Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Kwa mfano kama mke wangu hana kipato au pesa mimi sina shida naye at all ila kitu ambacho sitakikubali ni mwanamke kuwa na kipato halafu hataki kuitumia katika familia.
Mwanamke akiwa na pesa halafu hataki kuitumia katika familia atazifanyia nini? Naomba nijibu Kwanza hapa.
 
50/50 ni kuhusu ushirikiano na msaada. Huwezi kupima mchango wa ndoa kwa kiwango cha kifedha tu. Usawa wa ndoa unahusisha kujitolea, kuelewana na kusaidiana kwa njia nyingi, na siyo tu kwa michango ya pesa.
Na ww ni muumini wa fifty fifty?
 
Muda wa mke ni muhimu, lakini siyo lazima awekwe kwenye majukumu ya nyumbani pekee. Mama ni sehemu ya familia, na mchango wake unaweza kuwa kwenye kazi au biashara pia. Ikiwa mke anafanya kazi kwa faida ya familia, si vibaya, bali ni njia ya kusaidia familia kwa namna nyingine. Kuweka dada wa kazi siyo kwa ajili ya kupunguza mzigo wa mama, bali ni kuhakikisha kila mmoja anachangia kwa manufaa ya familia. Kazi ya mke ni muhimu, kama vile ya mume, na sio lazima kila kipato chake kionekane mara moja. Kila mmoja katika familia ana mchango wake.
 
Sio wajibu wake ila ni kwa hiari. Lakini inapendeza akifanya hivyo kama anao huo uwezo.
Yaani mwanamke uwe na pesa halafu utumie peke yako lakini pesa zangu tutumie wote?

Hiyo wafanyie wanaume malofa na mabushoke lakini siyo mimi, kwenye ndoa pesa zangu ni zako na zangu ni zako.

Asubuhi njema.
 
**Rahisi sana hii:-
1.Ikiwa mwanamke hafanyi kazi,ama anafanya ila wewe ndio umemuajiri kwenye miradi ya familia,hapo hatawiki kuchangia hata shilingi 1.
2.Mwanamke Nesi,Dereva,Mwalimu,mfanyabishara etc,unatoka na yeye anatoka kwenda kazini,mwisho wa siku wewe una muhudumia Tena,huo ni uhanithi na hamna maana ya ndoa hapo,**
 
Mkishafunga ndoa wote mnatumia muda wa familia kwaiyo ni lazima kila mmoja autumie huo muda kwa mambo ambayo yanaleta input kwenye familia. Mwanamke kwenda kutafuta halafu anachopata kisiwe na mchango wowote kwenye familia hayo ni matumizi mabaya ya muda wa familia.

Nina dada angu anafanya kazi benki, kipindi cha karibia na ndoa yake alituambia, akiolewa mizinga ya hapa na pale tupunguze kwa sababu akiingia ndoani wajibu wake utabasilika kwa maana ya kwamba anachopata hakitakua kipato chake binafsi tena
 
Hicho ndo tunacho maanisha ni lazima kila kitakacho kuwa kinafanywa na mwana ndoa basi kiwe ni kwa ajili ya manufaa ya familia kwa ujumla na si kwa faida za kibinafisi.
Haiwezekani eti mwanamke unafanya kazi una pata pesa alafu eti hizo pesa zako zisiwe na jukumu la kutatua matatizo ya familia ila kwa hisani.
 
Yaani mwanamke uwe na pesa halafu utumie peke yako lakini pesa zangu tutumie wote?

Hiyo wafanyie wanaume malofa na mabushoke lakini siyo mimi, kwenye ndoa pesa zangu ni zako na zangu ni zako.

Asubuhi njema.
Hiyo ni wewe na mke wako hatuwezi kukuingilia. Wengine tupo na wanaume ambao wanawajibika kwa kila kitu bila manung"uniko na tunasaidia pale inabobidi na hata tusipo saidia maisha yanasonga maana atatekeleza ni wajibu wake. Kama hataki aende huko na yeye akaolewe..
 
Ya kwamba kuhudumia watoto wako ulio wazaa sio wajubu wako ?
Nahudumia pale ninapotaka na sio lazima kama mume yupo na anao uwezo wa kucover kila kitu.
 

Ndoa itakushinda
 
Hahahaha 🤣 kama mmekubaliana ni sawa, pesa zenu mkazitumie kuhonga vijana wenye miguvu ya kiume.
 
Unatoka saa 12 asubuhi unarudi saa 2 usiku utalea watoto saa ngapi, utatunza mume saa ngapi? embu acha blah blah zako
 
Mwaka wa tatu huu sijawahi kuuliza mshahara wake anafanyia nini Ila yuko smart sometimes unakuta kanunua kitu flani for the sake of the family...!! Pia anasave sana hata ikitokea nimetingwa huwa anasupport but NEVER ASK WOMAN TO CARE FOR THE FAMILY.. mambo ya kodi sijui ada hela ya chakula nyumbani bills zote Mwanaume pambana unaepusha ugomvi usiokuwa na lazima.
 
Jibu la swali lako linategemea na tamaduni na imani ya jamii fulani. Kwa ulimwengu wa sasa kutoa fedha Katika familia ni hiari kwa wote.
 
Kama anajielewa ni afadhali siyo dude Lina hela alafu siku wewe kukosea hela mnalala na njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…