Je, Rais Magufuli alikuwa na Pacemaker au Defibrillator? Ilidukuliwa?
hiyo makala niliisoma vizuri.
lakini kuna point moja umeruka sehem. kifaa hicho mawimbi yakeni mafupi mno kiasi kwamba mtu lazima awe so close kuweza ku access hiko kifaa.

but in real sense. the way rais alifichwa. ilikuwa ni ngumu sana. kama PM na mawaziri hawakujua.. nani angemsogelea rais zaid ya walinzi wake na madkatari wa usalama?

plus tanzania hatufikia uwezo wa hacking kiasi hiko. bado tuna safari ndefu.


all in all our late president aliondoka kwa tatizo la moyo. hizi theory sijui ilikuwa hivi ilkkuwa vile hazimrudushia uhai.
wanausalama walishatoa sababu. Apumzike kwa amani
Mara ngapi tuliona rais akijichanganya na watu , ni rahisi kitu hicho kutekelezwa iliyokuwa inasubiriwa ni timing tu
 
Jamaa afya yake ni mbovu siku zote. Kipindi cha kampeni alikuwa na mapumziko mengi, pia alikuwa akizungukwa na mashine za kiyoyozi.
Hamna mtu wa kudukua pacemaker yake
Kumbuka amekuwa na pacemaker/defibrillator kwa zaidi ya miaka 10. why now!
 
I have five theories:
1. Corona (uzembe)
2. Corona (uzembe)
3. Corona (uzembe)
4. Corona (uzembe/"external job")
5. Inside job

Binafsi kwa haraka ukiniuliza Lisu kapataje habari, test yangu ya kwanza itaanza na link ya JPM na Mch Msigwa........

Hii ya marekani/SA pengine ni spin tu kujaribu ku protect "sources"
 
Jitu limekufa kwa korona bado mnapamba pamba huku Samia na viongoz wengine wakitamba bila barakoa ili baadae mje na story zingine ikiwaondoa.
Watanzania imekuaje tumekua wajinga hivi??
Tuliambiwa na ''watoa siri'' kuwa Rais Magufuli amechanjwa ndio maana alikuwa anatamba bila barakoa!
 
Endeleeni kushupaza Shingo hivyo hivyo!



Tuvae barakoa! Tu-keep distance! Tunawe maji tiririka Bila kusahau matumizi ya vitakasa mikono inapobidi!

Marekani vifo vilivyorekodiwa vinaelekea kufikia laki 6 na wanavaa barakoa mbilimbili na huduma za afya zilizo bora kabisa duniani.

Museveni wa Uganda kasema hadharani aliongea na JPM siku ile ya kikao cha wakuu wa jumuiya ya EAC alfajiri mapema na JPM akamuambia anasumbuliwa na Acute Head Ache na akashangaa baadaye kwenye kikao yuko Samia Naibu wa Rais.

Msimpangie Mungu endeleeni kumtegemea Mungu hapo ndipo majibu ya kweli yalipo. Propoganda uchwara hazisaidii kitu chechote kiwacho kile.
 
I have five theories:
1. Corona (uzembe)
2. Corona (uzembe)
3. Corona (uzembe)
4. Corona (uzembe/"external job")
5. Inside job

Binafsi kwa haraka ukiniuliza Lisu kapataje habari, test yangu ya kwanza itaanza na link ya JPM na Mch Msigwa........

Hii ya marekani/SA pengine ni spin tu kujaribu ku protect "sources"
Inside job hii

Lakin inside job wali recruit external mafia
 
Hii mada ipo nje ya uwezo wako wa uelewa na uwezo wako wa kufikiri,ni vizuri ukajikita kua msomaji tu wa comments za wataalam au watu wenye uwezo wa uelewa wa mambo,

