Monetary doctor
JF-Expert Member
- Oct 20, 2022
- 14,350
- 27,420
ni kweli mkuu, miaka takriban elfu mbili ni mingi sanaUtapoteza nguvu kwa hao wakatoliki kwanza wao wana misimamo wala hawabishani na mtu kwani wao ndio wameanda bibilia na hizi sherehe za christmass,Pasaka,Ijumaa kuu
Baada ya kupitia historia kupitia kwenye makongamano ya kisabato ndio nikajua nguvu zao,Wasabato wao wanasoma sana vitabu baadhi katoliki walivyoficha hivyo wana uelewa mpana zaidi kidogo
Wanawekeza kwenye ardhi na majengo dunia nzima,Wakiamua kujenga kanisa sehemu nzuri watakununua kwa pesa yeyote ile
Kama ni mwenyeji wa Dar hao watu wamepima upepo wameamua kwenda kujenga Basilica haijawahi kutokea huko kigambona baada ya kuona ST Joseph pa askofu wao mambo yao hayaendi wanavyotaka
Elewa aliyeandika bibilia ni huyo mkatoliki,Akafika sehemu na kuandaa kalenda tunayotumia sasa ya Papa Gregory inaitwa gregorian Calender
Mkatoliki akafuta miaka ya nyuma akaanza kuhesabu na leo ni mwaka 2025
Amekusanya maandishi akayaunganisha na mengine akayaacha hapo vatikana na vitabu hivyo vipo kwanini hakuviweka na kwanini alivitoa anajua yeye
Akaa akaamua kuweka mistari na namba kwenye bibilia huko watu wakibishana soma mstari huu mara ule yeye mwenyewe haongelei hiyo soma hapa wala pale
Makumbusho ya Vatikani yana siri nyingi,Ukifika huko utaacha hata kusali na utajiuliza mbona wao wanasali
Swali lako ni la msingi sanaβna linaonyesha unafikiri kwa kina! π Hebu tuchambue kwa uangalifu kuhusu swali hili muhimu:
---
π Je, Mtume Petro ndiye Papa wa kwanza?
β Ndiyo β Kwa mafundisho ya Kanisa Katoliki
Kanisa Katoliki linamchukulia Mtume Petro kama Papa wa kwanza, ingawa jina "Papa" halitumiki kwenye Biblia ya awali. Huu ni msingi wa kihistoria na kiimani zaidi kuliko lugha halisi.
π Sababu ya Kumuona Kama Papa wa Kwanza:
1. Mathayo 16:18-19
Yesu anamwambia Petro:
- Kanisa linafasiri maandiko haya kwamba Yesu alimpa Petro mamlaka ya kipekee ya kiroho β yaani kuwa kiongozi wa Kanisa hapa duniani.
- Petro (Kiyunani: Petros) linamaanisha "jiwe" au "mwamba".
2. Petro Alichukua Nafasi ya Uongozi
Katika vitabu vya Matendo ya Mitume:
- Petro ndiye anayeongoza mikutano ya mitume (Matendo 1:15).
- Anaongoza uchaguzi wa Yuda mwingine (Matendo 1:20-26).
- Ndiyo anayetoa hotuba ya kwanza ya kanisa baada ya Pentekoste (Matendo 2).
- Anafanya maamuzi muhimu katika baraza la Yerusalemu (Matendo 15).
- Neno "Papa" lilianza kutumika baadaye (karne ya 3 au 4), kutoka neno la Kilatini "papa", likiwa na maana ya "baba wa kiroho".
- Hapo awali lilitumika kwa viongozi wa kiroho wengi, lakini baadaye likahifadhiwa kwa Askofu wa Roma pekee.
---
ποΈ Kuhusianisha Petro na Roma:
- Inasadikika kwamba Mtume Petro alihubiri na kufa Roma, ambako aliteswa na kuuawa (kupitia kusulubiwa kichwa chini).
- Askofu wa Roma, anayefuatia kutoka kwa Petro, anachukuliwa kama mrithi wake wa kirohoβhivyo jina Papa.
---
π Hitimisho:
- Ni kweli jina βPapaβ halipo kwenye Biblia, lakini kanuni ya uongozi wa Petro ipo wazi katika maandiko.
- Kanisa Katoliki hutumia historia, mapokeo, na maandiko pamoja kueleza kwa nini Petro ni Papa wa kwanza.
