Je, Niwaambie Wazazi Kazi Ninayoifanya !?

Je, Niwaambie Wazazi Kazi Ninayoifanya !?

FB_IMG_1791527792596.jpg
FB_IMG_1791527825773.jpg
 
Baada ya Kwenda Zanzibar na Kukosa kazi Kisa Usikivu Hafifu 😢, Nikaamua Kurudi Nyumbani Dar es Salaam, Hakuna Rangi Sikuiona Aiseee Masimango, Dharau za kila Aina, ila Nilivumilia tuu, Nikawa Naenda Kijiweni Natuliaa jioni Narudi Home...
Siku Moja Tupo Kijiweni na Washkaji Kuna Mdada Akaja Akawa anaongea na Mwenzetu "Nina Shughuli Mbagala Nitafutieni Wapiga Ngoma" Kumbuka hapo Mimi Sielewi Chochote Nipo Bize na Simu 😅 , Yule Jamaa Akanishika Bega akaniambia "
jamaa ; Dogo si Ulikuwa Unapiga Ngoma Zamani

Mimi ; Ndio ila zile ni Bendi za shuleni Za Shughuli Sijui wanapigaje,

Mdada ; Kama Ana kipaji Twende, Nitafutie na wazoefu watamuelekeza.

Jamaa ; Dogo Nenda na huyu Dada Shika na hii elfu 5 itakusave. Ngoja niwapigie Wakina Shabani Uende Nao.

Na Hapo Ndo Safari Yangu ya Upigaji Ngoma ikaanza
Kiukweli Nina Kipaji cha Kupiga Ngoma, Nilipoelekezwa siku Moja tuu Nikaelewa.

Hii Kazi inanipa Pesa ya kula Sikosi, Nimepanga Chumba, Nimenunua Godoro Na ndio kwanza Nina Miezi miwili Na Nusu Tuu....

Tatizo Linakuja Nyumbani wanataka wajue Ninafanya kazi Gani !? Maana Niliwaambia Nafundisha Pre- Form One ( Mimi Ni Mwalimu ) Kimbembe kinakuja wanataka waje Kazini kwangu Ninapofundisha 😂 kila siku nawakwepa tuu...

Wakuu Natokaje Hapaa !?
Je, Niwaambie au Nikaushe !? Maana Nyumbani ni watu wa Dini Na Mazingira ya hii kazi Nadhani Mnayaelewa....
Wakwepe mpaka wakujue kubwa huyu hataki tupajue anapo fanyia kazi .

Mpango kazi
Akikisha wanajua kubwa wewe hutaki wao wajue

All the best
 
Maana Niliwaambia Nafundisha Pre- Form One ( Mimi Ni Mwalimu )

Sasa kumbe wewe by pro ni mwalimu, kwa nini ulikuwa unaenda kushinda kijiweni na una taaluma inayoweza kukuingizia pesa?

Hivi wadau siku hizi hakuna ile mwalimu anafungua darasa la "tuisheni"?
 
Sasa kumbe wewe by pro ni mwalimu, kwa nini ulikuwa unaenda kushinda kijiweni na una taaluma inayoweza kukuingizia pesa?

Hivi wadau siku hizi hakuna ile mwalimu anafungua darasa la "tuisheni"?
Kufungua Kunahitaji Pesa Ndugu, Hata Hivyo Zanzibar kazi nilipata Bandarini hivyo Nilivyokosa kisa Usikivu nikawa kama Nimevurugwa hivii, yaani Sikuwa Sawa...
 
Kufungua Kunahitaji Pesa Ndugu, Hata Hivyo Zanzibar kazi nilipata Bandarini hivyo Nilivyokosa kisa Usikivu nikawa kama Nimevurugwa hivii, yaani Sikuwa Sawa...

Huenda wewe ni Gen Z...

Kipindi hichoooooo...maticha wa zamani walivyokuwa wanafanya, wanaenda maeneo ya shule za serikali sana za msingi sababu huwa zipo free wanafunzi wanatoka mapema, anachonga dili na mkuu wa shule ili aweze kutumia darasa moja au mawili aweke "tuisheni"...

Unamkatia chake mwl mkuu na pengine mlinzi wa shule kama yupo (walinzi ukiwatoa huwa wanasaidia hadi marketing)...

Ukikuza mtaji unaweza tafuta eneo la kupanga...

Kipindi hichooo watu wamesoma "tuisheni" kwenye mabwalo ya shule, pembeni ya mabanda ya mbuzi na mifereji michafu na sehemu nyingine za kukodi...

Hata baadhi ya makanisa yameanzia kwenye madarasa ya shule za msingi/sekondari leo hii manabii wao wanakula waumini nyomi....

Kipindi hichooooo
 
Hizo Ngoma unapiga ni zile za kupiga na stick au za kupiga na viganja vya mikono!? Kama ni hiyo ya pili je unapiga vile vingoma viwili vidogo au Yale makubwa ya bass? Kama ni hiyo ya pili basi usithubutu kumpiga mtu Kofi maana unamtoa meno.
 
Huenda wewe ni Gen Z...

Kipindi hichoooooo...maticha wa zamani walivyokuwa wanafanya, wanaenda maeneo ya shule za serikali sana za msingi sababu huwa zipo free wanafunzi wanatoka mapema, anachonga dili na mkuu wa shule ili aweze kutumia darasa moja au mawili aweke "tuisheni"...

Unamkatia chake mwl mkuu na pengine mlinzi wa shule kama yupo (walinzi ukiwatoa huwa wanasaidia hadi marketing)...

Ukikuza mtaji unaweza tafuta eneo la kupanga...

Kipindi hichooo watu wamesoma "tuisheni" kwenye mabwalo ya shule, pembeni ya mabanda ya mbuzi na mifereji michafu na sehemu nyingine za kukodi...

Hata baadhi ya makanisa yameanzia kwenye madarasa ya shule za msingi/sekondari leo hii manabii wao wanakula waumini nyomi....

Kipindi hichooooo
Naelewa Unachosema, ila Nimemaliza Chuo Mwezi wa 5, Zanzibar Nikaenda Mwezi wa Sita, Matokeo Yakatoka Mwezi wa 7 , Ngoma nimeanza Mwezi wa 8, Nilipotoka Zanzibar Nililifikiria Suala La Tuition na Kujitolea ila Sukuwa Sawa Psychological Nikasema Ngoja nitulie kwanza, Na Kijiweni Nilianza Kwenda Baada ya Maneno kuwa Mengi home...

Hata Hivyo Mwezi wa Kwanza 2027 Tunaanza internship ya Mwaka Mzima Hivyo nilitaka Shughuli ya kufanya Miezi 6 Tuu Wakati Nasubiri intern,, Kumbuka Nimesoma Mtaala Mpya Bro.

Mwisho Kabisaaa Licha ya kuwa Gen Z, Mimi Ni Kijana Mpambanaji Sana Na Naamini Maisha Nitatoboa Tuu....
 
MTU ANAETAKA KUJA KAZINI KWAKO KUPAJUA HUYO NI MCHAAAAWIIIIIII
 
Back
Top Bottom