Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Mkuu ni wapi ulisikia watoto wa adammu walizaa na dada zao?. Adamu alipata watoto watatu tu wote wa kiume inamaanisha kulikuwa na jamii nyingine tofauti na mwanzo wa uzao wa adamu.
Mkuu Hilo nalo itabidi liangaliwe
 
Just chukulia wewe ndo ungekuwa huyo mtoto halafu ukaambiwa hiyo ni sheria ya Mola,je kweli utampenda huyo Mola?
Mkuu unajua wanaokubali Sheria za Mungu ni Wale wanao mjua Mungu

Kwa mfano Kwa mafundisho ya Uislamu pale Ibrahim alipomwambia mwanae Ismail kuwa nimeota ndoto Nataka nikuchinje na ndoto za Manabii ni maono

Ismail kwakuwa anamjua Mola wake akasema "Baba maadam Hilo ni agizo la Mungu basi hakuna tatizo"

Ninachotaka kusema hapa amjuaye Mungu ataelewa tu
 
Na lingine ni kumuozesha kwenye ndoa, Baba Hana haki ya kumuozesha binti yake WA nje ya ndoa Kwa mumewe kwani ndoa hiyo ni batili na haifai kabisa.
Hii hapa imekaaje? Sasa hapo huyo mtoto hatoolewa Ama ?
 
Mmekaa kikandamizi sana,ona lawama zote mnamsukumizia mwanamke…Hata katika mahusiano ya mapenzi kawaida nani huwa initiator kama sio mwanaume? Sasa mwanamke anakujaje hapo?ok sawa na je waliobakwa? Wao ndo wamesababisha?
Tembea kila kona nchi hii nani anae jiuza kila kona wako uchi
 
Mkuu Hilo nalo itabidi liangaliwe
Tuachane na kizazi cha kwanza cha adamu tuje kwa adamu wa tatu ambaye ni Ibrahim aliye tuletea imani mbili ya Isaka na Ismail, Iweje imani ya Ismail umbague na kumkandamiza mtoto wa nje ya ndoa kiasi hicho ilihali muasisi wake alizaliwa nje ya ndoa?. Kwanini isingetoa room ya kurekebisha na kupewa haki kama watoto waliozaliwa ndani ya ndoa.
 
Na lingine ni kumuozesha kwenye ndoa, Baba Hana haki ya kumuozesha binti yake WA nje ya ndoa Kwa mumewe kwani ndoa hiyo ni batili na haifai kabisa.
Hii imekaaje?
Sasa kama ni wazazi wake wa kiume na hai wazazi ndio hawatambuliki ina maana huyo mtoto hatoolewa?
 
Unyanyasaji huo….Nyie ndo chanzo cha watoto wa mitaani
Chanzo cha watoto wa mitaani ni uzinzi ambao nyinyi hapa mpo mna utetea.
Dawa ya kuhepusha watoto wa namna hiyo ni kutulia na wake zetu tuache uzinzi na kama huna mke oa na sio kuchezea chezea watoto wa watu hovyo na kuwapa mimba kwa kigezo cha kuwa utalea mtoto.

Hakika ni ukatiri mkubwa kumpa mimba binti wa wawatu wakati huna mipango ya kumuoa hata kama utatunza huyo mtoto.
 
Tatizo mtazamo wako hauwezi kubadilisha ukweli.
Kuna watu hawa kubaliani na utawala wa Samia lakini hilo haliondoi ukweli kuwa ndo kiongozi wa nchi hii.
Kitu chochote kinacho patikana nje ya utaratibu ulio wekwa na mungu aliye kuumba ni haramu.
Awe haramu kwa Mungu, lakini kwangu ni mtoto wangu halali. Na atapata haki kama wapatavyo watoto wangu wengine.
 
Inafikrisha. Kwaiyo wanawake hawatakuwa na adhabu ya uzinzi kwa muumba ? Maana ya kwao kameisha imaliza au watakuwa nayo nyingine tena ?
Mtoto kwa mwanamke sio hadhabu bali ni zawadi kwa sababu huyo mtoto akikuwa mama ana haki zote za kula matunda ya huyo mtoto ,wakati ww baba hutakuwa na haki ya kudai chochote kutoka kwa huyo mtoto hata kama atapata hela kama billget.

Mfano baba yake na Diamond alikuwa ana lalamika eti mtoto hamjali ila kidini domo yuko sawa huyo baba yake hana haki ya kudai chochote kutoka kwa domo lakini mama yake ana haki ya kula matunda ya mafanikio ya mwanae.
 
Tatizo mtazamo wako hauwezi kubadilisha ukweli.
Kuna watu hawa kubaliani na utawala wa Samia lakini hilo haliondoi ukweli kuwa ndo kiongozi wa nchi hii.
Kitu chochote kinacho patikana nje ya utaratibu ulio wekwa na mungu aliye kuumba ni haramu.
Ni vile sijazaa nje ya ndoa ila ingetokea ningempa jina langu mara mbili mbili. Yaani Tsh TSH TSH Na huyo mungu unayemuongelea hapa angemtambua.
 
Awe haramu kwa Mungu, lakini kwangu ni mtoto wangu halali. Na atapata haki kama wapatavyo watoto wangu wengine.
Na ndio maana unashauliwa kama ni kumpa huyo mtoto mali mpe kabla hujafa.
 
Sizani kama umenijibu swali langu nililouliza kulingana na nilichokuwa nimequote
 
Yaani dini zilizoletwa na majahazi zinampangia binadam jina la kumpa mwanae
 
Nikisahihishe kidogo, ni kweli ndoa ya msingi ya dini inapendelewa zaidi ila katika uislamu ndoa zilizofungwa kwa imani nyengine zinatambuliwa pia, yani mtu akifunga ndoa kanisani huko ama uhinduni huko hiyo ndoa inatambulika

Ndio maana wanaondoa wa imani tofauti wakiingia uislamu hawana haja ya kufunga ndoa upya
 
Chanzo cha watoto wa mitaani ni janja janja mingi za kutaka kumtumia binti na kumkimbia, Woga na udhaifu wa kushindwa kubeba majukumu kama mwanaume.

SIMAMA TETEA DAMU YAKO HATA MBELE YA MUNGU KAMA ANA HASIRA SANA AKUUE UKITETEA ZAWADI YA MAISHA ALIYOILETA DUNIANI KUPITIA WEWE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…