Je, ni sahihi kwa mwanamke kunyonyesha hadharani?

Je, ni sahihi kwa mwanamke kunyonyesha hadharani?

Je wewe huwa unakula hadharani?
Kama jibu ni ndio basi jiweke kwenye nafasi ya mtoto anatakiwa kunyonya sababu ya njaa na yeye na mamaake wapo kwenye basi safari ya Mpanda kwenda Mwanza
Mama anatakiwa afiche au kufunika kifua chake pale anapo mpatia mtoto chakula hadharani
 
Kama hujui maana ya kujistiri basi nenda ukajifunze kwanza kuhusu hilo.
Amino nakwambia kujistiri ktk muktadha wa kufunika viungo vya mwili ni subjective. Kuna jamii ambazo mwanamke kuwekwa sura yake hadharani ni kutokujistiri.
 
Amino nakwambia kujistiri ktk muktadha wa kufunika viungo vya mwili ni subjective. Kuna jamii ambazo mwanamke kuwekwa sura yake hadharani ni kutokujistiri.
Jamii yetu ya kitanzania inajali heshima ya maumbile ya mwanamke
 
Ndio, maziwa hayatakiwi kuonekana na mtu yeyote, tofauti na mume wake
Kama kazungukwa na mume pamoja na michepuko yake Kama ishirini hivi,kuna haja ya kujificha?
Sidhani kama mtoto anatakiwa kunyimwa chakula chake,kisa maziwa ya mama yasionekane,hata hivyo unatamanije mariti yanayonyonyesha?
 
Mimi binafsi naona sio vizuri. Ikibidi ni vizuri amfunike mtoto wakati ananyonya... sio kuonesha nyonyo lote nje , huwa linawavutia baadhi ya wanaume kula chakula cha mtoto
 
Back
Top Bottom