1. Nani anaabudu sanamu? Kuabudu manaake nini?
2.Ni lini kanisa Katoliki limeruhusu ndoa za jinsia moja
3.ubatizo manaake nini na lengo lake nini?
Yesu aliwaagiza wafuasi wake hivi: “Mkafanye wanafunzi . . . . mkiwabatiza katika jina la Baba na la Mwana na la roho takatifu, na kuwafundisha kushika mambo yote niliyowaamuru.” (
Mathayo 28;19-20)
Kwanini mna lazima ha ubatizo uwe wa kuzamishana,ni wapi Yesu alisema ili mtu anayo we ni lazima azame majini?
4. Biblia inasemaje kuhusu padri kuwa mpatanishi wa Mungu na mwanadamu?
Mathayo 16;19
NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGWA MBINGUNI, NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGULIWA MBINGUNI.”
Kosa letu ni nini hapo?
5. Mnada kanisani manaake nini na huo mnada huwa unahusu nini?
6 Litrujia manaake nini na kazi yake ni nini?
7. Kanuni ya imani ina shida gani?
Kanuni ya imani inasema Hivi.
Nasadiki kwa Mungu mmoja (wewe husadiki)
Baba mwenyezi ( unakubali kuwa Mungu ni baba mwenyezi)
Muumba wa mbingu na nchi/dunia (unabisha)
Na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana (unakubali?)
Na kwa Yesu kristo bwana wetu (unapinga)
Ngoja niishie hapa,niambie kanuni ya imani ina shida gani?
Huujui ukatoliki,umekaririshwa na wachungaji wako namna ya kuutukana ukatoliki.