Je ni kweli watu wenye miguu isiyo na uvungu wanakataliwa jeshini? Kama ni kweli zipi sababu?

Jeshini kuna vigezo vya ovyo sana

Wacheza Kung Fu/kareti wengi tu wana miguu ya namna hiyo na wala siyo nongwa. Haya na watuambie wajeda huko jeshini na kwenye madojo tofauti ni nini katika swala la foot

Halafu siyo jeshini pekee ni sehemu nyingi tu kuna ujinga ujinga. Vitu vingine ni vya kurithi tu hakuna hoja yoyote ya msingi inayosimamiwa. Utakuta eti ni marufuku kazini kuvaa suruali ya mifuko ya kubandika, mifuko ya kulaza, jinsi, dera, msuli na kadhalika. Uliza sasa sababu uone maafisa watakavyojing'atang'ata
 
Kabla ya kuingia maabara ni lazima wapitie the recruit stage (mafunzo makali) ili kuujengea mwili uvumilivu
Si kweli , endeleeni ,
Wanajeshi wa Israel hufanya mambo yote mawili, ikiwemo mafunzo magumu ya mwili na vita ya kiteknolojia ya kisasa.

Mafunzo ya Mwili na Viapo
    • Hupitia mazoezi magumu ya kijeshi na sanaa za kupigana kama Krav Maga.
    • Kazi yao inajumuisha kuvunja matofali au mbao ili kujenga nguvu za kimwili na ujasiri wa kiakili.

Vita ya Kiteknolojia
    • Huwekeza sana kwenye maabara za kisasa na vitengo vya intaneti na mtandao.
    • Vitengo maalum kama Unit 8200 husoma na kupambana na vita ya kiteknolojia na kompyuta.
 
Vikwazo siyo kutembea au kukimbia tuu hata kupanda na kuruka high jumps bado ni kipengele
Lol imebidi nijitazame mguu wangu vyema

Uvungu ni nao bwana 😄😄😄

Mfano ikitokea vita watu kama sisi wenye miguu yenye uvungu breki ya kwanza utanikuta Misri 😄

Hao wasio na uvungu Kwa kuwa hawawezi kukimbia I bet wengi watafia kwenye milango ya nyumba zao
 
Flat foot haiwez kupitisha HEWA kwenda seheme ya chini ya mguu ambako kuna mishipa ya neva of which kuna effect yakee. Zipo sababu zingine pia.

Nakumbuka kuna jamaa babake alitoa pesa nyingi mwanaye apata nafas yes mwazo alipita but kweny Final inspection alipigwa chini kisa Flat foot.
 
Ukienda vitani misitu ya Congo ndani ndani huko dozi ikiisha nani atakuletea kwenye uwanja wa vita?

Kiufupi vitani inatakiwa uwe na kinga za mwilini zakutosha Sio uwe na upungufu wa kinga mwilini(VVU).

usije ukatufia katikati ya vita tuwe pungufu.
Ulivyoandika kwa maringo utafikiri umepima
 
Imethibitishwa kitaalamu kuwa hawawezi ama ni nadharia mkuu? Nifahamishe kwa hili
Uvungu ni kama shock-up (shock absorber); mtu akiruka, akibeba vitu vizito, uvungu husaidia kubalance weight.
Mtu akikimbia pia humsaidia kubalance weight na kumfanya aweze kukimbia umbali mrefu bila kuchoka.
Hivyo mwili ambao hauna shock absorber, huonekana sio imara sana kwa kazi zinazohitaji kutumia nguvu na kazi za sulba, japo wanaweza kufanya kazi nyingine za kawaida vizuri.
Ina maana kwa kazi kama za jeshi ambapo, kukimbia, kutembea umbali mrefu, kubeba vitu vizito ni jambo la kawaida; watu ambao hawana shock absorber huonekana kama wanakosa sifa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…