Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 6,607
- 14,076
Ufahamu wako wa kuhoji haunitoshelezi Mheshimwa.Kwa maelezo yako ni kwamba hata yeye hakuwepo, kama ni absolute nothingness, in every sense of the word (unayoijua na usiyoijua) , means hakuwepo, hata consiousness yake, haikuwepo, ili kitu kiwepo, inabidi kiwepo. Haiwezekani kitu hakipo halafu useme kipo, how?!
Uwepo wa nukta A hali yake ni lazima ufanane na uwepo wa nukta B?
Labda nilielezee kwa mifano: Tabaka la viumbe hai liko kwenye mpangilio wa kushangaza na wanasayansi kila mwaka wanakuja (wanavumbua) sheria mpya zinazoendana na mpangilio huo. Katika elimu ya fizikia, ili mabadiliko yaweze kutokea kwenye dutu, dutu hiyo itabidi ibadilike.
Mfano mwengine: Hewa ni mchanganyiko wa nitrogen 78%, oxygen 21% na noble gases ambayo ni 1%. Hewa si kitu kimoja bali ni mchanganyiko. Basi oxygen angezidi kipimo cha 21% angeweza kuyachoma mapafu yetu. Na angelikuwa chini ya 21% asingeweza kuchoma rutuba za damu. Na isingewezekana binadamu na wanyama kuishi. Kipimo hiki hakibadiliki kutoka kwenye sehemu kwenda nyengine hata mvua ikinyesha.
Haya ni mabadiliko yaliyo kwenye mpangilio wa kushangaza. Na mabadiliko haya hayajaanza leo wala jana, tangu dunia ilipoanza kusapoti uwepo wa viumbe hai mpaka sasa. Hii inaonyesha yupo aliyeweka huu mpangalio. Huu utaratibu upo pia ndani ya kanuni zinazojulikana za kifizikia, kimia, astronomy n.k. Mpangilio wa kanuni hizo upo kimahesabu.
Huu mpangilio si wa bahati mbaya, bali unaonekana una msimamizi, na msimamizi huyu anaonekana ni mwenye uwezo, mda wote yupo hai, mjuaji wa kila kitu, kusikia kila kitu, mwenye kuona kila kitu, mwenye kusema na mwenye kuumba. Kwa sifa kama kutokuwepo, kifo, ujinga, kutokuweza au kuondolewa na wengine, kulazimishwa, uziwi, upofu na ububu ni sifa zenye kasoro na hazijakamilika. Kwa hivyo basi sifa zenye kasoro kama hizo haziwezi kuwa kwa msimamizi, mleaji wa kanuni na mahesabu hayo maalumu.
Nukta yangu ni nini? Tizama sifa zake na sifa zako wewe zinaendana? Narudi awali kwenye swali langu; Uwepo wa nukta A hali yake ni lazima ufanane na uwepo wa nukta B? Sifa za A ni lazima zifanane na za B? Uwepo wako wewe ni lazima ufanane na uwepo wa Mungu? Nguvu zako ni lazima zifanane za nguvu za Mungu? Ufahamu wako ni lazima ufanane na wa Mungu? Hata logic inakataa.
Alikuwepo Mungu pasipo na chochote kuwepo!
Na nani aliyekuambia pasipokuwepo kitu, hicho kitu nacho hakipo? Space ipo, ipo kwenye nini?