Je, mwanamke uko tayari kumpa pesa mchumba wako akakulipie mahari kwenu?

Je, mwanamke uko tayari kumpa pesa mchumba wako akakulipie mahari kwenu?

We jaribu hata siku moja kuomba hela ya mwanamke ukanunue shati la sh 10000 uone moto utakao waka hapo. Ila wao ni sawa kukuomba 50,000 akanunue nguo ya kuvaa kwenye send off ya rafiki yake.
Kumpa hela mwanaume kwa ajili ya matumizi pale inapobidi sio shida.
Shida kutoa mahari,,lol hapana kwa kweli.
 
Kumpa hela mwanaume kwa ajili ya matumizi pale inapobidi sio shida.
Shida kutoa mahari,,lol hapana kwa kweli.
Mlivyo wagumu kutoa hela zenu sijui wenzetu huwa mnazitoa wapi ? Mwanauke akikuomba 5,000 tu utajiuliza maswali 200. Huko kwenye mahari ni mbali sana.
 
Mlivyo wagumu kutoa hela zenu sijui wenzetu huwa mnazitoa wapi ? Mwanauke akikuomba 5,000 tu utajiuliza maswali 200. Huko kwenye mahari ni mbali sana.
Itakuwa uliyekutana nae wewe tu.
Mimi sioni shida kumsaidia hela mwanaume wangu ninayempenda kwa dhati anapopata tatizo na anahitaji msaada.
Kama ninayo Nampa,tena simkopeshi...Nampa kwa moyo MMoja.
Kumuomba hela Ni Hadi niwe na shida kubwa ya muhimu ambayo nyumbani wameshindwa kabisa kunisaidia...na Mara nyingi shida zangu zote huwa najitahidi kuzisolve kwa msaada wa wazazi..kwa hiyo mwanaume kumuomba hela atakusikia tu redioni.

Kumnunulia zawadi sio shida.

Ila kumpa/kumkopesha hela ya mahari...sijui labda ngoja nizeeke kwanza.
 
Hehehehhe. Ukipenda unakua kipofu. Kuna mtumishi mwenzangu yeye alimpaga boy wake hela akaenda kumtolea mahari. Ila sasa boy anavyomdharau, kinyesi kuna uafadhari.
Mwanaume kaliyekamilika hawezi kukubali kulipiwa mahari ili ndoa ipite hata kama hana uwezo,wengi wanaume wa hivyo ni Mario na wanakuwa na dharau kiwango kikubwa
 
hiyo mbona unampa bila wasi wasi ...pesa kama izo za siku moja moja sio mbaya ...ila isiwe ndo mazoea ...
We jaribu hata siku moja kuomba hela ya mwanamke ukanunue shati la sh 10000 uone moto utakao waka hapo. Ila wao ni sawa kukuomba 50,000 akanunue nguo ya kuvaa kwenye send off ya rafiki yake.
 
Dunia Ina mambo aisee [emoji134][emoji134].
Kwenda kuolewa na mtu anayekaa tu nyumbani Kama mgonjwa,analishwa na wazazi[emoji134][emoji134]!!
Yaani huyu dada nae akaenda kutegesha mimba hapo???
Wanaume kweli wajifunze kutafuta.
Kama mtu hawez tafuta hela ya mahari,, familia ataiwezea wapi kuitunza??
Ndo kupenda uko mkuu...wanawake wakipenda wanapenda haswa...yani apo haoni ata kama anateseka , anaona tu heri
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na hali halisi ndani ya nyumba unaionaje?
 
Kama mahari inamshindwa Mwanaume kuhudumia Familia ataweza kweli,mahali sio lazima iwe million mwanamke unaangalia uwezo wa mpenzi yaani hata kubeti ili apate mahali kutamshindwa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Hivi kuna ulazima wa MAHARI ? Kwa nini wazee wenu wasitugaie nyie bure ukisema wamewalelea hadi hapo mlipofika hata mwanaume kalelewa na wazazi wake na bado anaendelee kukulelea wewe na watoto mtakaowapata

Hivi kuna umuhimu gani wa hii
BARTER TRADE ?
 
Ndo kupenda uko mkuu...wanawake wakipenda wanapenda haswa...yani apo haoni ata kama anateseka , anaona tu heri
Huko Ni kupenda kijinga.
Ndiyo wanawake tunapenda lakini nadhani kila mtu Ana vigezo vya mume anayemtaka.
Hivi upende tu kichwakichwa,mtakula upendo???
Sitaki kuja kushuhudia wanangu kuwa ombaomba.
 
Dash,kuna jamaa alioa kwa mtindo huo, sasa hivi,mwanamke aliempa pesa ya mahari,hana kazi,jamaa na yy yupo yupo tu,imebidi akaishi na mkewe kwa wazazi.wanalishwa na baba wa mume.
 
Back
Top Bottom