---
wengi hawajui kanisa ni nini ? wengi hawajui ukweli ni nini ?Baada ya muda mrefu kuwa nipo kanisa katoliki nikasema nijaribu huku kwingine
Hawa wanao jiita protestant kama wao wapo sahihi mbona ninyi kwa ninyi mna matabaka kama kumi+
Ukiwaangalia Lutheran wana mgawanyiko wao huko kuanzia Moravian, sjui Methodist, ukija hapa Tanzania tuu Lutheran ina migogoro sijawahi ona, mpaka Arusha wana dhehebu jingine kutoka Lutheran church,
Hujaja kwa Anglican wana lower Anglican hii kama walokole flani, afu kuna hii Higher Anglican ambayo kwa sehemu kama 80% inafanana na kanisa katoliki. Hizo ni tofauti baina yao binafsi
Njoo kwa Hawa wanaojiita walokole,
Kuna mlokole TAG, FPCT, MASHAHIDI WA JEHOVA, EFATHA, JESHI LA WOKOVU, RGC, na hao wote wana taratibu zao Kuna ambao wanasema kanisa hili halina upako kama letu wanavyosali sio kama sisi yaan tafrani tupu
Nibaki zangu kanisa katoliki pengine Lina mapungufu kadhaa lakini Ibada zake zina utaratibu na uwepo wa kipekee, tofaut na baadhi ya makanisa mengine.
Kanisa halitetewi kwa Upanga,
ila alimteua petro kua kiongoziKwa maoni yangu yesu aliwapenda wanafunzi wake wote na wote walikuwa sawa
acha kueleza maandiko jinsi unavyotaka wewe, naona neno mtume linakuchanganya sanaila alimteua petro kua kiongozi
"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni..."
"Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewaomba kuwapepeta kama vile ngano; lakini mimi nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakapoongoka, waimarishe ndugu zako."
βLisha kondoo zanguβ¦ chunga kondoo zanguβ¦β
Mitume walikuwa wanasali kanisa gani?kama katiliki sio kanisa La kwanza je kanisa la kwanza ni lipi ?
Hivi hawa kina mwamposa na manabii sijui kiboko ya walozi kuna mwengine anajiita somebody lukulelo huwaga ni walokole au waganga wa jadi?Njoo kwa Hawa wanaojiita walokole,
Kuna mlokole TAG, FPCT, MASHAHIDI WA JEHOVA, EFATHA, JESHI LA WOKOVU, RGC, na hao wote wana taratibu zao Kuna ambao wanasema kanisa hili halina upako kama letu wanavyosali sio kama sisi yaan tafrani tupu
Nibaki zangu kanisa katoliki pengine Lina mapungufu kadhaa lakini Ibada zake zina utaratibu na uwepo wa kipekee, tofaut na baadhi ya makanisa mengine.
Kanisa halitetewi kwa Upanga,
Umesomeka chali ya kwakwanaomba kuuliza alisurubiwa na nani ? na petro aliishi kwenye kipindi cha ufalme gani ? naomba pia niambie sababu ya kusulubiwa kwake ni nini ?
naomba pia uniambie petro alifundisha utaratibu huo wa ibada ulio utaja kutoka kwa nani ? kama ni kwa yesu wapi yesu alifundisha hizo ibada za sanamu, za kumuabudu maria ?
unajua maana ya mtume ? ngoja nikwambie mtume maana yake ni mtu aliye tumwa na flani kwaajili ya kupeleka kitu flani hii ndio maana ya mtume
Ukiangalia katika maneno ya mwisho ya yesu kabla hajapaa mbinguni aliwaambia nendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu mka wafundishe yale yote niliyo wafundisha ikumbukwe mitume waliishi na yesu miaka mingi kwa kadhaa wali kaa na yesu walikula na yesu walitembea na yesu wakifundishwa na mafundisho yote yapo kwenye biblia pekee hakuna hizi ibada za maria au za sanamu au za kusherekea kuzaliwa kwa mungu kila mwisho wa mwaka hakuna kitu hicho.
nime furahi kuona kuwa unajua historia, kama shida yako ni mitume ndio inakuchanganya ngoja nikuambie.
ukitaka kuujuwa ukweli na uokolewe fuata nyayo za yesu na matendo aliyoyafanya na mafundisho aliyo yatoa pekee kutoka kwenye biblia, biblia ndio ya kweli na ndio mwongozo kumbuka yesu ni mkubwa kuliko mitume na manabii hivyo alikuja ili kukuonesha jinsi tunavyo paswa kuishi na kutenda aliwachukua mitume wengine walikuwa ni wavuvi wengine walikuwa ni watoza ushuru aliwakusanya akawafundisha kwa miaka kadhaa baadae akawatuma ulimwenguni wakawafundishe na wengine yale aliyo wafundisha kisha yeye akaondoka.
wengi hawajui kanisa ni nini ? wengi hawajui ukweli ni nini ?
