wakristo na hata kuwaua. Paulo, akiwa Sauli wakati huo, naye alikuwa ana msimamo mkali wa kubaki na Judaism, akawa kinara wa kupinga ukristo hadi alipotokewa na Yesu na kupofushwa ndio akawa Mkristo. Hadi leo nchi ya Israel kama taifa inafuata dini ya Judaism na hivyo hawamtambui Yesu. Judaism bado wanamsubiri Masihi alieahidiwa na hawakubali kwamba Yesu ndie alikuja kama Masihi.

Sasa hili la Israel kama taifa teule la Mungu kumkataa Yesu lilimuudhi Mungu, kwa sababu walengwa wa kwanza wa dhabihu ya Yesu walikuwa Waisrael. Sasa Israel walipomkataa Yesu na kuchagua kumuua, Mungu wa kweli aliamua kuacha kuwatambua rasmi kama taifa lake teule. Akasema kuanzia sasa, mtu yeyote duniani ana nafasi sawa kuwa mtu wake, bila kujali ni Muisrael, Mwarabu, Mwafrika au Mhindi, ili mradi huyu mtu atambue sehemu ya Yesu kama dhabihu, jambo ambalo watu wangu niliowaona kama taifa langu teule wamekataa kulikubali. Akaenda mbali ya hapo. Akaamua kuwaadhibu Waisrael kwa kumkataa na hata kumuua Yesu. Aliwatumia Waroma kuwaadhibu Waisrael, baada ya kuhakikisha Waisrael wote waliomkubali na kumtambua Yesu wametoka nje ya Yerusalemu, kama walivyoagizwa na Yesu kabla hajauwawa, pale aliposema mkiona Waroma wameizunguka Jerusalem tokeni ndani yake mkimbilie milimani msirudi hata ndani kuchukua kitu. Wakristo wafuasi wa Yesu walitii hili. Wale Wajudaism na Mafarisayo walikaidi wakakumbwa na dhoruba ya Waroma. Cha moto walikiona!

IIlikuwa mwaka 70 Mungu alipowatumia askari Waroma kupiga Israel na kuisambaratisha yote, na kuharibu hekalu walilolitumia na kujivunia na Judaism yao. Waroma wakawaondoa Waisrael waliobaki na kuwapeleka Roma na kwingineko, na ukawa ndio mwisho wa Israel kama taifa, huo mwaka 70. Waisrael waliishia kutawanyika Ulaya na Marekani na sehemu yao ikaja kukaliwa na Wapalestina baada ya kubaki tupu baada ya Waisrael kusambaratishwa na Waroma. Wengine waliishia German, UK, USA nk, hadi mwaka 1948 ambapo baada ya kuuwawa sana na Hitler, mpango ulifanyika ili kuwapatia nchi yao. Kwanza iliamuliwa waje Uganda, koloni la Uingereza. Wakagoma, wakasema historia (Biblia) inasema nchi yetu ni pale wanapokaa Wapalestina kwa sasa. Wakaambiwa mliondoka pale toka mwaka 70 leo 1948 mnataka tukawaondoe Wapalestina kuwa ile ni nchi yenu? Hatimae iliamuliwa kwamba basi wakae pamoja, na yakawa ndio matokeo ya kuwa na Palestina na Israel ya sasa. Waisrael walikubali, Wapalestina walikataa. Ikaleta vita, na ndio mgogoro uliopo hadi leo.

Turudi kwenye Mungu wa kweli. Wakati aisrael wamemktaa Yesu, Mungu alihitimisha ujumbe wake kwa wanadamu kama namna ya kuwapa maagizo katika kitabu kinaitwa Biblia, kitabu cha mwisho kikiwa Ufunuo kikieleza nini kitafuata baada ya yesu kupaa mbinguni, na kikikamilishwa kuandikwa na Yohana mwaka 93, miaka karibu 60 tangu Yesu auwawe na kupaa mbinguni.

