FurahayaMoyo
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 582
- 750
Kwani mwanaume anapolipia watoto wa dada zake wenyewe hawana baba yao? Sizani mke mwenye utimamu anaweza enda kulipia watoto ada za watoto wa ndugu zake ili hali wakwake bado, labda mwehu au kuwe na kitu hapo kati ya mke na mme.Lakini kabla ya kulipia ada watoto wa dada ni lazima kwanza nihakikishe watoto wangu wameshatimiziwa mahitaji yote, nitakuwa kichaa eti niwalipie ada watoto wa dada yangu hali yakuwa watoto wangu wamekaa nyumbani.
Sasa inashangaza kuona ww mwanamke watoto wana mahitaji fulani mwanaume ana kuambia sina pesa ebu na ww yatatue una kataa eti hilo siyo jukumu lako ila unaenda kutua matatizo ya watoto wa dada yako ambao nao wana baba yao mwenye jukumu la kutatua matatizo hayo.
Kabla ya kutoa msaada nje ni lazima uhakikishe kuwa ndani ya familia hakuna pengo lolote sio unaacha pengo kwenye familia yako unaenda kuziba mapengo kwenye familia za wenzako.
Na aliyesema Adam utakula Kwa jasho na wewe Eva utazaa Kwa uchungu alimaanisha nini?Majibu yapo kwenye biblia kama we ni msomi kasome!
Mwanamke aliumbwa kama msaidizi Kwa mwanamme Kwa Hali zote!hwakusema kulea watoto TU na kupika !MSAIDIZI!
ukisoma mithali 31 najua hampendi kusoma na hamtaki kukubaliana mwanamke anaonekana anachapa KAZI na anafananishwa na merikebu ya chakula yaani meli iliyosheni vyakula! Akileta mapato nyumbani mwake!!
Kizazi Cha kikahaba Cha wanawake wa kileo kilichojaa ubinafsi kinataka kujiuza ndani ya ndoa Kwa kutoa mchango wa tendon la ndoa na mapishi plus kulea watoto TU ndicho kinachosumbuka na kuuliza uliza maswali kana kwamba hakijui asili na wajibu wake!!
Tangy zamani bibi zetu walilima mazao ya biashara na mababu zetu ,walikamua ngombe wakauza maziwa na mapato wakayaleta ndani ya familia na kulea wakalea watoto katika bidii na kazi!na mababu wakabaki kama viongozi wenye kuongoza jahazi na kutoa uelekeo familia iendapo!!!
MWANAMKE UNAEJIULIZA MASWALI KAMA HAYA UNAPASWA UKASOME HISTORIA YA BIBI ZAKO WALISHIRIKI VIPI SHUGHULI ZA KIUCHUMI NA KUSAIDIA FAMILIA ZAO,PIA KASOME MITHALI 31!
zamani hakukua na michepuko coz mitara iliruhusiwa na baba alioa pale alipopataka!Sasa leo Dini zimekataza tusioe mitara nasema DINI na sio maandiko Wala neno la Mungu wamekataza mitara ndio mnalia na michepuko kama kigezo Cha kuleta ubinafsi ndani ya familia!NASEMA DINI NA SIO MAANDIKO YA MUNGU!HAKUNA MWANAMME ANAWEZA KUWA MKRISTO KULIKO IBRAHIM BABA WA IMANI MWENYE WAKE WAWILI,YAKOBO MWENYE WAKE WANNE,MUSA MWENYE WAKE WAWILI,YESU HAKUOA MSIFANANISHE ANGEOA TUNGEANDIKA MENGINE!!
RUDINI KWENYE MISINGI ACHENI KUULIZA ULIZA NA MAJIBU MNAYO!