Hayo makanisa yote ukijumuisha na rumi sio makanisa ya mungu wa mbinguni, ukweli na kuushinda uzushi na uongo ni kujifunza na kufuata nyayo za yesu katika matendo yake moja kwa moja kutoka kwenye biblia,
yesu hakuwa mrumi wewe unakuwa mrumi kama nani na kwa miongozo ya nini ? wewe unakuwa mprotestanti kama nani na kwa miongozo ya nani kadhalka wewe unakuwa msabato au mlikole kwa muujibu wa nani ?
Hakuna hata nukta kwenye biblia inayowataka watu wawe watumi au walokole bali wawe wanafunzi wa yesu na hawa wanafunzi wa yesu ndio kanisa lake hii ndio sababu hakuna andiko linalo tambulisha makanisa haya ya leo kuwa ninlanisa la mungu. jiulize hivi roamn liwe kanisa la mungu alafu mungu asilitaje kwenye biblia? kama alivyo wataja waisrael kuwa ni watu wake ?
Ngoja kwanza neno kanisa linakuchanganya "bila shaka neno lanisa ni kikundi cha watu wanao muamini na kumtumikia mungu" mfano mitume wale kwa kuunda kikundi kile chenye imani ya yesu ndio kanisa la mungu kanisa la mungu sio jengo,
kikundi cha watu wanaweza kukusanyika hata chini ya mti wakaunda kanisa kwahiyo kuna jengo la kanisa alafu kuna kanisa sasa,
hivyo jamii ya watu wenye ushuhuda wa yesu kwa kipindi hiki ndio kanisa la mungu wanahushuda wa yesu wanafanya yale yesu aliyo yafanya pekee, wanaamini yesu ndio njia na yeye aliishi bila dhambi duniani na hakuwa mroma au mlokole au msabato na kwasababu makanisa haya hayapo kwenye biblia ni wazi mungu hayatambui kama angeyatambua angeyataja.
Hongera sana kwa hoja hii, naamini utapata majibu ya unachotamani kukipata na kupunguza dukuduku yako.Ndugu zangu wa Kanisa kubwa duniani, Kanisa Katoliki - poleni sana kwa msiba mzito. Wakati maombolezo yakiendelea, naomba tuongee kiutu uzima; kwa heshima na upendo.
Kwanza ninawapongeza: mkiwa Kanisani, mnaonyesha heshima kubwa kwa Mungu. Sasa naomba mnijibu swali hilo: Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?
Nimesikia mnafundisha kwamba Mtume Petro ndiye aliyeteuliwa na Yesu kuwa msingi wa Kanisa au Papa wa kwanza. Mnanukuu Mathayo 16:18 na kusema kwamba katika Andiko hilo Yesu alimwambia Petro, βWewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu.β Kwa tafsiri yenu, βmwambaβ huo ni Petro mwenyewe, na hivyo mnamuona kama Papa wa kwanza. Mnaamini kwamba, mamlaka ya Petro kama kiongozi wa mitume yaliendelezwa na Mapapa waliomfuata, wakiwa viongozi wa juu wa Kanisa la Kristo duniani. Ni kweli?
Kama ni kweli, mbona mtazamo wa Kiprostestanti unatofautiana na mafundisho yenu. Waprotestanti wanasisitiza kuwa msingi wa Kanisa sio mtu binafsi, bali ni Yesu Kristo mwenyewe (1 Wakorintho 3:11), na kwamba βmwambaβ aliouzungumzia Yesu ni Yeye mwenyewe(Yesu) kama Petro alivyokiri: βWewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.β (Mathayo 16:16).
Kwa mtazamo wa Kiprostestanti, Petro hakuwa Papa, kwa sababu hakuna ushahidi wa kibiblia unaoonyesha kuwa alipewa mamlaka ya kipekee juu ya mitume wengine. Na wakati wa Kanisa la kwanza mfumo uliopo leo wa kipapa, haukuwepo.
Waprotestanti wanaeleza tena kwamba Viongozi wa kwanza wa Kanisa walifanya maamuzi yao kwa ushirikiano (Mdo 15), sio kwa mamlaka ya mtu mmoja(Papa). Wanasimama na Andiko la Waefeso 5:23 linalosema kwamba Yesu ndiye Kichwa cha Kanisa. Wanaamini pia kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayeliongoza Kanisa lote sasa, na sio kiongozi mmoja wa kimwili. Wananukuu Yohana 16:13
"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote."
