Je, ni kweli Yanga tunafanya hivi?

Je, ni kweli Yanga tunafanya hivi?

Tatizo la kuanza kushabikia mpira juzijuzi. Nataka nikupe taarifa maana hata nikikukumbusha sina hakika kama unajua. Kuna match ilichezwa ya Yanga na TP Mazembe mwaka kati ya 2014 hadi 16. Nenda kafuatilie nini kilitokea nje ya uwanja. Yanga alikufa goli 1-0. Msipende kujiona nyie wasafi sana hizi propaganda zolianza muda sanaa

Msipende kulalamika kwa uzushi wa mitandaoni kutokana na hisia binafsi za kinyangarakata mmoja. Mwishowe anabeba kijiji kizima mnaanza kuamini maneno yake
Yani unasema propaganda wakati video na picha zipo, kuna mtu kaweka video juu hapo mkipokea mashabiki ni uwongo huo ??
 
Yaani unaamini kilichoandikwa hapo?

Basi wewe huzijui vizuri timu za Kariakoo, Simba na Yanga ni mapacha wasioweza kuumizana linapokuja suala la kitaifa na hili mashabiki wengi wa miaka hii hawakijui...

Kama kweli Yanga iliwahost hao jamaa, basi ilikuwa ni makakati mahususi wa kimafia wa timu hizi za Kariakoo 😅, kuwaingiza mkenge hao wageni wakiamini wamepata rafiki kumbe ni tego...

Na kama wamekula vya Avic na walishaji ni Yanga, wajue wamekula vya Simba pia 😅
Umefunga mjadala
 
Kitu hiki nimetoka kukieleza sehemu. Mwaka Jana wakati Yanga anacheza Shirikisho dhidi ya TP Mazembe na Simba wanacheza Champion dhidi ya Wydad hapa Dar nilibahatika kukaa na timu ya Simba pale Hotelin Element Masaki.

Jioni nikawa napiga story na viongozi wa Simba kuelekea hizo Mechi. Walimieleza namna gani wameshirikiana kuelekea hizo mechi na namna gani wanafanya fitina nje ya uwanja ikiwemo kununua vyumba kwenye hotel zote za nyota 5 na kushirikiana na wenye hotel wa hapa Dar kiwanyima vyumba hizo timu iliyopelekea hizo timu kutoka nje kukosa hotel za hadhi na kwenda kuishi nje ya jiji.

Hao viongozi wana mikakakti ya kitaifa ambayo pia inaratibiwa na viongozi wa serikali na TFF. Kimsingi, sisi watanzania tangu enzi za ujana wangu tulikuwa tukilalamila namna tunavyofanyiwa fugisu tukienda cheza nje ya nchi na sasa jamaa wameamua kufanya finish kwa timu zinazokuja kucheza Tanzania. Haya ya kusema Yanga anaihujumu Simba ni ya wachambuzi uchwara ambao hawajui nini kinaendelea na wanatafuta attention tu.

Leo nchi kuingiza timu 2 ni mission ya kitaifa na haiwezi kuhujumiwa. Hao akina Kamwe, Hersi, Mangungu, Manara na Ahmed Ally nje ya media ni wamoja.
Na vipi pale Raisi wa TFF alipozionya timu zinazopokea wapinzani alikuwa muongo au ?
 
Jwaneng Galaxy ni timu bovu tu hatua ya makundi kafunga goli moja tu hiyo nayo ni timu..kwanza ilitakiwa icheze na lipuli au tra hakuna timu pale ya kubweka nayo..
Wachezaji wengi wa Jwaneng Galaxy hata uwezo tu wa kutuliza mpira mguuni hawana kipa ana kitambi kama afisa masurufi..
 
Yani unasema propaganda wakati video na picha zipo, kuna mtu kaweka video juu hapo mkipokea mashabiki ni uwongo huo ??
Ndugu mtu akisema propaganda maana yake ni mpango fulani unaandaliwa kwa ajili ya jambo fulani. Kwa maana hiyo hata ushahidi wa picha na video unaweza kuwepo ili ku emphasize kile kilichokusudiwa.

Propaganda sio habari ya uongo au udaku, ni uhalisia ila upo kwa ajili mlengo fulani. Uelewe hilo
 
Inatusaidia nini sisi? Haya kiko wapi? Na kama Simba wangeshindwa sisi tungefaidika na nini? Hizi ni roho za kichawi tu. Viongozi badilikeni acheni huu upumbavu.

Mwishoni wote tunaonekana tu vilaza.
View attachment 2922583
Kumbe na maana baada ya mechi kule Misri walirudi mapema kabla ya mechi yetu kuchezwa.Daaaah Mungu ni mwema tumemunywa shoga yao 6-0
 
Wakati Manara anawaambia wapinzani wa Simba wasiingie vyumbani wala wasiwashe AC naona ulikuwa kwenu Tandahimba huko hujaja mjini bado
Maskini AS-Vita Hadi walivalia Jezi zao Barabarani kwa kumsikiliza Minara Mitatu.
Walitishwa sana, hadi Maafisa wa CAF walishikwa na Butwaa maana Dactari wao hakuona dalili yoyote ya hujuma.

