Hizi pacemaker huwa zahitaji kubadilishwa kila baada ya miaka 6 au 7 hivi.
Kuna risks za kutumia hivi vifaa bila kuchukua tahadhari.
1. Mgando wa damu kwenye sehemu ya kifaa hadi kwenye mkono ulio upande wa moyo. Kuna siku (hivi karibuni) akiwa kwenye ziara zake utamwona akiwa na bandage mkono wake wa kushoto.
2. Infection au au wadudu kushambulia sehemu iliyo na kifaa. hali hii hutokea miezi 12 tangu kifaa kipya kipandikizwe. Hivyo inawezekana kifaa kilipandikizwa miezi 12 ilopita. Moja ya dalili za infections ni joto kali na ndo ukaona feni yatumika kila mara.
Hii infection isiposhughulikiwa hupelekea mgonjwa kupata homa ya mapafu (Pneumonia) kuzunguka sehemu ya moyo na njia za damu kwenda kwenye moyo.
3. Kifaa hiki kikipandikizwa vibaya na kukawepo nguvu kubwa basi husababisha kuweo njia za wazi (air leak) ambapo hewa hujipenyeza kwenda kwenye mapafu. Hapo ndipo huitajika upasuaji kuondoa hewa ya ziada.
Hivyo hupenyezwa kiwaya kidogo kutoa hewa na mgonjwa hutakiwa kukaa hospitali kama siku mbili hivi.
Moja ya hatari ya pacemaker kushindwa kufanya kazi yake sawasawa ni kukutana na miali mikali ya mvuto au magnetic fields.
Mgonjwa alieathirika na kushindwa kwa pacemaker kufanya kazi yake sawasawa ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa ya taratibu sana, kizunguzungu, kupiga kwikwi mfululizo na kupoteza fahamu na kuanguka ghafla.
Marehemu alikuwa akitumia kipoza hewa, na gari maalum kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza, na pia mmoja wa walinzi alianza kubeba kisanduku kidogo pengine kwa ajili ya kuichaji pacemaker.
Hivyo Pacemaker ni kifaa muhimu sana na kinahitaji watu ambao wanaelewa matumizi yake na utunzaji wake.
Naamini watu hao wapo na waliaminiwa kukitunza kifaa hicho.
Pia hospitali ya MOI huenda ina vifaa muhimu vya kushughulikia watu wenye pacemaker na kuhakikisha hawavurugi utaratibu mzima wa mstakabali wa kifaa hicho na hali ya mgonjwa.
Hata hospitali ya Mzena sidhani kama ina wataalam wa kushughulikia pacemaker.
Lakini pia siwelewi kwanini marehemu hakupata nafasi ya kubadilishiwa kifaa ambapo sasa hivi hukohuko walikoweka vifaa vya mwanzo, sasa hivi wanatengeneza kifaa hicho chenye umbo la dawa ya kidonge.
Kifaa hicho kipya hupandikizwa moja kwa moja kwenye moyo na hutumia wireless technology ambapo kukiprogram inakuwa rahisi na pia kunazuia infections ambazo husababishwa na kupandikizwa kifaa cha zamani ambacho hutumia nyaya.
Tukija kwenye suali lako lina possibilities mbili:
1. Ugonjwa wa UVIKO-19
2. Mwingiliano wenye vurugu ambao unaathiri utendaji kazi wa kifaa.
RIP John Pombe Joseph Magufuli.