Je, ni sahihi kwa majaji kuvaa mawigi ya kikoloni katika zama hizi?

Je, ni sahihi kwa majaji kuvaa mawigi ya kikoloni katika zama hizi?

Mzee umeona hao majaji tu? Tena mavazi?

Mfumo wa Bunge, ni wa kikoloni, anavyovaa spika vazi lake pamoja na kanuni karibu zote pale ni za kikoloni, mavazi ni ya kikoloni, dini zetu ni za kikoloni, ujenzi wa nyumba na miundombinu ya kisasa ni za kikoloni, rasilimali tunazoringia mfano madini ya almasi ama dhahabu ni wakoloni ndio wamefanya hadi tunaona yana thamani, mfumo wa mawasiliano ni wa kikoloni...mbona ume target hao majaji tu?
Suala ni weupe wa nywele, huitaji kuambiwa kujua kwamba ni symbol ya ukoloni
 
Hoja ya mtoa mada ilikua nzuri sana ila watu wameipindisha sijui kwanini?

Mada ni kuvaa mawigi katika mahakama zetu na sio sijui smartphones, sijui nguo...

Utumwa umetuathiri sana.
 
Kwani serikali ni nini mpaka useme ile haikuwa serikali, utumwa mbaya sana aisee, nakuhurumia kwa jinsi ulivyoipiga ganzi akili yako
Mbona unapaniki hovyo??

Nimekwambia usiondoe wigi tu.

Ondoa kila kitu kuanzia bunge, serikali kuu, shule, mavazi yako, dini, na kila kitu ulichonacho.

Ninyi waafrika ni watu duni tu, hakuna hata kimoja kilicho chenu!

Eti utamaduni wetu?? Utamaduni gani?

Utamaduni wa kuchimba mizizi? Hahahaaa

Kichaa mmoja hapo juu ananiambia mkwawa alikuwa na serikali.

Mmestaarabishwa na kuwekewa namna bora za maisha na hao wazungu, halafu anakuja kichaa kama wewe kulilia "utamaduni"??
 
Aliyeanzisha technology ya mawasiliano ni mzungu hao wamekopi tu,.Nambie simu ya kwanza kuingia ilikuwa inaitwaje na ilitengenezwa wap
Kama wakileta simu zenye wigi jeupe la kizungu nitazipiga vita pia, ila kwa kuwa simu hazina wigi jeupe au ishara zinginezo za kikoloni, basi sina shida nazo
 
Hata lile sanamu la Askari lina symbolise ukoloni wa mababu zetu kwenda kupigana vita ya mkoloni, ni utumwa kuendelea kutukuza lile sanamu, ling'olewe pale! Bora hata awekwe diamond tu au baba wa taifa!
 
Acha wavae tu mbona sisi ni watu wa kucopy na kupest vitu vya wenzetu, hatunaga vya kwetu
 
Bora wavae hata migololo au mashuka ya kimasai?

Hapa tutaambiwa na wanajeshi wavae yale masempele ya jeshi la Mkwawa au Shaka Zuru
 
Mbona unapaniki hovyo??

Nimekwambia usiondoe wigi tu.

Ondoa kila kitu kuanzia bunge, serikali kuu, shule, mavazi yako, dini, na kila kitu ulichonacho.

Ninyi waafrika ni watu duni tu, hakuna hata kimoja kilicho chenu!

Eti utamaduni wetu?? Utamaduni gani?

Utamaduni wa kuchimba mizizi? Hahahaaa

Kichaa mmoja hapo juu ananiambia mkwawa alikuwa na serikali.

Mmestaarabishwa na kuwekewa namna bora za maisha na hao wazungu, halafu anakuja kichaa kama wewe kulilia "utamaduni"??
Hilo anzishia uzi, katika uzi huu jibu hoja iliyopo mezani, 'two rongs don't make it right'
 
Bora wavae hata migololo au mashuka ya kimasai?

Hapa tutaambiwa na wanajeshi wavae yale masempele ya jeshi la Mkwawa au Shaka Zuru
Jinsi unavyotaja hiyo migololo na mashuka ya kimasai kwa dharau inaonyesha jinsi ulivyoathiriwa na utumwa, unadharau kila kilicho chako na kutukuza cha former colonial master
 
Jinsi unavyotaja hiyo migololo na mashuka ya kimasai kwa dharau inaonyesha jinsi ulivyoathiriwa na utumwa, unadharau kila kilicho chako na kutukuza cha former colonial master
Sasa wewe...... hivi haujui hata hicho kiingereza uchwara unachokiandika hapa ni cha wakoloni???
 
Back
Top Bottom