Je, Mapambano ya Wanaharakati na Diamond yana faida kwa nchi?

Je, Mapambano ya Wanaharakati na Diamond yana faida kwa nchi?

Kachagua side au kachagua pesa? CCM walimlipa 100m ili aburudishe na kuburudisha ni kazi yake huyo diamond hata kadi ya CCM Hana na Wala sio mwanachama wa CCM na pia si mwanaharakati wewe ungekuwa ndio yeye hiyo million 100 ungekataa? Na onyesha wapi aliwahi kusapoti mauwaji badala ya Chadema waliumia Diamond kuwafanyia burudani CCM kwenye mikutano ya siasa kwanini na wao wasimlipe waone kama hatawafanyia kuliko kuendesha kampeni za kipuuzi
Hujaelewa au huelewi kabisa...

Kumbuka ulivyofundishwa shuleni kwenye somo la FASIHI kuwa, MSANII yeyote kama alivyo KIONGOZI yeyote ni KIOO CHA JAMII...

Kioo hakioneshi kisichoonekana. Jamii inatazama kile msanii anachofanya hadharani na kuonekana na kila mtu. Jamii ndiyo inayotoa hukumu ya kile msanii au kiongozi afanyacho..

Hayo ya kupewa milioni 100 unayajua wewe na yamefanyika sirini huko. Jamii haijishughulishi nayo hayo. Tunataka kumhukumu kwa kile anachokisambaza ktk jamii kupitia usanii wake. Kizuri au kibaya. Hapo kila mtu atajaji kivyake...

By the way, siyo kila sehemu/mahali palipo na pesa utakwenda kuchukua pesa hizo hata kama itabidi "uvuje jacho" kuzipata eti tu kwa sababu untafuta pesa...!

Alichofanya Diamond Platnumz na kujipatia hizo usemazo milioni 100 huko sirini ni ujambazi tu dhidi ya utu na haki za raia kwa kutumiwa na utawala katili wa CCM kwa jina la "kutoa burudani...."

Hapa ndipo lilipo tatizo ndugu. Fungua macho yako ya ndani uone. Acha kutazama kwa juu juu tu bila kutafakari...

The guy doesn't deserve any international recognition under this circumstances and we are going to make sure that is happening...!!
 
Ila hii chadema inawachezesha KRONO sana

Wapi kuna neno chadema kwenye comment yangu?
Yule ni mfanyabiashara kaenda pale kufanya burudani baada ya kulipwa sio kufanya siasa ungeelewa Hili lisingekusumbua na kuna wengine wameenda pale kufuata burudani sio hotuba za wanasiasa ndio maana baada ya diamond kutumbuiza wanasepa shida ni nyinyi mnaoteseka
 
E3Nf0AjWYAUhGAL.jpg
 
Yule ni mfanyabiashara kaenda pale kufanya burudani baada ya kulipwa sio kufanya siasa ungeelewa Hili lisingekusumbua na kuna wengine wameenda pale kufuata burudani sio hotuba za wanasiasa ndio maana baada ya diamond kutumbuiza wanasepa shida ni nyinyi mnaoteseka

Kajaribu kuingia mikumi kuvuna pembe za ndovu upige pesa uone jamii itakutazamaje. Sibiashara!

Tunaongelea utu na haki zake

Pesa zinazidi utu? Pesa zinazidi haki za watu?
 
Kwa mliokuwa hamjui, ogopa sana mtu/watu wenye uwezo wa kuandika. Ukiandikwa majambo yako yote kwa namna inavyostahili, utapata au kukosa ukitakacho chote. Mwambie Diamond Platnumz apoe, akae, aombe radhi kwa umma na ajirekebishe. Akitunisha mabega anaweza kuishia hapa kwa sababu biashara yake inategemea sana public relations.
 
Back
Top Bottom