The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Imekaa poa sana
Ikiwa mmoja anataka kubadilika ila mwingine ni mgumu inakuwaje mfano
Imepitia kwenye mkasa wa rafikiyangu anampenda sana mumewe ila sio mtu wa kujali Wala kumsaidia japo mwanamke anatumiza majukumu yake pia Kuna Ile akimkosea anadai atamuacha kama mwenzio
Mtu kma huyu unaishi nae vipi?
Vitu vingi sana vinapelekea watu kubadilika, na hasa upendo ukipoa, hapo ndio uvumilivu huisha, unaanza kuyaona mapungufu ya mwenza wako.
Kikubwa ikiwa mmoja atabahatika kuona kwamba vitu haviko sawa akaamua kujitoa muhanga kunusuru ndoa/ mahusiano, inaweza kusaidia badala ya wote kuingia kwenye mashindano ya kukomoana au kuchoka kuendelea kuwa mwema Kwa kuona hakuna mabadiliko upande wa pili.
Kuna vitu kama vingezungumzwa, unawezagundua kumbe ni mtizamo tu tofauti wa jambo ambalo halipo kama mnavyolichukulia ila mmeamua kunyamaziana au kuingiza chuki ikafanya ugomvi uzidi kumlea na kuleta madhara zaidi.
Narudia tena, watu wanabadilika kutokana na sababu tofauti tofauti na mazingira wanayokutana nayo, kikubwa hakikisha mna mazingira Rafiki ya kuweza kuongea na kuzungumza mambo yenu. Na usimuwazie hasi mwenzio wako, wakati huo huo uamue kuwa sehemu ya suluhu ya kunusuru mahusiano.
Ukiamua kumchukulia mtu ni mmvaya au ana kasoro nyingi, hautaona jema hata Moja Kwa huyo mtu.
Mwambie huyo Rafiki Yako shida inaweza kuwa sio yeye ila ni kipindi anachopitia mwenza wake, ajaribu Kwa upole kuonyesha kwamba anaona mabadiliko kwenye mahusiano Yao na Yuko tayari kujadili kuepusha intimacy kupotea.
Mwisho kabisa. Natamani wanaume tungekua nasisi tuna vikao vyetu kukumbushana namna Bora ya kuwa wapenzi Kwa wake zetu. Tunajisahau mno, ilimradi unahudumia familia na kufanya mambo ya msingi, unaona inatosha lakini kumbe wake zetu Wana mahitaji ya kihisia na kupendwa kuliko hata vitu vikubwa tunavyofanya.
Unakuta haukumbuki Mara ya mwisho tulimnunulia lini zawadi au kumdanyia kitu maalum Mke wako kuonyesha upendo wako kwake, na hatuoni ni tatizo. Basi hata mlitoka wote lini mkaenda mahali pamoja mkawa na muda wakufueahia, hakuna. Tokea enzi za uchumba na baada ya siku za awali za ndoa mambo mengi yamepoa na sie waume hatuoni ni tatizo.
Nimejikuta naandika mambo mengi hata sijui kama nimegusa Kwa ufasaha swali ulilouliza.
Kwa kumalizia, hakuna user guide au instraction manual ya mahusiano, bado haijatoka.