Tatizo ni kwamba baada ya kitabu cha Ufunuo, wakaja wanadamu wengine ambao wakadai nao ni wawakilishi au mitume wa Mungu wa kweli. Na wakaja na vitabu vyao au filosofia zao. Sasa ili kujua kama je, kweli hawa waliokuja baada ya kukamilika Ufunuo mwaka 93, ni wawakilishi wa Mungu wa kweli? Sasa hawa wawakilishi waliokuja baada ya Yesu imani kubwa walizonzisha zilikuwa zifuatazo

1. Uislamu, ukaanzishwa na Mohammed mwaka 610,miaka kama 577 baada ya Yesu kuuwawa
2. Usingasinga wa India ulianzishwa karibu miaka 900 baada ya Uislamu

Sasa hizi ndizo dini kubwa, na utaona kwamba wafuasi wake wote wanadai wote wanakubalika kwa Mungu wa kweli. Kwa mfano, Uislamu ulipoanza mika ya 610, mauaji na mpambano mkubwa ulifuatia kati ya Uislamu na Ukristo. Sasa haiwezekani kwamba kama wote walikuwa wanafuata Mungu wa kweli wangekuwa na mpambano huu.Pia utaona baada ya Uislamu kuanzishwa, kuna mambo ndani ya Uislamu yalipingana kabisa na Ukristo, na yakarudisha tena mambo yaliyokuwa seheu ya dini ya Judaism ambayo nayo ilipingana na Ukristo.

Nadhani nimekupa msingi wa kutosha kukufanya uanze kuchukua uamuzi
 
Nimecheka sana kijana, shida yako husomi ninacho kiandika. Katika nilicho kiandika nimeweka maana ya imani ya ujumla na maana ya imani ya kifani. Labda huenda mamiati nilio utumia ni mgeni kwako na hukujua ya kwamba nimetoa maana ya ujumla. Ukiambiwa maana ya kilugha ya tamko fulani ujue hiyo ndio maana ya ujumla, na ukiambiwa maana ya kiistilahi ndio maana ya kifani.

Sasa, kwa sababu hukuliona hilo, rejea katika ile maana niliyo itoa huko juu kisha ujenge hoja, baada ya hapo tujadili maana nilizo zitoa ili tuone je ni za kweli au si za kweli kwa kuzingatia uhalisia. Hivi ndivyo watu wenye ufahamu hupaswa kujadili, yaani tunajadili kilichoandikwa sio mnakimbia hoja.

Lakini, imani ya kidini kwa maana ya kiistilahi ina nguvu zaidi juu ya hiki tunacho kijadili labda uwe umesahau msingi wa mada yako na hili litakuwa la ajabu sana. Lakini sio geni kwa Wakanamungu, sababu mnauwezo mdogo sana wa kufikiri na kung'amua mambo.
Kufanya maelezo marefu yawe mafupi

Nipe source ya hiyo tafsiri kwanza nisome nihakikishe kabla hatujafika mbali.

Nataka hiyo ambayo haijatolewa na wazee wako wa zuoni.
 
Sijaelewa una maanisha nini ? Kwamba sio maana ya imani au ? Hoja yako hapo ipo wapi ? Au wewe ulitaka niitoe wapi ? Maana nimejibu swali kama ulivyo uliza.

Kwani ya kwenye Kiarabu imeandikwaje ?
Ulisema kuna ya wanazuoni na kiarabu, sasa hiyo tafsiri uliyoweka inatoka kwenye chanzo kipi kati ya hivyo viwili?

Au ni mchanganyiko?
 
Ndio kwa kudhani.

Na ndio maana kuna wababa wengi wanalea watoto sio wao, wakidhani na kujua watoto ni wao. Kumbe sio wa kwao.

Hata wewe unaweza kulelewa na wazazi wa kambo ukadanganywa ni wazazi wako na wewe ukadhani na kujua kweli ni wazazi wako. Kumbe sio wa wazazi wako.

Kwa vile huna uthibitisho wa kwamba hao ni wazazi wako.
Ok haya hebu nipe tofauti ya kuamini na kujua kwa kudhani?
 