Unazani utakuwa wakwanza? Watu wanaishi hivyo kila mtu na kwao na wapo hivyo na ndoa zikafa kimya kimya, nilishuhudia rafiki wa kaka yangu alifiwa baba yake mkewe hakuonekana kaka yangu kamuuliza shem yupo wapi? Kasema mie sikwenda kwenye msiba wa baba yake hivyo aliapa naye hatokuja angalia maisha kama hayo!Ukiniletea hii mentality mimi mbona utafurahi, yaani hata kukuachia hela ya matumizi ndani itakuwa ni hiari yangu sio lazima, ukipatwa na changamoto binafsi kama kufiwa,kuugua kukusaidia kwangu kutakuwa ni kwa hiari sio lazima. Kiufupi tu vitu vingi sana nitavifanya kwa hiari na sio kama wajibu... maana unajifanya mbinafsi hivyo mimi nitakuonesha ubinafsi uko vipi na unafanywaje
Ngoja nikuache unaonekana unaroho mbaya sana, itakuwa mkeo akipata hela kidogo lazima uikombe uipangie majukumu hutaki awe na chochote.Kwa hiyo unataka kwa vile mimi ndugu yangu nimemsaidia laki 2 na kwa ndugu yako pia nifanya hivyo hivyo sio? Yaani nichukue laki 2 mfukoni mwangu nimpe ndugu yako wakati huyo ndugu yako ana ndugu zake ambapo wewe ni mmoja ya hao ndugu zake na unafanya kazi? Uwendowazimu siwezi kufanya hata kidogo.. na hii ni level ya juu kabisa ya toxic entitlement ya nyie wanawake kujiona mna mamlaka na pesa za waume zenu...
Sasa kosa lake hapo liko wapi? Kwani ni kweli kwamba ameoa ukoo mzima wa nyumbani kwenu? Si amekuoa wewe tu, sasa kwanini umbebeshe mumeo majukumu ya huko nyumbani kwenu? Kaka zako hawapo? Na hao wazazi wako walikuwa wanafanya nini ujanani mwao mpaka leo waje wamtegemee mkwe wao ndio awatunze? Haya malawama pengine huwa ni ya kipuuzi sana, halafu mara nyingi wanawake wenye mentaliy hii ya kutaka mume awasaidie mpaka wazazi wake hawanaga shukrani... unaweza ukamsaidia yeye na hao wazazi wake ila siku mkitofautiana kidogo tu au ukasitisha msaada kwa sababu zilizoko nje ya uwezo wako utashangaa unaambiwa una roho mbaya au mchoyo, wanasahau kabisa uliyowahi kuwafanyia huko nyuma.
Sio wajibu wa mwanamke kuhudumia familia kifedha. Mke anamsaidia mume wake namna ya kupangilia na kutumia fedha zake kuhudumia hapo nyumbani
Ndo ushangae na ww alafu mkiachana anataka mgawane 50 kwa 50 kwenye mali za familia ambazo alikuwa anasema si jukumu lake kuziendeleza.Nilivyosoma comment kwenye hii thread nimegundua wanaume mtaani tumebaki wachache
Haingii akilini mwangu eti kipato cha mke wangu ni chake na ndugu zake ila kipato changu ni cha mke wangu na watoto.
Ninashukuru mke wangu tunashirikiana vizuri sana katika mgawanyo wa kipato na tunaishi kwa furaha
Kama unajijua hutakiwi kula kwa jasho mbona usikae nyumbani ukalea watoto alafu mmeo akatafuta pesa za kujenga familia?Na aliyesema Adam utakula Kwa jasho na wewe Eva utazaa Kwa uchungu alimaanisha nini?
Inategemea na wwe unataka mke wa aina gani business partner au mlezi wa familiaNB usioe Mwanamke goli kipa kwenye karne hii ya 21
Ishu ya uchumi ni jukumu la mwanaume bora nioe mama wa nyumbani lakini ananipa energy ya kupambana ananipa amani na utulivu wa akiliUsioe mwanamke ambaye hana mbele wala nyuma kiuchumi .
Wee chilumendo chapee (nkûune)Nilivyosoma comment kwenye hii thread nimegundua wanaume mtaani tumebaki wachache
Haingii akilini mwangu eti kipato cha mke wangu ni chake na ndugu zake ila kipato changu ni cha mke wangu na watoto.
Ninashukuru mke wangu tunashirikiana vizuri sana katika mgawanyo wa kipato na tunaishi kwa furaha