Je, Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi?

Ufahamu wako wa kuhoji haunitoshelezi Mheshimwa.

Uwepo wa nukta A hali yake ni lazima ufanane na uwepo wa nukta B?

Labda nilielezee kwa mifano: Tabaka la viumbe hai liko kwenye mpangilio wa kushangaza na wanasayansi kila mwaka wanakuja (wanavumbua) sheria mpya zinazoendana na mpangilio huo. Katika elimu ya fizikia, ili mabadiliko yaweze kutokea kwenye dutu, dutu hiyo itabidi ibadilike.

Mfano mwengine: Hewa ni mchanganyiko wa nitrogen 78%, oxygen 21% na noble gases ambayo ni 1%. Hewa si kitu kimoja bali ni mchanganyiko. Basi oxygen angezidi kipimo cha 21% angeweza kuyachoma mapafu yetu. Na angelikuwa chini ya 21% asingeweza kuchoma rutuba za damu. Na isingewezekana binadamu na wanyama kuishi. Kipimo hiki hakibadiliki kutoka kwenye sehemu kwenda nyengine hata mvua ikinyesha.

Haya ni mabadiliko yaliyo kwenye mpangilio wa kushangaza. Na mabadiliko haya hayajaanza leo wala jana, tangu dunia ilipoanza kusapoti uwepo wa viumbe hai mpaka sasa. Hii inaonyesha yupo aliyeweka huu mpangalio. Huu utaratibu upo pia ndani ya kanuni zinazojulikana za kifizikia, kimia, astronomy n.k. Mpangilio wa kanuni hizo upo kimahesabu.

Huu mpangilio si wa bahati mbaya, bali unaonekana una msimamizi, na msimamizi huyu anaonekana ni mwenye uwezo, mda wote yupo hai, mjuaji wa kila kitu, kusikia kila kitu, mwenye kuona kila kitu, mwenye kusema na mwenye kuumba. Kwa sifa kama kutokuwepo, kifo, ujinga, kutokuweza au kuondolewa na wengine, kulazimishwa, uziwi, upofu na ububu ni sifa zenye kasoro na hazijakamilika. Kwa hivyo basi sifa zenye kasoro kama hizo haziwezi kuwa kwa msimamizi, mleaji wa kanuni na mahesabu hayo maalumu.

Nukta yangu ni nini? Tizama sifa zake na sifa zako wewe zinaendana? Narudi awali kwenye swali langu; Uwepo wa nukta A hali yake ni lazima ufanane na uwepo wa nukta B? Sifa za A ni lazima zifanane na za B? Uwepo wako wewe ni lazima ufanane na uwepo wa Mungu? Nguvu zako ni lazima zifanane za nguvu za Mungu? Ufahamu wako ni lazima ufanane na wa Mungu? Hata logic inakataa.

Alikuwepo Mungu pasipo na chochote kuwepo!

Na nani aliyekuambia pasipokuwepo kitu, hicho kitu nacho hakipo? Space ipo, ipo kwenye nini?
 
Okay! Na maendeleo ya sasa vumbuzi kubwa ya nchi (maeneo) tofauti tofauti yanachagizwa na nini?
 
Okay! Na maendeleo ya sasa vumbuzi kubwa ya nchi (maeneo) tofauti tofauti yanachagizwa na nini?
Mkuu chunguza kwanini Wazungu miaka ya 1400's walianza kuizunguka Dunia,wakitumia nguvu kubwa sana na kuwekeza Pesa nyingi kuwa finance kina Captain Magellan, Christopher Columbus,Vasco da Gama, Hernandez Cortez nk kwenda pande za mbali za Dunia kuchunguza vitu?
Unaambiwa jamaa kama
Hernan Cortez alibeba tablets za Siri kutoka huko Jamii za Aztec, Maya, Peru nk
Tablets nyingine walizibeba misri na huko Mesopotamia ya Assyrian na Babylon wakaanza kuzifungua code Na ndio maana miaka 1880's mapinduzi ya viwanda yalitokea ghafla sana kiasi kwamba Kuna baadhi ya vitu kama ingines na mitambo mbali mbali ilianza tengenezwa Kwa Kasi sana na ndio Ilikua miaka ya mageuzi ya Dunia ndani ya Muda mfupi sana ukilinganisha na historia ya kuhusle miaka maelfu ila ndani ya Karne Moja tu Kila kitu kiakawa kimeundwa
Utaona magari,balloons,marine ingines,train ingines
Aircraft zikaanza kufanyiwa innovation
Mapinduzi mengi ya kijamii yalizuka na kuibadilisha Dunia kua kama ilivyo Hii Leo
Hii ilitokea ndani ya Karne Moja na nusu tu Kila kitu kikawa top
Mpaka miaka 1915 vita ya kwanza ya Dunia inapigwa watu walikuwa na mashine za hatari sana zilizoundwa Muda mfupi tu!

Hayo ni maendeleo yaliyochagizwa na Accient writings zenye ujuzi wa Hali ya juu na ndio maana mataifa makubwa yanajua Siri ya mchezo!
 
Hayo uliyoyauliza hapa kama masihara au kwakujivunia uzima wako yatakuja kukuadhibu soma coment zote ukimaliza naomba utubie kwa ulicho kiongea Mungu ni mwingi wa kusamehe ila ukikaza sana kichwa ukifa kaulize hayo maswali ukiwa kaburini utajibiwa
 
Kama Unakubaliana Na Hayo basi Hata Wale waliosema Sisi Tumetokana Na Nyani Wapo sawa.

Kwamba Nyani walibadilika Wakawa Binadamu. Kitu unachosema Kikichunguzwa Kwa Muda Mrefu kitaonekana Hakina Ukweli ndani yake. Kama Ilivyo kwa Binadamu kutokana na Nyani.

Na Yote hayo Hayatakuwa tofauti na Vitabu vya Dini Mbalimbali tu Hzii tulizonazo
 
Hadi leo hawaelewi jiwe la tani 10 linapandishwaje hadi kwenye kilele cha pyramid bila vifaa vya hydraulics kama vya sasa, na wakiambiwa hao wamisri wa kale walikuwa weusi wanagoma na kupindisha ukweli hasa kwenye movies zake. Mzungu hapa anatupiga changa la macho
 
Nakujibu hayo yote kwa namna rahisi kabisa. Katika chujio lenye vitundu vya sentimita 1, unategemea jiwe la sentimita 2 lipite? Na kila wakati yakipita mawe ya sentimita 1 tu na si mengine utashangaa? Ulimwengu wetu kuanzia mwanzo ni chujio, kinachokidhi vigezo tu ndio kinabaki. Hence evolution (natural selection and adaptation). Na nilishafafanua kwenye uzi huo chini

 
Namaanisha kabla ya ulimwengu kuumbwa, Mungu aliumba ulimwengu na kila kilichomo akiwa wapi? Je, alikuwa Mbinguni? Na wakati anaumba mbingu, alikuwa anaiumba akiwa wapi?
MUNGU NI MUNGU.... Yeye ni mwanzo, na pia mwisho. Alikuwepo tangu mwanzo, yupo na atakuwepo to the infinity. Wewe utaondoka na vizazi vyako vyote... Lakini yeye atakuwepo. Aliamuru ulimwengu nao ukatokeza... Hazuiliwi na nafasi , anakaa popote... Beyond space !!
 
Sijabisha, aliumba akiwa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…