Hatuui mada tuna expose ushamba wa Yanga.
Kuna baadhi ya vitu huwezi kushangazwa kuviona kwasababu vinafanywa na mashabiki.
Lakini kuona kiongozi wa juu kabisa wa Club anavaa hadi jezi ya timu pinzani huo ni ushamba
MABINGWA wa kihistoria Tanzania, Yanga
wameanzisha ushirikiano na klabu kubwa
ya Kaizer Chiefs, vinara wa Ligi Kuu ya
Afrika Kusini.
Hiyo ikiwa ni miezi michache imepita tangu
Yanga iingie udhamini na wadhamini wao
ambao ni Kampuni ya GSM Tanzania chini ya
Said Gharib Mohamed ambaye ni Rais wa
Makampuni ya GSM.
GSM hadi hivi sasa imeifanyia makubwa klabu
hiyo kubwa na kongwe nchini ikiwemo
kufanikisha usajili wa wachezaji watano katika
usajili wa dirisha dogo msimu huu.
Wachezaji hao ni kiungo fundi Mnyarwanda
Haruna Niyonzima, Muivory Coast Yikpe
Gnaimen, Tariq Seif, Adeyum Salem na Ditram
Nchimbi huku ikifanikisha kumshusha kocha
mpya wa timu hiyo Luc Eymael aliyetua jana.
Yanga kupitia wadhamini wao, Kampuni ya
GSM, walipata mwaliko kutoka Chiefs kwenye
sherehe ya kutimiza miaka 50 ya klabu hiyo
tangu ianzishwe nchini huko Afrika Kusini.
Katika sherehe hizo, Mkurugenzi wa Uwekezaji
wa GSM, Injinia Hersi Said, ndiye
aliyehudhuria tafrija hizo huku akipata nafasi
ya kutoa zawadi ya jezi ya Yanga yenye chata
ya GSM kwa baadhi ya viongozi.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata
Championi Ijumaa kupitia kwa Ofisa Habari
wa Yanga, Hassan Bumbuli alithibitisha hilo
kwa kusema kuwa: “Ni kweli Hersi alipata
mwaliko huo kutoka Chiefs katika sherehe ya
kutimiza miaka 50 ya klabu hiyo.
“Mengi wamezungumza na viongozi wa Chiefs
na kikubwa ni kujenga ushirikiano kati ya
klabu hizi mbili kwenye masuala mbalimbali
ya soka kati ya Yanga na Chiefs.”
Source: Globalpublishers