Wewe ndio kumbe hujui.
Simba na Yanga hazijawahi kuombeana mema kwa namna yeyote ile bila kujalisha ni katika ushiriki wa michuano ambayo inaweza kuitangaza nchi.
Kila timu ina hiyo spirit.
Hata wanaojitokeza hadharani kusema kwamba wanaiunga mkono Yanga au Simba kwa kigezo cha kuiwakilisha nchi, wengi hufanya kwa unafki tu sio kwa mapenzi ya kweli kutoka moyoni.
Utofauti unakuja ni kwenye njia zinazotumika katika kuonesha wewe huisapoti Yanga au Simba kwenye michuano ya kimataifa.
Kwa Simba utaona kabla na baada ya mechi wakionesha kutoitakia mema Yanga kwenye mechi yao ya kimataifa.
Hiyo inaitwa inderect
Lakini kwa Yanga utaona hilo lipo tofauti.
Kwani hadi viongozi wanahusika kama mpango kazi wa kuifelisha Simba.
Yanga ndio timu pekee ambayo viongozi wake waliwahi kwenda kuwapokea wapinzani wa Simba ili Simba ifungwe.
Yanga ndio timu pekee ambayo imewahi kuwatengea semina ya kuwapa mbinu wapinzani wa Simba ili waifunge Simba.
Yanga ndio timu pekee ambayo viongozi wao waliwahi kutoa shutuma za uongo kwa timu pinzani kuwa iwe makini na vyumba vya kubadilishia nguo kwa maana Simba hupulizia sumu.
Na jana tulisikia hizi tetesi za Jwaneng Galaxy kupokelewa hapo Kigamboni
Japo hiyo habari bado haijawa confirmed ila kupitia rekodi hizo hapo juu naona hilo linauwezekano mkubwa kuwa ni kweli.