Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Inafikirisha na msingi wa swali langu ulikua hapa hua inakuje kuaje yaan mtu unapata taarifa za mbele?
KUna mtu wangu pia wa karibu huwa anaona vitu mbele ,akiona kitu kwenye ndoto huwa kinatokea ,sasa baada ya kuona vitu mbele ya muda basi wazee wakamshauri akiota kitu kibaya basi akistuka aamke na akemee ili kisije kutokea.
Wewe umenielewa sana asantee
 
Nimefurah kuona ww uko upande wa pattern za Ubongo.

ila kuna matukio kadha wa kadha yanatokea, mfano watu wanaota kuna kifo cha watu wao wa karibu. Bila hata kuambiwa nan anaumwa au nan atapata ajali. Na inatokea kweli.

Pili Kuna hii simpe asf.
Unawaza kuna mtu hujamchek kwa muda mrefu, miezi au mwaka. ila unanyanyua sim kumpigia akipokea anakuambia nilikuwa nakuwaza. Au nimekuwaza muda si mrefu na ndio ww unapiga.
unaweza kusema ni Ubongo wako ww na ubongo wake ukakumbuka?. Kwa wakat mmoja?.
Hapa sio pattern maana ni muda umepita . Na sio bahat maana utakuta wote hamjawah kuwazana for months or days. Iweje coincedence itokee same day same hours na minutes? .

thus why nina amini kuna power iko beyond na ina control haya.
 
Castle_Lite umeelewa sana hii mada japo watu wanatoa majibu mepesi
Et Patten yaan ki vp ?
 
Kama hakuna anayewajibika, kwanini kuna haki?

Lawama ndiyo kitu pekee kinachotutofautisha na wanyama.

Tukiachana na lawama basi unapaswa kukubalia agency Mkuu.

Sawa bro. Basi naomba niambie ni nani anayewajibika kwa haya yanayotutokea na anawajibikaje ?.

Kwa sababu ni madhara.
 
Hawawezi kupata majibu ya hayo kwa kuufanyia ubongo research. Ubongo ni tangible, physical.

Hayo mambo yana uhusiano na connection katika uhalisia wetu ambao hauonekani, haushikiki.

Kule unakoota ndoto ndiko kwenye uhalisia wako. Na sio ulimwengu wa siri kwakua kila mtu anapoenda usingizini huingia kwenye hiyo realm. Ni tunakosa tu attachment na uhalisia kiasi kwamba hao wachache wanaonekana maalum.

Fikiria mara ngapi imetokea unamfikiria mtu, muda huo huo anakupigia simu.. au wewe unampigia, anakwambia nilikua nakufikiria sasahivi.

Dimension ya kule tunakoita usingizini, kila kitu kipo reachable kwa kila mtu, tofauti ni strength ya connection yako na ule ulimwengu
 
Kupata ajali si jambo geni kwa akili ya mwanadamu.

Akili yako tayari inajua kwamba ajali zipo na huweza kutokea kwa yeyote muda wowote.

Kuota ndugu yako anapata ajali, hakufanyi apate ajali kweli.

Kwa hiyo Kuota ndoto na Kupata ajali ni Mutually exclusive events.

Ni matukio mawili ambayo hayawezi kutokea kwa pamoja kwa wakati mmoja.

Ndugu yako anaweza kupata ajali bila wewe kuota.

Kuota leo ndugu yako amepata ajali, halafu ipite siku, wiki, mwezi au mwaka halafu ndugu yako aje Kupata ajali kweli. Hakufanyi ndoto yako uliyoota kabla iwe ndio imetimia.
 
Mkuu nadhani kuna kitu haujakielewa hapo, yeye ameelezea namna ubongo unavyo fanya kitu kinaitwa constant risk assessment.

Iko hivi, ndoto ambazo wengi huwa wanaziona kama ni maono, yale huwa ni matokeo ya kile wanacho kutana nacho kwenye maisha yao ya kila siku (matukio ya siku zote, kuanzia unayoyaona mtandaoni mpaka yale mnayoyaishi mtaani).
 
Ndoto ni mkusanyiko wa mambo unayoyaona kuyasikia na kuyahisi kila siku
ukiota kwa mfumo wa video_
ukiota kwa mfumo wa kuhisi_
ukiota kwa mfumo wa sauti tuu huo ni ujumbe uzingatie!
 
Kuna mtu anaota kuna mtu kafa hata kabla kifo hakijatokea na hata kama hana taarifa kuna family member mgonjwa. Hii inaletwa na nini?
 
Ndoto ni mkusanyiko wa mambo unayoyaona kuyasikia na kuyahisi kila siku
ukiota kwa mfumo wa video_
ukiota kwa mfumo wa kuhisi_
ukiota kwa mfumo wa sauti tuu huo ni ujumbe uzingatie!
Na wale wanaoota vitu ambayo hawajawahi hata kuviona au kuvifahamu halafu baadae inatokea kweli inakuwaje?
 
Shukran mkuu🙏🙏
 
Mkuu nadhani kuna kitu haujakielewa hapo, yeye ameelezea namna ubongo unavyo fanya kitu kinaitwa constant risk assessment.
Ooh sawa Asantee
Iko hivi, ndoto ambazo wengi huwa wanaziona kama ni maono, yale huwa ni matokeo ya kile wanacho kutana nacho kwenye maisha yao ya kila siku (matukio ya siku zote, kuanzia unayoyaona mtandaoni mpaka yale mnayoyaishi mtaani).
Kwahiyo ndoto ni matokeo au matukio ya kila siku ooh sawa sawa

Vipi kuhusu matukio tunayoota kwanza halafu baadae ndio yanatokea kwa namna ya kufikirisha ?
Sijui hata niseme vp uelewe
 
Ndoto ni mkusanyiko wa mambo unayoyaona kuyasikia na kuyahisi kila siku
ukiota kwa mfumo wa video_
ukiota kwa mfumo wa kuhisi_
ukiota kwa mfumo wa sauti tuu huo ni ujumbe uzingatie!
Asante
 
Hatuwezi kujua tusivyo vijua.

Lakini tuna endelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, udadisi na uchunguzi zaidi.

Kuto kujua kwa nini jambo fulani hutokea, Sio hitimisho la moja kwa moja kwamba kuna high power ina control mambo.

Bado uelewa wetu na akili zetu zimeshindwa kutafiti vya kutosha kuelewa jinsi mifumo ya mwili na akili zetu inavyo operate.

Kusema kwamba kuna high power, kwanza kutahitaji uthibitisho wa hiyo power yenyewe, tuchunguze tujue, ipo au haipo.

Na sio kuamini tu kuna high power bila uthibitisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…