Kuna thread niliwahi andika ikahamishiwa jukwaa la Dini/ Imani.Kuna jukwaa ambalo wengi hatuwezi kuchangia?
Tunaweza kuingiaje huko, kuna mchango?
NIKO AMBAYE NIKO=YEHOVA."Niko, Ambaye Niko"
"I Am Who I Am"
BWANA, MUNGU; vyote hivi ni vyeoNIKO AMBAYE NIKO=YEHOVA.
Pengine amejitambulisha kama BWANA.
Pengine amejitambulisha kama BWANA Mungu.
Yote hayo ni Majina, Jina lake personal ni nani?
Soma (Wafilipi 2: 10-11) lipo Jina Moja pekee la Mungu lipitalo Majina yote ambalo tumepewa WANADAMU liwezalo kuokoa.
Ubarikiwe.
Ni Kweli, umeshalijua Jina lake pekee sawasawa na (Wafilipi 2:10-11)?BWANA, MUNGU; vyote hivi ni vyeo
Na utagundua kuwa pale MUNGU alipokuwa anakwenda kwa ajili ya misheni za kivita, mithili ya pale alipokuwa anaenda kuchoma SODOMA na GOMORA, alikuwa anatumia cheo BWANA, japo si kila cheo BWANA kilipotumika, alikuwa kwenye misheni
Nilipata kusikiliza muhadhara wa mtu mmoja anaitwa Dr. Ali Ataie ambaye alizungumzia kuhusu jina la Mungu kutoka lugha mbalimbali na imani mbalimbali, kama utakuwa interested na una wakati na bando lakutosha pitia link hapo chini.Salaam, Shalom!!
Mungu ni Jina la Cheo kikubwa kuliko vyeo na mamlaka yote Mbinguni na duniani.
Swali ni je, Mungu analo Jina lake binafsi?
Jina la Mungu ni nani?
Karibuni 🙏
Hilo Bado ni Jina la kificho.Niko ambae niko huyo ndio Mungu wetu
Ahahaha Basi na Yeye ni Msanii tu..Cos ni vipi kama Tusipotubu Kabisa?ina maana ndio Basi ataghairi asije?haha ..haya mambo haya yanachanganya sana ndugu yanguAnachelewa kurudi sababu anasubiri wewe Fendi utubu na kuacha DHAMBI.
(Wafilipi 2:10-11)Ushasema Mungu,ila ana majina mengi sana,niko ambae niko,
Mada inauliza kuhusu Jina la Mungu,Dini ni mind control systems
RUVAhii kumuita 'mungu' imeanza karibuni tu ila 'mungu' ni nomino ya kikundi kama 'binadamu'
miungu ni mingi sasa jina inategemea na dini yako
Sasa bila kuwepo Kwa Dini huyo Mungu ungemjuaje ?Mada inauliza kuhusu Jina la Mungu,
Wewe unaongelea dini,
Pana mahusiano Gani hapo?
Elimika ndugu!!
Kwa sisi waislamu Mungu ana majina 100.
Majina yanayojulikana na wengi ni majina 99 hilo moja wanalijua mitumie na wale watu wacha Mungu sana.
Ukilijua hilo jina chochote utakachokiomba ni rahisi kukubaliwa ndani ya muda mfupi sana.
Adam bustani ya Eden alimjua Mungu bila kuwepo dini yoyote.Sasa bila kuwepo Kwa Dini huyo Mungu ungemjuaje ?
We shetani anaogopa mamlaka sio jina. Unaweza tumia jina Yesu shetani asiogope kama huna muunganiko na mamlaka ya kimungu. Atakachofanya ni kukutandika viboko kwa nini umetaja hilo jina.Kwa Ukristo.
Mungu ni cheo cha juu anatambulika kama Jehovah.
Yesu ni nguvu kuu ya utendaji iliyo ndani ya Mungu.
Thus huwezi kemea pepo kwa jina la Mungu bali Yesu.
Shetani anaogopa jina la Yesu na sio Jehovah.
Imani au utashi, bila hiyo Mungu hana muda na huyo binadamu kwani yeye hana hasara, anaangalia wale wenye uhitaji, wamtafutao kwa bidii atawaruhusu wamjue, waujue ukuu wake.Adam bustani ya Eden alimjua Mungu bila kuwepo dini yoyote.
Ibrahim hakuwa na dini yoyote alipoitwa na Mungu.
Kumjua Mungu inahitaji Imani pekee, baas!!