Leo asubuhi nememsikia mtangazaji mmoja wa East Africa Radio (kwenye kipindi cha 12:00- 04:00) akisema Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa awamu ya sita. Yawezekana wengi wakawa na mtazamo huo, au wengi wakafuata mtazamo huo baada ya kumsikia mtangazaji huyo. Je, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, toleo la 20 Juni 2005, Rais wa sasa anamalizia awamu ya tano au anaanza awamu nyingine, yaani ya sita?
Je, awamu ya tano (phase 5) imekuwa na Marais wawili? Mmoja ameshika kipindi cha kwanza (1st term) na mwingine karibu kipindi cha pili (2nd term) kwa sababu yule wa kwanza amefariki dunia?
Ikumbukwe kuwa awamu moja ina vipindi viwili (one phase has two terms).
Je, mwanahabari huyo aliptitia katiba ya nchi kabla ya kuongelea facts?
Kwa mujibu wa ibara ya 40 (4), jibu sahihi la swali juu ya kuanza kwa awamu ya sita au la, ni kuwa Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan amefungua awamu ya sita. Hivyo ndugu mtangazaji alikuwa sahihi! Je, amebahatisha au alikuwa na uhakika?
Rejea ibara ya 37, kifungu cha 5.
Yaani hii nchi tunakwenda tu maana si katiba wala utaratibu vyote vinachanganya kwa kweli.
Ebu acha nikokotoe nione kama inakuja , tukianza na awamu ya hayati Mwalimu hii itakuwa ni ya kwanza lakini si kwa hesabu ya miaka maana utaratibu wa kikomo ulianzia kwa Mwinyi. Kwa maana hiyo awamu itategemea mazingira ya upatikanaji wa rais.
Kwa nini? Kwa sababu rais anapatikana kwa sanduku la kura ama kwa makamo kurithi kiti ikihitajika kufanya hivyo.
Hapa sasa ndio tuanze mjadala iwe ni wa kikatiba, utaratibu ama vyovyote itakavyo kuwa.
Nimesoma hapa kwamba baraza la mawaziri (serikali) inahesabika pia kama awamu, kama ni sawa basi tuanze na hesabu za karibu, je mzee kikwete aliongoza awamu (serikali) ngapi kwa kuwa alivunja baraza la mawaziri (serikali).
Na kwa mfumo huo huo wa baraza la mawaziri (serikali) tunajua adi sasa hivi ni baraza lile lile la awamu ya 5.
Sasa inakuaje rais awe ni wa awamu ya 6 lakini serikali yake ni ya awamu ya 5?
Tukikubaliana kwamba mama Samia ni rais wa awamu ya 6, je muhula wake wa kwanza ni miaka mingapi kwa mujibu wa katiba/utaratibu? Na ni mawaziri gani wameapa mbele ya rais ili kuunda baraza la mawaziri (serikali) awamu ya 6?
Sasa nimalizie kwa maoni yangu binafsi:
Mama Samia ni rais wa 6 wa JMT katika awamu ya 5, kwa sababu urais wake si wa uchaguzi wala si wakuanza awamu, bali ni wa kurithi kiti kilicho achwa wazi kufuatia kifo cha rais aliyekuwa madarakani. Kama ataitisha uchaguzi mpya hapo ndio angekuwa rais wa awamu ya 6. Lakini haja hitisha uchaguzi bali anaendelea na awamu ile ile ambayo uchaguzi wake ulisha fanyika. Kwa maana hiyo amerithi kiti cha urais na awamu ambayo ilisha anzwa na mtangulizi wake kwa miaka mitano na siku 114.
Kwa mfano kama akiunda baraza jipya la mawaziri (serikali) ili awe rais wa awamu ya 6 itabidi tufute zile siku 114, yaani tubadilishe tarehe za uchaguzi mkuu ili kukamilisha kipindi chake cha miaka mitano.