Hoja hizo mnazijibuje?
Ntashukuru sana nikipata majibu ya swali langu na majibu kuhusu hoja hizo za Kiprotestanti. Majibu yajengwe kwenye Maandiko Matakatifu(Biblia). Tumsifu Yesu Kristo.
walikua hawasali kanisa kolote ila ndo ukristo ulivyoanza kama early comunityMitume walikuwa wanasali kanisa gani?
Makanisa yamekuwepo hata kabla ya Yesu.
Soma Biblia yako Matendo ya Mitume 11:26.
Mimi nilijua ni walokole kuuliza walokole wanawakana na kusema zile ni ministry au hudumaHivi hawa kina mwamposa na manabii sijui kiboko ya walozi kuna mwengine anajiita somebody lukulelo huwaga ni walokole au waganga wa jadi?
Maana unaweza kukuta hapa unabishana na mtu anayeamini ktk hao jamaa na huwa ni wa hovyo sana watu kama hawa huwezi ukawaelesha kitu wakakuelewa.
sasa ndo ujue hawakua sawa na ukisoma vizuri matendo ya mitume utaona petro alifanya maamuzi mbalimbali na ali play kama kiongozi wa wengineacha kueleza maandiko jinsi unavyotaka wewe, naona neno mtume linakuchanganya sana
Hebu fungua akili yako tafuta masna halisi ya neno mtume
Rudi kwanza uelewe hilo andiko, yesu aliwakusanya mitume nakuwafundhisha akawatuma waende kuwafundisha na wengine huku kuwafundisha na wengine ndio kuunda kanisa au kuunda wanafunzi wa yesu kama yesu alivyo waagiza hivyo yesu hakujifanyia flani kuwa kiongozi wa mitume kwenye biblia yeye aliwapa roho mtakatifu kila mmoja akafanye kazi hiyo na hawa mitume walifundisha mafundisho waliyo fundishwa na yesu na kuonya yale yesu aliyo waonya na sio mafundisho yao qenyewe.
Hii ndio maana halisi ya hilo andiko ulilo nukui Petro hakuwai kuwa kiongozi wa kanisa lolote lile au kiongozi wa mitume bali alitumwa na yesu akawafundishe wale wote watakao amini ndio kanisa lake na hakutumwa aende kufungua kanisa la rumi
sasa kufanya maamuzi ndio kuwa kiongozi kila mtu alifanya maamuzi una akili ndogo sanasasa ndo ujue hawakua sawa na ukisoma vizuri matendo ya mitume utaona petro alifanya maamuzi mbalimbali na ali play kama kiongozi wa wengine
sawa geniussasa kufanya maamuzi ndio kuwa kiongozi kila mtu alifanya maamuzi un akili ndogo sana
yesu na mitume nani mkubwa ? maana unazani labda mtume ni mtu flani wa ajabu sana ndio unavyozaniasawa genius
Wakatoliki hawana muda wa kubishana na wa protestant! Waprotestant wenyewe ni zao la wakatoliki, Wakatoliki ndiye Mama na Baba wa waprotestant. Hivyo wazazi hawana muda wa kubishana na watoto, ndio maana hata katika malezi watoto unakuta wanalia, wanataka hiki au kile mzazi anajua Cha kufanya!Waprotestanti nimewasikia kwa undani. Ila Wakatoliki sijasikia hoja zao kwa kina. Ndio sababu natafuta kusikia na kuthibitisha kutoka kwenye vinywa vyao wenyewe. Halafu kwa taarifa yako, Wakatoliki wanasema hata Mtume Petro alizikwa kwenye Kanisa lao, Vatican! Kama ni hivyo, hao si ndio wenye majibu mazuri ya maswali yangu?
Nimesikia pia kwamba baada ya Mtume Petro, Wakatoliki wanaamini kuwa Papa aliyefuata alikuwa Linus β ambaye anatajwa kama Papa wa pili (mnamo mwaka 67β76 BK).
Orodha ya Mapapa wa awali kwa mtazamo wa RC ni kama ifuatavyo:
Mtume Petro (c. 33β67)
Linus (c. 67β76)
Anacletus (au Cletus) (c. 76β88)
Clement I (c. 88β97)
Evaristus (c. 97β105)
Taarifa hizo sina uhakika nazo. Wakiniambia wenyewe na kunipa uthibitisho nitashukuru sana.