Walianzia kuwapokea wapinzani wa Simba Uwanja wandege.
Hadi hao wapinzani walipo wakatalia baada ya kuwaibi vitu vyao.

Tumewazoea.
 
MABINGWA wa kihistoria Tanzania, Yanga
wameanzisha ushirikiano na klabu kubwa
ya Kaizer Chiefs, vinara wa Ligi Kuu ya
Afrika Kusini.

Hiyo ikiwa ni miezi michache imepita tangu
Yanga iingie udhamini na wadhamini wao
ambao ni Kampuni ya GSM Tanzania chini ya
Said Gharib Mohamed ambaye ni Rais wa
Makampuni ya GSM.

GSM hadi hivi sasa imeifanyia makubwa klabu
hiyo kubwa na kongwe nchini ikiwemo
kufanikisha usajili wa wachezaji watano katika
usajili wa dirisha dogo msimu huu.

Wachezaji hao ni kiungo fundi Mnyarwanda
Haruna Niyonzima, Muivory Coast Yikpe
Gnaimen, Tariq Seif, Adeyum Salem na Ditram
Nchimbi huku ikifanikisha kumshusha kocha
mpya wa timu hiyo Luc Eymael aliyetua jana.

Yanga kupitia wadhamini wao, Kampuni ya
GSM, walipata mwaliko kutoka Chiefs kwenye
sherehe ya kutimiza miaka 50 ya klabu hiyo
tangu ianzishwe nchini huko Afrika Kusini.
Katika sherehe hizo, Mkurugenzi wa Uwekezaji
wa GSM, Injinia Hersi Said, ndiye
aliyehudhuria tafrija hizo huku akipata nafasi
ya kutoa zawadi ya jezi ya Yanga yenye chata
ya GSM kwa baadhi ya viongozi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata
Championi Ijumaa kupitia kwa Ofisa Habari
wa Yanga, Hassan Bumbuli alithibitisha hilo
kwa kusema kuwa: “Ni kweli Hersi alipata
mwaliko huo kutoka Chiefs katika sherehe ya
kutimiza miaka 50 ya klabu hiyo.
“Mengi wamezungumza na viongozi wa Chiefs
na kikubwa ni kujenga ushirikiano kati ya
klabu hizi mbili kwenye masuala mbalimbali
ya soka kati ya Yanga na Chiefs.”

Source: Globalpublishers
Kaizer Chiefs waliokuja kwenye tamasha lenu waliulizwa kuhusu Yanga wakasema hawaijui.
 
Ndugu mtu akisema propaganda maana yake ni mpango fulani unaandaliwa kwa ajili ya jambo fulani. Kwa maana hiyo hata ushahidi wa picha na video unaweza kuwepo ili ku emphasize kile kilichokusudiwa.

Propaganda sio habari ya uongo au udaku, ni uhalisia ila upo kwa ajili mlengo fulani. Uelewe hilo
 
Ndugu mtu akisema propaganda maana yake ni mpango fulani unaandaliwa kwa ajili ya jambo fulani. Kwa maana hiyo hata ushahidi wa picha na video unaweza kuwepo ili ku emphasize kile kilichokusudiwa.

Propaganda sio habari ya uongo au udaku, ni uhalisia ila upo kwa ajili mlengo fulani. Uelewe hilo
Kwahiyo mlikuwa sahihi mlichokifanya ? Hivi mpaka Raisi wa TFF akemee bado utasema mipango ya ndani ni kuwa kitu kimoja ???

Kweli Yanga wenye akili wawili tu
 
I
Huyu mwamba anavyotema madini humu halafu ghafla mpira unakuja katikati na kumtemesha pumba kama hizi inasikitisha sana!!
Madini ukiyaona utayajua?

Kwanza ligi ya bongo unaujua na kuifatilia au ndio wale wadau wa big event?
 
Tatizo mnalazimisha hizi timu zipeane sapoti hicho ni kitu hakiwezi tokea, kila mtu apambane na hali yake.
Kwani nani aliyesema tunataka support yenu ? Nyinyi si ndio mliita press conference kuwa tuwe kitu kimoja ilhali nyinyi ndio vinara wa kupokea timu pinzani.

Tukiyasema haya mnapokea timu pinzani, wenzako wanakataa, tazama huko juu pumba walizokuwa wakitema.
 
Kwani nani aliyesema tunataka support yenu ? Nyinyi si ndio mliita press conference kuwa tuwe kitu kimoja ilhali nyinyi ndio vinara wa kupokea timu pinzani.

Tukiyasema haya mnapokea timu pinzani, wenzako wanakataa, tazama huko juu pumba walizokuwa wakitema.
Kuna haja gani ya kusema timu fulani inapokea timu pinzani.

Labda mnasahau Simba mlipokuwa mnawaspoti TP Mazembe enzi za Manji.

Pokeeni malipo na riba juu.

Simba ikifungwa ni furaha kwa Yanga, Yanga ikifungwa ni furaha kwa Simba.
 
Back
Top Bottom