Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Hizi dini bwana.
Ommy dimpos kawa tajiri baba na ndugu wanajipendekeza kumjua mtoto wao mlikuwa wapi na dini zenu.

Domo leo ni tajiri kila ndugu na masheik mnajazana kwake mlikuwa wapi pindi maskini.
Na hapo ndio ujue haijalishi ulizaliwa ndani ya ndoa au nje Mungu anaweza kumjalia yeyote kati yao.

Na hapo ndio ujue pia Mungu hajasema hicho kilicholetwa na mleta mada,ni mambo yaliyopangwa na wana wa adamu tu kwa kuwabagua wengine ambao pia ni viumbe kwa maslahi wanayoyajua wenyewe
 
Usizae nje ya ndoa
Ndo tunafundishwa ivo kua ni vibaya
Kuzaa hovyo kunapoteza uwezo wa mzazi kutoa huduma, hii ndo sababu yenye maana ya katazo la usizae nje ya ndoa, nyingine zote ni ubatili.
 
Hivi wakati Mungu ananiumba alinijua kuwa nitakuwa mzinzi?
 
Watu wa dini wanatakiwa kuelewa kuwa hakuna mtoto halamu,lakini wazazi waliomzaa ndio halamu.

Mtoto hajachagua kuzaliwa nje ya ndoa,lakini wazazi ndio walifanya mapenzi.

Na kwa kusema haya natangaza kuwa dini zenu zina upotofu kwa kuwatenga watoto wasio na hatia
 
Sasa mtoto anakuaje hana baba aisee. Na vipi mtoto akipatikana kabla ya ndoa na mkaoana mkiwa na huyo mtoto bado atakua hana baba??
 
Upo sahihi hata huku kwa wakristo ni hivyo hivyo .. Nilisoma kitabu cha Esta kwenye biblia kuna stori yake ilinivutia ikabidi niende deep kujua historia na namna walivyokuwa wanaishi wakati ule ... kwa wakati huo (ancient time) kule kulikuwa kuna wanawake walikuwa wanaitwa MASURIA ambao siku hizi mnawaitwa nyumba ndogo a.k.a Mchepuko hawa kisheria toka enzi za wafalme walikuwa ni Low class wife kwa mfalme na endapo watazaa basi watoto na huyo mwanamke haki zao za urithi zinakuwa limited tofauti na wale ambao wamezaliwa na mke wa kwanza wa mfalme.
 
nimesoma title tu.Ukoo ni bloodline haijalishi ilizaaje au na nan na kivipi.
watoto wangu ni royal blood wanatumia majina yangu
 
Sizani kama umenijibu swali langu nililouliza kulingana na nilichokuwa nimequote
Ww umeniuliza swali kana kwamba mtoto ni hadhabu kwa mwanamke na mimi nime kujibu kuwa mtoto sio adhabu kwa mama, mwanamke anaye hesabu kulea mtoto kama adhabu ni mpumbavu.
 
Kumpa mimba binti unaye jua huna mpango wa kumuowa ni moja wapo ya upumbavu na uzwazwa hata kama utajifanya kumlea huyo mtoto maana pamoja na kutoa matunzo lakini bado atakosa haki nyingi sana kutoka kwako ambazo wana zipata wenzake ambao umewazaa ndani ya ndoa.

Njia pekee ya kuzuia hilo ni kuacha uzinzi na mtulie ndani na wake zenu mnaharibu mabinti za watu kwa kisingizio cha akipata mimba nitalea.
Unaweza kumlea hujakatazwa unaweza kuwa unatoa matunzo lakini hutokuwa na haki wala amri yeyote mbele ya huyo mtoto bali mwenye mamlaka na huyo mtoto ni mama yake tu.
 
IPO kauli ya baadhi ya Ahlul ilmi ( Wanazuoni wa dino ya kiislamu) nafikiri mmojawapo ni Al-uthaimiin, kuwa mtoto wa nje ya ndoa anaweza kunasibishwa na baba Kwa masharti kadhaa, miongoni mwayo ni (I) Baba kumkubali mtoto kuwa ni wake (Ii) mwanamke aliyezaa na asiwe mke wa mtu (III) kusiwe na mtu mwingine anaedai pia kuwa mtoto husika ni wake.

Ninayoyakumbuka ni hayo juu, hivyo yakitimia hayo mtoto atapata haki zote apatazo mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa, Allah ni mjuzi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…