Nimeeleza kuwa sayansi hapingwi bali kinaachopingwa au kukosolewa ni tafiti za kisayansi ambazo hufanywa na watu.
Hata hiyo kauli ya sijui sayansi imesema....si sahihi.

Ajabu unasema napinga sayansi, yani mimi kukukosoa wewe na mtazamo wako kuhusu sayansi ndio unanuona napinga sayansi.
Ukipinga tafiti ndio umeipinga Sayansi hivyo.

Halafu kuna shida ya uelewa hapa naiona.

Hivi ukisikia kauli kuwa Bunge linajadili hoja ni ipi tafsiri unayoipata? Kwamba ni jengo linaloitwa Bunge ndio linalofanya mjadala?

Au ni wabunge ndio wanaofanya mjadala?

Mara nyingi tunatumia msemo "Sayansi imesema hivi" au "Sayansi inaonyesha kwamba" kama uwakilishi tu kumaanisha utafiti na data zilizopatikana kupitia mbinu za kisayansi zinazoonesha ushahidi au matokeo fulani.

Ingawa sayansi yenyewe sio mtu au kiumbe cha kutambua, tunatumia msemo huo tu kwa urahisi na niijua haiwezi kuleta shida ya kutoeleweka kwasababu najadiliana na mtu ambaye hivi vitu kwake ni rahisi.

Kwasababu hata makanisani ni kawaida kusikia Pastor katika mahubiri yake akiongea maneno haya "Biblia inasema" japo kuwa wote tunajua Biblia sio mtu mpaka iseme ila kwenye ishu yako maana yake hiyo ni mada nyingine ambayo utaipinga.
 
Ok haya hebu nipe tofauti ya kuamini na kujua kwa kudhani?
Kuamini ni kutokuwa na uhakika, ushahidi wala uthibitisho wa jambo au kitu fulani. Ambapo jambo au kitu hicho kinaweza kiwepo ama kisiwepo.

Kujua kwa kudhani, Ni kutokuwa na taarifa sahihi zenye uhakika, ushahidi, ukweli na uthibitisho kuhusu jambo au kitu fulani ambacho tayari kipo in reality.
 
Tatizo lako sio issue ya mungu feki, bali ni dini feki. Lakini naelewa pia filosofia ya Mungu feki inatoka wapi. Tuanze na hilo. La msingi ujue mungu feki na dini feki vipo karibu sana, lakini unaweza kuwa na dini feki ambayo iinadai inakubalika na Mungu wa kweli. Hilo ni jambo jingine.
Hapa ndio sehemu shida ilipo.

Umetumia SI Unit gani kupima ufeki na uhalali wa dini?

Kwasababu nacho kiona hapa ni ishu ya mwamba ngoma ambaye wote tunajua lazima aivutie kwake.

Nini kinachokufanya uone kauli unayoitoa wewe dhidi ya dini zingine haiwezi kutolewa na mtu wa dini hizo kwa kuitaja dini yako kuwa ni feki pia??

So itakuwa ni swala la nani kamuwahi mwenzake. Ikiwa ningemuuliza hili swali muumini anayehusika na hizo dini ulizoziita feki pengine angetoa majibu haya haya kuilenga dini yako.

Tambua kuwa swala la ufeki wa dini zingine haliwezi kuamuliwa kupitia sheria au mitizamo ya dini yako.

Kila dini imejiwekea miiko ambayo itaitofautisha na dini zingine, na kwamba chochote kinachofanyika nje na hiyo miiko kitahesabika kuwa si chema.

So wewe kusema dini fulani ni feki unaweza kuwa sahihi machoni mwa waumini wenzako mnao share common interests kwenye dini yako.

Lakini kauli hiyo ikawa na mipaka katika macho na masikio ya watu wa dini hiyo unayoitaka kuwa ni feki.

Kwasababu nao wana miongozo yao inayowatambulisha kuwa ni dini original na kuwataka waachane na dini kama yako kwasababu ni feki.
 
Back
Top Bottom