Je ni sahihi kumuacha huyu mwanaume, au ni mvumilie huku naumia ?

upande wa pili upo wapi😅

Yaani ni janga kubwa
Wanawake pia ni sehemu ya tatizo. "Wanawake tunaweza" ni kauli mbiu ambayo ikitekelezwa bila hekima majanga kama haya hutokea. Wanawake wengi wanaojitwisha majukumu ya mwanaume pia huwa ni 'sifuri' nyumbani. Hilo pia huchochea mwanaume kutokuona faida ya kupambania familia yake na kudhani kwamba hana cha kupoteza asipowajibika kikamilifu kutekeleza majukumu ya ki familia. It's a sad reality.
 
Kwahy ulimuacha mkeo
 
Aisee mambo ni mengi sana
 
Na kitakacho nwokoa mwanaume ni kujitafuta upya, sio nje tuu.. Inabidi aanzie ndani ya nafsi yake
 
😂😂😂😂😂 Katika comment zote hii imenichekesha sana.

Kiukweli hiki nacho huwa ni kichaka cha kukwepa kuwajibika, wanaume ni wazuri sana wa kukwepa uwajibikaji, kwa jinsi huwa na assess maoni yao sehemu mbalimbali. Huna pakusemea kivipi? kukosa pa kusemea ni choice, watu wote hawa duniani kwanini ukose wa kuongea nae? Unaweza kuamua kuchukua speaker ukaongea hata stendi kwani utakamatwa kwa kosa la uhaini?

Kukosa pa kusemea ni kulinda ego zao, ego ya mwanaume ni ya muhimu kuliko kila kitu………….!
 
Nimekusoma tangu mwanzo unatumia hisia sana kwa ku refer past issues zako!
Muulize mwanaume yeyote mwenye akili timamu, alotafuta maisha kwa nguvu zake na sio waliorithi, walopewa mitaji au wanaofanikiwa kwa uchawa. Lazima atakueleza hii dark fase ni kitu gani.

Hata maakama inahuku kwa past, sidhani kama ni mbaya kuweka reference kwenye huu mjadala.

Just for the benefit of the doubt, wanaume ambao tumekua forged in fire matumizi ya hisia hua yanaishia kitandani. Tukitoka hapo ubongo una operate. We don't have any mental similarities with women, thats how you operate.
 

Fact​

 
Pole sana dada mm ni kijana wa kiume ila kwasasa nmebeba majukumu mazito ya mzazi wangu naye hataki kazi yeye ni kula kulala mm napamban kusomesha mdogo wangu na mengineyo hii inaumiza mno pole ila dunia Ina watu wakushangaza sana
 
Msaada niliompa ni zaidi ya milioni
Msaada ni msaada tu hata yeye alikupa. Huyo ni mumeo endelea kumpambania usimuache hewan kwenye hali hiyo. Kazi za viwandani kama huna moyo unakimbia kiukweli. We mzoefu kwenye biashara mjaribu upande huo labda anaweza kufanya jambo.
 
Yeye ndo aliniacha mimi, nilipitia wakati kama anaopitia mumuo sahizi. Akashindwa kuvumili

Msaada ni msaada tu hata yeye alikupa. Huyo ni mumeo endelea kumpambania usimuache hewan kwenye hali hiyo. Kazi za viwandani kama huna moyo unakimbia kiukweli. We mzoefu kwenye biashara mjaribu upande huo labda anaweza kufanya jambo.
Mtaji anapata wapi wa biashara bila kufanya kazi unahisi wanaume wote wanafanya kazi viwandan wanapenda ila unafanya kwa sababu maisha hayana huruma na kila kazi fanya kwa malengo ili utimize ndoto ya biashara unayotaka
 
Ukweli mchungu sana. Ndo maana ndoa za "wamama wa nyumbani" hua zinadumu sana.
 
Ni phase muhimu sana ambayo kila mwanaume hupaswa kupitia maana society will never give you any other chance.

Ukiyasema ni sawa na kuonesha kidonda, hata hawa wanawake wanaosema uyaseme will be first ones to use that against you

So inabidi upitie hiyo phase mbaya ya maumivu makali na ifike mahala ya kufanya ujione huna thamani then ukivuka sasa unakuwa unstoppable
 
Mtaji anapata wapi wa biashara bila kufanya kazi unahisi wanaume wote wanafanya kazi viwandan wanapenda ila unafanya kwa sababu maisha hayana huruma na kila kazi fanya kwa malengo ili utimize ndoto ya biashara unayotaka
Kufanya kazi yoyote mnaweza wanawake tu. Wanaume tuna mipaka ya kazi, hiyo ipo waze dada angu. Hata huyo anaefanya kiwandani ukimwambia awe bodaboda anaweza akakugomea kabisaa mpaka ukashangaa. Au umchukue mkaanga chips akawe saidia fundi.
 
Kukosa pa kusema sio choice, hiyo ni survival mechanism katika jamii iliyo normalize masculinity kuwa strong
 
Kufanya kazi yoyote mnaweza wanawake tu. Wanaume tuna mipaka ya kazi, hiyo ipo waze dada angu. Hata huyo anaefanya kiwandani ukimwambia awe bodaboda anaweza akakugomea kabisaa mpaka ukashangaa. Au umchukue mkaanga chips akawe saidia fundi.
Hujui mana ya uanaume ww uchague kazi na hujui unakula nn bado hujapatwa na shida ukipatwa na shida hata legend utabeba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…