Sio kila thd inakuja hapa coz ya ushabiki,hii ni mada fikirishi inayohitaji utulivu na uelewa na sio tu kucomment kwa mihemko ya chuki ili na wewe uonekane umepinga ili upate kuchekewe na wenzako wenye uwezo mdogo wa kufikiri kama wewe.
Haha hahah haha.
Magufuli alikuwa a walking dead, hakuwa na afya, alikuwa very much short tempered, alikuwa na dalili zote za kufika ukingoni mwa maisha.
Pacemaker haikufanyi uishi milele.
Pia Magufuli hakuwa threat kwa dunia hadi wamuue.
Kama PSU walijua njia rahisi ya adui kumdhuru raisi ni kupitia kudukua pacemaker yake, walichukua tahadhari gani kuiwekea Artificial Intelligene security Ili Kama iki sense kwamba inaingiliwa itoe taarifa?
Waliiwekea backup system gani ili kama ikiwa hacked backup ifa ye kazi?
 
Hizi pacemaker huwa zahitaji kubadilishwa kila baada ya miaka 6 au 7 hivi.

Kuna risks za kutumia hivi vifaa bila kuchukua tahadhari.

1. Mgando wa damu kwenye sehemu ya kifaa hadi kwenye mkono ulio upande wa moyo. Kuna siku (hivi karibuni) akiwa kwenye ziara zake utamwona akiwa na bandage mkono wake wa kushoto.

2. Infection au au wadudu kushambulia sehemu iliyo na kifaa. hali hii hutokea miezi 12 tangu kifaa kipya kipandikizwe. Hivyo inawezekana kifaa kilipandikizwa miezi 12 ilopita. Moja ya dalili za infections ni joto kali na ndo ukaona feni yatumika kila mara.

Hii infection isiposhughulikiwa hupelekea mgonjwa kupata homa ya mapafu (Pneumonia) kuzunguka sehemu ya moyo na njia za damu kwenda kwenye moyo.

3. Kifaa hiki kikipandikizwa vibaya na kukawepo nguvu kubwa basi husababisha kuwepo njia za wazi (air leak) ambapo hewa hujipenyeza kwenda kwenye mapafu. Hapo ndipo huitajika upasuaji kuondoa hewa ya ziada.
Hivyo hupenyezwa kiwaya kidogo kutoa hewa na mgonjwa hutakiwa kukaa hospitali kama siku mbili hivi.

Moja ya hatari ya pacemaker kushindwa kufanya kazi yake sawasawa ni kukutana na miali mikali ya mvuto au magnetic fields.

Mgonjwa alieathirika na kushindwa kwa pacemaker kufanya kazi yake sawasawa ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa ya taratibu sana, kizunguzungu, kupiga kwikwi mfululizo na kupoteza fahamu na kuanguka ghafla.

Marehemu alikuwa akitumia kipoza hewa, na gari maalum kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza, na pia mmoja wa walinzi alianza kubeba kisanduku kidogo pengine kwa ajili ya kuichaji pacemaker.

Hivyo Pacemaker ni kifaa muhimu sana na kinahitaji watu ambao wanaelewa matumizi yake na utunzaji wake.

Naamini watu hao wapo na waliaminiwa kukitunza kifaa hicho.

Pia hospitali ya MOI huenda ina vifaa muhimu vya kushughulikia watu wenye pacemaker na kuhakikisha hawavurugi utaratibu mzima wa mstakabali wa kifaa hicho na hali ya mgonjwa.

Hata hospitali ya Mzena sidhani kama ina wataalam wa kushughulikia pacemaker.

Lakini pia siwelewi kwanini marehemu hakupata nafasi ya kubadilishiwa kifaa ambapo sasa hivi hukohuko walikoweka vifaa vya mwanzo, sasa hivi wanatengeneza kifaa hicho chenye umbo la dawa ya kidonge.

Kifaa hicho kipya hupandikizwa moja kwa moja kwenye moyo na hutumia wireless technology ambapo kukiprogram inakuwa rahisi na pia kunazuia infections ambazo husababishwa na kupandikizwa kifaa cha zamani ambacho hutumia nyaya.

Tukija kwenye suali lako lina possibilities mbili:

1. Ugonjwa wa UVIKO-19

2. Mwingiliano wenye vurugu ambao unaathiri utendaji kazi wa kifaa.

RIP John Pombe Joseph Magufuli.
 
Back
Top Bottom