Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

“Kila ndoa ina mfumo wake wa kiuchumi kulingana na makubaliano ya wanandoa. Kama wote wanatoka asubuhi kwenda kazini, basi inapaswa kuwa na uwiano fulani wa majukumu ya kifamilia. Ila si lazima iwe sheria kwamba kila mwanamke achangie, inategemea maelewano yao. Kila mtu aishi kwa mfumo unaomfaa na mwenza wake.”
 
Ndiyo zinazotumika kupandia bodaboda au guitar uber kwendea kusikojulikana ila ndani hapana kuchangia,dadeki... bodaboda unakuta anatunzw vizuri kinoma.
Hahaha 😂 hii ni noma mkuu.
 
Maybe
 
Si suala la 50/50 kwa lazima, bali ni juu ya kila wanandoa kukubaliana kulingana na hali yao. Kama nitatoa mchango, ni kwa hiari, si kwa kulazimishwa. Kila ndoa ni tofauti, na cha muhimu ni maelewano na uwazi kuhusu majukumu ya kifamilia.
Sasa wewe unataka hiyo "lazima" ikae kwa mwanaume tu?
 
“Kila ndoa ina misingi yake, lakini muhimu ni uwazi na maelewano kati ya wanandoa. Kama wote wanatumia muda wa familia kwa kazi za kuleta kipato, basi ni busara kipato hicho kiwe na mchango kwenye maendeleo ya familia. Ila si kila mtu ana mtazamo huo, ndio maana mazungumzo kabla ya ndoa ni muhimu ili kuepuka migogoro ya baadaye.”
 
Si suala la 50/50 kwa lazima, bali ni juu ya kila wanandoa kukubaliana kulingana na hali yao. Kama nitatoa mchango, ni kwa hiari, si kwa kulazimishwa. Kila ndoa ni tofauti, na cha muhimu ni maelewano na uwazi kuhusu majukumu ya kifamilia.
Yeah, ndoa siyo vita vya maumau.
 
Hii mentality ndio inawafanya Wanawake wa Kiafrika kuwa loose sokoni; wewe aliyekwambia Mwanamke anayefanya kazi ni hiari kuchangia ni nani? Kwanini unatoka kwenda kazini? Unajua maana ya Wanawake kutoka kwenda kutafuta? Msibaki kama mikia ndio mana mnanyanyasika.

Halafu unaongea as if Wanaume hawalei watoto, mnasikitisha mjue. In short ndani ya ndoa hakuna kitu 'changu' kwenye ndoa kuna 'chetu' tatizo ni ubinafsi unawasumbua, eti kisa ni Wanawake, yaani mnafanana fanana kabisa privileges na Walemavu. Ninyi mna shida gani?

Yani mnabariki ubinafsi in the name of Mwanamke and Mwanamume. Huwa inawauma kutoa, kama hutaki kutoa kaa nyumbani, unatoka kutafuta nini sasa?
 
Lakini sheria ya ndoa haitambui hiyo mifumo ya kila ndoa. Nyie ni parasites na selfish sana
 
Au wasiolewe tu, wafanye kazi wapate pesa zao wenyewe.
 
Daah!! Mada ina mapambano balaa. Naungana na yule jamaa anayesema 'humanity is work' (ubinadamu kazi)😀
 
Si suala la 50/50 kwa lazima, bali ni juu ya kila wanandoa kukubaliana kulingana na hali yao. Kama nitatoa mchango, ni kwa hiari, si kwa kulazimishwa. Kila ndoa ni tofauti, na cha muhimu ni maelewano na uwazi kuhusu majukumu ya kifamilia.
Hakuna cha hiari, wewe ni mbinafsi tu. Suala la ndoa halina changu, wala chake. Kama unatoka kutafuta lazima utoe, utaishiaje kusema unatoka kwenda kufanya kazi, unaacha watoto nyumbani halafu unachopata kiwe hiari kutoa? Mna kichaa kizazi hiki kwa sababu hamkuelewa kwanini dunia imewapa fursa za kufanya kazi, nenda katafute urudishe kwenye ndoa na familia yako. Huwezi kaa nyumbani usubiri kuletewa, msitupunguzie mzunguko wa fedha.
 
Nikajua hoja Yako Ina evidence kumbe ni maoni tuu.

Kwangu ni lazima Kwa sababu hai make sense kwamba unapata hela harafu usipotumia kujenga familia Yako utatumika wapi?

Binafsi siko hapa kulea mtoto wa mtu,hiyo ni kazi ya mzazi wake
 
Unatoka saa 12 asubuhi unarudi saa 2 usiku utalea watoto saa ngapi, utatunza mume saa ngapi? embu acha blah blah zako
“Kila familia ina mpangilio wake. Muda wa kutunza familia haujapimwi kwa masaa, bali ni jinsi gani kila mmoja anavyochangia kwa pamoja.”
 
Tofautisha mwanamke msomi na yule wa kipindi cha nyuma, hawa wenye ajira ni jeuri,kiburi,na usawa wa kijinsia kwamba 50/50.
 
Mzee wa kimasikhara, kumbe uko vizuri hivyo. Bas ndoa yako na idumu milele.
 
Mimi ni housewife. Nafanya shughuli zote za nyumbani unazozijua wewe yeye jukumu lake ni kusupport financially. Akitaka na mimi nianze kutoa pesa zangu basi akubali na yeye kuosha vyombo. Ipo hivyo.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sijui kwann nimecheka.
 
Misingi ni upendo na wewe kukubali kuwa MSAIDIZI WA KILA HALI NA SIO NUSU NUSU!
Na ukubali pesa sio kitu Cha maana kuliko mumeo,yaani pesa makaratasi na suo big deal!

Leo mnaamini mwanamme mwenye Hela nyingi ndio mwanamme na sio mwenye upendo mwingi ndio inawachanganya na ndoa zenu!!

MATUMIZI YA PESA MMETANGULIZA MBELE BADALA YA KUWA MSAIDIZI MKUU WA MAONO YA MUMEO!!

RUDI KWENYE MISINGI!!

MIMI NI CONSERVATIVE WA MISINGI YA KIZAMANI ILIYO LETA MATUNDA HADI WEWE LEO UKAZALIWA !BIBI ZAKO WANGEKUA NA MTAZAMO KAMA HUU ULIONAO NAKUHAKIKISHIA WEWE UNGAKUA SEHEM YA UZAZI WA MPANGO NA USINGEKUWEPO!
 
HAPANA .

ANATAKIWA KUKAA NYUMBANI.

ILA KWAKUWA WAMEAMUA TUWE SAWA WACHANGIE KWA USAWA PIA.
Naelewa unavyosema, lakini kila familia ina muktadha wake na makubaliano yao. Kila mmoja ana jukumu lake la kuchangia kulingana na uwezo wake, na siyo lazima kuwa sawa kwa kila mtu. Hivyo basi, kuna umuhimu wa kujadili na kufikia makubaliano ya pamoja kuhusu mchango wa kila mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…